Saturday 16 March 2013

[wanabidii] Re: FIDIA BARABARA YA SERENGETI-SERIKALI YETU INAWAZA NINI?

Bw. Maro!
Naelewa si vema kujadili suala ambalo lipo Mahakamani, lakini nimesikitika sana kusikia taarifa hizo kupitia kwako kuwa kuna NGO ambayo imetoa fedha kwa baadhi ya wananchi wa serengeti, ili wasidai barabara!

Naweza kusema kuwa huo ni ulaghai na utapeli ongeza usaliti dhidi ya wana serengeti! Maendeleo bila miundo mbinu ya barabara? Hata mtoto wa chekechea hawezi kudanganyika na upumbavu wa aina hiyo!

Katika shauri hilo, ni nani anayewawakilisha wakazi wa serengeti? Naomba hao walioandika proposals na kilaghai na kuchukua fedha za wazungu kwa maslahi yao binafsi, huku wakiwadanganya kuwa wamezitoa kwa wakazi wa serengeti, wakome kutumia fursa hiyo kutunyima maendeleo yetu na vizazi vyetu! Wakumbuke iko siku tutalazimika kuwatoa kafara kama wakina Ken wa Jimbo Ogoni huko Nigeria!

Tunaomba serikali yetu iendelee na mchakato wa mradi huo wa ujenzi wa barabara, huku serikali ikihakikisha haki za watu waliofuatwa na barabara na kufanyiwa tathmini ya mali zao, wanapata haki zao kwa mujibu wa sheria!

----------
Sent from my Nokia phone

------Original message------
From: Yona Maro <oldmoshi@gmail.com>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, March 16, 2013 8:15:33 PM GMT+0300
Subject: Re: [wanabidii] RE: FIDIA BARABARA YA SERENGETI-SERIKALI YETU INAWAZA NINI?

Ndugu Mairi

Hili suala liko mahakamani na waliopeleka suala hili mahakamani ni NGO moja
ya nchi jirani ambayo imefadhili miradi kadhaa ya maendeleo kwa wananchi
wanaoishi karibu na maeneo ambayo barabara inategemewa kujengwa ili
wasiweze tena kudai hiyo na pengine hata kuuonyesha ulimwengu kwamba
maendeleo yanawezekana bila barabara hiyo kupitishwa mbugani , Sasa tuache
sheria ichukuwe mkondo wake .

2013/3/16 <chachamairi@gmail.com>

> Naomba kuweka hoja hii wazi mbele ya Wanabidii, ili kupata mtazamo wa
> watanzania wengine, na labda kupata ushauri nasaha kwa pande zote husika.
>
> Awali, nitoe maelezo kuwa, mnamo mwezi Julai 2010 ilifanyika tathmini kwa
> Wananchi waliokuwa wameguswa na mradi huo wa barabara kwa nyumba zao na
> mali nyingine kuwekewa alama ya X kama ishara kuwa sasa hawaruhusiwi
> kufanya maendelezo ya aina yoyote ikiwemo ukarabati wa nyumba!
>
> Wakati huo, yalitolewa maelekezo kutoka kwa viongozi kadhaa wa kitaaluma
> na kisiasa kuwa, fidia ingelipwa ndani ya kipindi cha miezi sita.
>
> Kwa niaba ya waathiriwa wa mradi huo wa barabara, nasikitika kuandika
> kuwa, mpaka sasa hakuna fidia iliyolipwa, na hakuna maelezo wala maelekezo
> kutoka kwa viongozi wataaluma na wasiasa kwa waathiriwa nini cha kufanya!
>
> Linalosikitisha zaidi ni kuwa, baadhi ya nyumba sasa zimeanza kutengeneza
> nyufa na kuanguka, huku wenye nazo wakiogopa kuingia gharama ambayo
> haitambuliki na tathmini iliyokwisha fanyika mwaka 2010!
>
> Wanabidii wenye taaluma ya sheria, naomba waone umuhimu wa kuwashauri
> wahusika wa pande zote, yaani serikali itoe tamko juu ya mradi huo na
> tathmini hiyo. Aidha, watoe ushauri kwa waathiriwa nini cha kufanya ili
> kutetea haki zao ambazo kwa sasa zimecheleweshwa, kitendo ambacho ni sawa
> na kuzipoteza!
>
> Naomba kuwasilisha!
>
> ----------
> Sent from my Nokia phone
>
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>
>


--
www.wejobs.blogspot.com Jobs in Africa
www.jobsunited.blogspot.com International Job Opportunities
www.naombakazi.blogspot.com

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.



--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment