Saturday 16 March 2013

[wanabidii] RE: FIDIA BARABARA YA SERENGETI-SERIKALI YETU INAWAZA NINI?

Naomba kuweka hoja hii wazi mbele ya Wanabidii, ili kupata mtazamo wa watanzania wengine, na labda kupata ushauri nasaha kwa pande zote husika.

Awali, nitoe maelezo kuwa, mnamo mwezi Julai 2010 ilifanyika tathmini kwa Wananchi waliokuwa wameguswa na mradi huo wa barabara kwa nyumba zao na mali nyingine kuwekewa alama ya X kama ishara kuwa sasa hawaruhusiwi kufanya maendelezo ya aina yoyote ikiwemo ukarabati wa nyumba!

Wakati huo, yalitolewa maelekezo kutoka kwa viongozi kadhaa wa kitaaluma na kisiasa kuwa, fidia ingelipwa ndani ya kipindi cha miezi sita.

Kwa niaba ya waathiriwa wa mradi huo wa barabara, nasikitika kuandika kuwa, mpaka sasa hakuna fidia iliyolipwa, na hakuna maelezo wala maelekezo kutoka kwa viongozi wataaluma na wasiasa kwa waathiriwa nini cha kufanya!

Linalosikitisha zaidi ni kuwa, baadhi ya nyumba sasa zimeanza kutengeneza nyufa na kuanguka, huku wenye nazo wakiogopa kuingia gharama ambayo haitambuliki na tathmini iliyokwisha fanyika mwaka 2010!

Wanabidii wenye taaluma ya sheria, naomba waone umuhimu wa kuwashauri wahusika wa pande zote, yaani serikali itoe tamko juu ya mradi huo na tathmini hiyo. Aidha, watoe ushauri kwa waathiriwa nini cha kufanya ili kutetea haki zao ambazo kwa sasa zimecheleweshwa, kitendo ambacho ni sawa na kuzipoteza!

Naomba kuwasilisha!

----------
Sent from my Nokia phone

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment