Saturday 16 March 2013

[wanabidii] PBZ LTD YAONGEZA HUDUMA KWA WATANZANIA WA DIASPORA!

BENKI YA WATU WA ZANZIBAR (PBZ Ltd) YAONGEZA HUDUMA KWA WATANZANIA WA DIASPORA!

The PBZ Managing Director, Mr Juma Amour Mohamed
 
Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ Ltd) ambayo ni benki pekee yenye makao makuu yake Zanzibar na ambayo inamilikiwa mia kwa mia na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuja na huduma mpya yenye kuwawezesha Watanzania wanaoishi nje kuleta pesa nyumbani Tanzania kwa bei nafuu kuliko wanavyolipia hivi sasa kupitia kampuni za nje za kigeni za kutuma pesa.

Katika waraka ambao blog la Zanzibar Ni Kwetu wameuona, benki hio inawataarifu wana-jumuia wa Diaspora ya Watanzania huko Canada juu ya huduma hio na wanawataka wawajulishe Watanzania wengine wote wanaoishi nje, ili na wao wapate kufaidika.

Katika kufanikisha huduma hii Benki ya Watu wa Zanzibar inashirikiana na kampuni moja maarufu kutoka Uingereza inayoitwa World Remit ambayo Benki ya Dunia inadai kuwa bei zake za kutuma pesa kutoka nchi moja kuenda nyengine zipo chini.

Kwenye waraka huo Benki ya Watu wa Zanzibar inamuandikia rasmi Communication Director wa Zanzibar-Canadian Diaspora Agency (ZACADIA) Bw. H.S. Othman wa Toronto, Canada, kuwa,..."We are therefore kindly asking your Agency in the Diaspora to pass the message contained in this letter to all Tanzanians abroad, so that they could use the services of our local indigenous bank in Tanzania,...."

Mwakilishi wa Zanzibar Ni Kwetu kutoka Toronto, Canada, alilinganisha bei ya hudumu hii kwa kutaka kupeleka Tanzania viwango tofauti vya pesa kutoka Canada kupitia PBZ/World Remit na kampuni nyengine ya Western Union. Tofauti aliyoiona kama alivyoiwakilisha hapa chini itawastaajabisha wengi wanaowaletea jamaa zao na ndugu zao pesa kutoka nje.

AMOUNT FROM CANADA TO TANZANIA ($)
FEES CHARGED BY ONLINE REMITTING COMPANIES ($)
PBZ /WORLD REMIT 
WESTERN UNION 
1.
Up to  50.00
3.99
5.00
2.
50.00 – 75.00
5.99
12.00
3.
75.00 – 100.00
6.99
12.00
4.
100.00 – 150.00
7.99
20.00
5.
150.00 – 300.00
9.99
25.00
6.
300.00 – 500.00
11.99
30.00
7.
500.00 – 600.00
12.99
30.00
8.
600.00 – 995.00
13.99
40.00

Huduma hii yenye bei nafuu inapatikanwa online kwa nchi zote za European Union, Canada, Australia, New Zealand, etc na karibuni itapatikanwa katika USA.

Benki ya Watu wa Zanzibar inayo matawi tisa katika Tanzania nzima - mawili yakiwa mjini Dar Es Salaam na karibuni itafungua matawi mapya katika mji wa Mtwara na Mwanza, huku ikilenga kuwa na tawi katika kila jimbo la kule Bara.

Huduma hii ya kupeleka pesa inapatikanwa online kwenye address ya hapa chini:


Benki ya Watu wa Zanzibar inawashauri Watanzania wanaoishi nje kuitembelee hii site na kujiandikisha hata kama hawana nia ya kupeleka pesa nyumbani hivi karibuni. Ukijiandikisha mapema itakusaidia wakati wa dharura!

0 comments:

Post a Comment