Wednesday 20 March 2013

[wanabidii] Neno La Usiku Huu; Ni Lazima Tupande Mbegu!



Ndugu zangu,

Kwenye moja ya mashairi ya Marcelino Dos Santos wa Msumbiji  ( Pichani kulia) anasema; " We Must Plant".  Kwa maana ya tuna lazima ya kupanda.

Dos Santos hazungumzii kupanda mbegu za mahindi au mtama, bali kupanda fikra za kimapinduzi kwa wanajamii.

Ni Fikra zitakazowasaidia kutoka katika hali iliyopo na kwenda kwenye hali nyingine iliyo bora zaidi.

Na mwanadamu unafanyaje unapoamka na kukuta dunia unayoishi ardhi yake imeanza kumegeka na kuchotwa na bahari? Kuna niliyemwuliza swali hilo. Naye akanijibu;

" Huo ndio utakuwa mwisho wa dunia!" Aliyenijibu alikuwa amechoka kufikiri. Nilidhani amgetamka, kuwa angeanza kujifunza kuogelea. Maana, kwa kuogelea majini angeweza kukutana na kisiwa, au nchi kavu.

Wanadamu tumejaliwa akili ili tuweze kufikiri. Na kufikiri ndiko njia mojawapo ya kuiteka kweli. Kufikiri kunahamisha milima na hata kuiweka kando kuruhusu mwanga upite.

 Inakuwaje basi mwanadamu anapoacha kufikiri? Haya ya ya kuendekeza abrakadabra za Freemasons ni kielelezo cha Watanzania, kama ilivyokuwa kwa Babu wa Loliondo,  kuamua kuacha kufikiri. Ndiyo, kuna waliojifunika vilemba vya ujinga. Wako  gizani. Wanahitaji mwanga.
Ni Neno La Usiku. ( Pichani nilipokutana na Mjamaa mwenzangu, Marcelino Dos Santos, Nairobi , 2007)
Maggid Mjengwa,
Iringa
http://mjengwablog.co.tz

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment