Sunday 17 March 2013

[wanabidii] Neno La Leo; Na Tuyaishi Maisha Ya Kadiri...



Ndugu zangu,

DUNIANI hakuna miujiza katika kuyafikia mafanikio. Hakuna njia za mkato pia. Ni sharti tufanye kazi kwa bidii. Tusiwe ni watu wenye kutanguliza taamaa na hata kuwadhulumu wengine.

Tuyaishi maisha ya kadiri. Ni kwa kuyafanya yale yaliyo ndani ya uwezo wetu.

Maana, ni wachache duniani walioweza kufanya miujiza kama tunayoambiwa kwenye vitabu vya dini; Bwana Yesu yu miongoni mwa wachache hao. Tunasoma, kuwa Mafalisayo walimshangaa Yesu na mafanikio yake. Wakatamka; " Hivi ni Yesu huyu huyu mwana wa Joseph fundi Seremala!"

Naam, mwanadamu usitazame tu alipofikia sasa mwanadamu mwenzako kwenye safari yake. Jitahidi uangalie mwanzo wa safari yake. Alikotokea. Ndipo hapo utayapata ya kujifunza.

Papa Francis wa Kanisa Katoliki amefikia kiwango cha juu cha mafanikio kwenye ngazi ya kanisa. Ni rahisi kumwangalia hapo alipo, lakini ni muhimu kuiangalia safari yake ilipoanzia.

Tunasoma leo, kuwa Papa Francis ni mtu wa kadiri. Muda wote wa uhai wake amejitahidi kuishi maisha ya kadiri. Papa si mtu wa makuu. Na kule Vatican wanashangazwa hata na mavazi yake yasio gharama kubwa, ikiwamo viatu pia.

Hapa kwetu Tanzania Julius Nyerere ni mfano wa viongozi walioishi maisha ya kadiri. Mwalimu aliishi kama alivyohubiri. Ni mfano wa kuigwa.

Ni Neno La Leo
Maggid Mjengwa,
Iringa
http://mjengwablog.co.tz/

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment