Monday 11 March 2013

[wanabidii] MRADI WA BENKI

Wanabidii,

Habari za siku nyingi,

Napenda kuwafahamisha wote kwamba baada ya kupata muitikio mdogo kwenye mradi wa benki tumeamua kuwekeza katika kampuni ya kuagiza mafuta masafi (refined white petroleum products). Maandalizi yako tayari ikiwa ni pamoja na usajiri wa kampuni.

Wale wote waliochangia mradi wa benki fedha zao ziko salama. Ni kama shilingi 1.1 milioni. Kama watakubali kuwa wanahisa wa kampuni hii ya mafuta tutawashukuru sana kuliunga mkono wazo hili.

Kwa wale waliokuwa wamejiorodhesha kuwa wanahisa wa kwanza wa benki tungependa kusikia mawazo yao kama wako tayari kujiunga na kampuni hii ya mafuta.

Kumbuka: Mradi wa benki bado haujaachwa. Umesimamishwa kwa muda. Baada ya kuisimamisha kampuni ya mafuta tutakuwa tayari kwa ajili ya kuendelea na wazo la mradi wa benki.

Mnasemaje?

Peter

0 comments:

Post a Comment