Friday 8 March 2013

[wanabidii] Kwa Wakenya Ni Ushindi Wa Mfumo

Ndugu zangu,

Naziona ishara za sisi Watanzania kufunga safari kuelekea kule jirani zetu wa Kenya walikotoka. Wakenya wa sasa wametokea kwenya machafuko ya 2007. Wakajitafakari. Wakaanzisha mchakato wa kufanya mabadiliko ya kimsingi yaliyopelekea kupata Katiba yao mpya na ya wananchi ya 2010.

Matokeo ya Uchaguzi yanayotarajiwa kutangazwa usiku huu ni USHINDI MKUBWA kwa Wakenya wote. Ndio, Wakenya wote watakuwa wameshinda, maana, kitakachotokea usiku huu ni ushindi wa mfumo. Wakenya sasa wanaonekana kuwa na imani na mfumo.

Kwamba vyombo vya umma vilivyoundwa ni kwa ajili ya kuutumikia umma wa Wakenya na si chama wala kikundi cha watu.

Kama Watanzania tusipokuwa makini kwenye kuyafanya mabadiliko ya kimsingi kupitia Katiba yetu ijayo, basi, nahofia kuwa tutaelekea kule ambako ndugu na jirani zetu wa Kenya walikotoka; kwenye vurugu za 2007. Tafadhali Usininukuu!

Maggid Mjengwa,
Msamvu
0788 111 765
http://mjengwablog.co.tz/

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment