Monday 11 March 2013

[wanabidii] Kero na Ushauri kwa mnaotafuta kazi

Ninaomba niliweke hili wazi lakini ninaomba lisichukuliwe personal
zaidi, ni katika kuelimishana na kushauriana kwa mawili matatu
yanayoweza kuwa katika uwezo wetu.

Naumia sana ninapoambiwa au kusoma post za vijana wenzangu kuwa
wanatafuta kazi na hawapati au wana-apply sana na hawaitwi hata kwemye
interview hata moja.

Kama wiki moja iliyopita nilitangaza nafasi za kazi ambazo mimi
mwenyewe ninazi-monitor application zake (naomba ruhusa yenu nisifanye
reference ya tangazo hilo), tangazo langu lilikua na maelezo ya kina
sana juu ya taasisi yetu, aina ya kazi na mazingira ya utendaji kazi.
Kwenda mbele zaidi nilielekeza namna ya tutuma maombi kwa kirefu
zaidi, na nikatoa njia mbili tofauti za utumaji wa maombi kama moja
wapo ingekua na ugumu wake. Mwisho nikaweka namba ya simu pale chini
kwa lengo la kumsaidia mtu mwenye shida ya ziada kabisa (nashukuru
walionipigia kwa kutaka maelezo ya ziada).

KERO: Unaachaje kusoma tangazo ulielewe badala yake unapiga simu
kuniambia umeona namba yangu nikueleze tangazo linahusu nini? Ina
maana huwa tunaangalia contacts tu katika matangazo ya kazi? Mbaya
zaidi application procedure iko pale document za msingi unazotakiwa
kutumia zipo pale lakini bado unafanya unachojiskia wewe... kweli
mwajiri ahangaike kuiangalia application yako? Unakuta mtu ameombwa
ajaze application form na ipo pale unaweza kujaza online au
ukadownload ukajaza, lakini yeye kwa kujiamini kwake ANATUMA cv yake
then anakwambia "NAOMBA UNIFIKIRIE".. Unakuta mtu ana CV nzuri na
unahisi kabisa huyu mtu ni ASSET, lakini kama hajui hata namna ya kuji-
organize yeye mwenyewe, atamfanyia nini mwajiri labda?

Anyways, ninayo mengi ya kushauri vijana wenzangu katika kutafuta
ajira, lakini naombeni tuwe makini. Tusiwalaumu waajiri kwa kashifa za
UPENDELEO au KUJUANA. Kwa namna fulani sisi pia tunahusika
kujipunguzia alama katika ushindani. Katika soko la ajira la sasa
UMAKINI wa mtafuta kazi ni kitu ambacho kila mwajiri anaangalia tangu
siku ya kwanza. Niliweza kuwajibu baadhi kwa email zao kuwa wafuate
utaratibu wa kuomba, lakini naamini kabisa sio kila mwajiri ana muda
wa kupoteza na watu wasiojielewa.

---
andernormans

Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2NGE2JdVQ

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment