Wednesday 6 March 2013

[wanabidii] HASARA ZA MOTO ANALIPA NANI?

Ndugu Wanabidii
siku za karibu kumetokea ajali za mara kwa mara za Moto. Morogoro kulitoka moto uliojeuka kuwa sumu watu wakazirai hadi kupelekwa hospital. Mwezi huu pia viwanda kadhaa Dar vimelipuka kwa moto. Jana kiwanda cha Sunda investment na Hawk Security system navyo tulishuhudia vikiteketea.

Swali langu ni kwamba hizi hasara zinasababishwa na nani au nini, na ni nani atalipa na je anayepata hasara ni nani? Au inabaki kusemwa ni hasara basi?

Du, jamani nisaidieni; napatwa msongo mwili wa matukio haya!

0 comments:

Post a Comment