Tuesday 12 March 2013

[wanabidii] GARAMA KUMSOMESHA MWANAFUNZI KWA MWAKA NI SH. NGAPI?

Ndg wanabidii
wote mmeshuhudia anguko la kiwango cha Elimu Nchini kutokana na kufeli watoto zaidi ya asilimia 75 ya wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka Jana.

Hali hii inasikitisha kwa kila mtu mwenye mapenzi mema na Taifa letu la Tanzania.

Kwa kupitia mtandao huu ninaomba kama kuna anaweza kufanya mahesabu na kujua Taifa linatumia GARAMA GANI kumsomesha mwanafunzi kwa mwaka, na hatimaye kwa miaka 4. Kwa njia hii tunaweza kufungua macho ya Taifa na pia wanafunzi wenyewe wajue wameliletea Taifa hasara kiasi gani. Na pia itasaidia watu kujua gharama halisi za Elimu kwa kila mtoto. Kwa hali ilivyo sasa kuna hatari ya kudhani kuwa mtoto husomeshwa katika shule ya kata sh 20,000 kwa mwaka. Na hivyo kwa kidato cha 1 hadi 4 ni sh 80,000/-

Naomba anayeweza kufanya hesabu hizi atuwekee kwenye mtandao huu wa jamii. Au Wizara husika ifanya kazi hii.

Naomba kuwakilisha. 

Kessy

0 comments:

Post a Comment