Saturday 16 March 2013

Re: [wanabidii] Wazanzibari tuwe na subira, ushindi waja!

Hebu tuambie vizuri mataifa ya magharibi yanahusika vipi na vurugu za
makundi haramu ya kiislamu ya boko haram,al-shabaab na azawad
republican halafu unasema wazanzibar hawajui kutumia bunduki ? Hao
magaidi kina Ghailani walizaliwa mbeya siyo zanzibar, unajenga hoja za
kuvunja muungano. Jikite kwenye kero za huo muungano siyo kuingiza
mambo ya dini.

On 16/03/2013, Fakhi Karume <fkarume@gmail.com> wrote:
> *Na: Maalim Omar Sheikh Kisisyina*
>
> Kama kuna binaadamu ninaowaogopa zaidi duniani, basi ni Wazungu na watu wa
> jamii zao. Na ninaposema wazungu nakusudia watu wenye asili ya mataifa ya
> Ulaya, Magharibi na Israel zaidi. Katika woga wangu huu nawaogopa zaidi
> watu wa mataifa manne makubwa duniani, ambayo kama si mataifa hayo dunia
> ingekuwa nusu ya pepo. Mataifa hayo ni Uingereza, Ufaransa, Marekani, na
> Israel.
>
> Nayoaogopa mataifa haya kwa sababu hata mola muumba amesema kuwa
> tuwahadahari sana watu wa jamii hii katika Quran tukufu pale anaposema kuwa
> tusiwafanye marafiki mayahudi na manasara kwani wao ni maadui wa Mwenyezi
> Mungu na pia ni maadui wa Uislamu, na kwa hivyo tuwatahadahari sana. Hili
> ni agizo kutoka kwa Muumba wetu Subhanahu wataala.
>
> Bila shaka mwenyezi mungu hakatazi kitu kama hakina madhara makubwa kwa
> wale aliowatahadharisha au kuwakataza. Na kwa mintarafu hii ndugu zetu hawa
> wa jamii ya Wazungu kwa ujumla wao, hasa wanaotoka mataifa hayo manne ni
> miongoni mwa watu wabaya sana hapa duniani, tena si kwa sababu ya chuki
> zangu, bali kwa ushahidi wa Quran tukufu.
>
> Nimesema kuwa dunia bila mataifa hayo manne ingekuwa pepo ya dunia. Ni
> kweli. Kwa sababu hakuna maafa yoyote duniani yatokeayo ukitowa yale ya
> muumba mwenyewe, yanayotokea pasipo kuwa na mkono wao. Mfano mdogo ni
> ufisadi, fitina, vita, dhuluma, na uharibifu wa nchi na mataifa ya wenzao
> kwa visingizio vyao vya kifisadi na kinafiki.
>
> Ukichunguza fitina inayoletwa na watu hawa imepelekea maafa makubwa hapa
> duniani. Kwa fitina zao watu hawa, Somalia imefutika katika ramani ya
> dunia. Kwa ubaya wao watu hawa Iraq, Libya, Misri, na sasa Mali na Nigeria
> Kaskazini na hata sehemu kubwa ya mataifa ya Kiarabu yenye muelekeo wa
> Kiisalmu, yamefaitika na kuporomoka. Yote hayo kuna mikono yao.
>
> Kwa sababu ya fitina za watu hawa Afrika haipati viongozi wenye heri wala
> wa kimaendeleo kwani wao wana mchango mkubwa wa kutuchagulia mapandikizi ya
> vibaraka wataoksimama pale kama vikatuni vinavyoendeshwa kwa rimoti zao, na
> sio viongozi watakokuwepo kwa ajili ya kuwaletea wananchi wao maendeleo.
>
> Na hili tumeliona kila mahala ambapo kuna kiongozi anaesimama kwa ajili ya
> wananachi wake, wao hufika na kuleta fitina na kumuondoa au kuvuruga nchio
> hiyo. Iko wapi leo Libya na mtetezi wa Raia, Muammar Gaddafi? Na si huyu tu
> kuna Omar Bashir na wengineo wanafatia, na kila mwenye muelekeo huo hasa
> akiwa katika mataifa ya Kiislamu, huyo uhai wake uhesabiwa kuwa ni mfupi.
>
> Fitina za mataifa haya ni mkakati maalum unaopangwa na mayahudi na manasara
> dhidi ya nchi za Kiisalmu. Kwa mfano, hivi siku za makaribuni kumekuwa na
> harakati za wananchi wa Zanzibar kutaka kujikomboa na uonevu na dhuluma
> wanazoizpata dhidi ya Muungano. Juhudi hizi zimekuwa kubwa na zinaelekea
> kuzaa matunda.
>
> Kwa bahati nzuri au mbaya, matokeoa ya awali ya maoni juu ya katiba
> yanaonesha kuwa wanachi wa Zanzibar zaidi ya asilimia 60 wanataka Muungano
> wa mkataba. Jambo hili halikuwapendeza mataifa makubwa ambao kwa maksudi
> ndio wanaowapa nguvu wenzetu wa Muungano kule bara kwa kupitia mwavuli wa
> Ukanisa na udini kuitawala Zanzibar kwa kile wanachokihofia kuwa Zanzibar
> huru itakuwa ngome ya Ugaidi Afrika Mashariki.
>
> Hii ndio propaganda yao, na kwa vile Zanzibar kuna waislamu wengi hili
> linashadidiwa na kupaliliwa kwa fitina lukuki alimradi juhudi zetu za
> kujitawala zishindikane. Kuna mengi yamefanywa ili kututisha na kuturudisha
> nyuma ili tuogope na tusiendelee na harakati zetu za kuitetea nchi yetu.
>
> Moja ya hujuma inayofanywa hapa ni kuwadhibiti viongozi wa dini ya kiislamu
> wasifikishe ujumbe kwa wananchi na baada ya hilo kutosaidia sana kumekuwa
> na hujuma za kuwauwa viongozi wa dini kwa kupata kisa na sababu ya
> kuitangazia dunia kuwa Zanzibar kuna ugaidi.
>
> Wahenga walisema njia ya muongo fupi, pamoja na hujuma zote hizo ambazo
> zimelenga kuizamisha Zanzibar na kuinakamisha kwa mataifa maovu ya dunia,
> mataifa ambayo yapo kuidhibiti usilamu tu kwa nguvu zao zote, mafanikio yao
> bado ni madogo mno. Mungu haachi mja wake, pamoja na kuleta makachero wao
> hapa nchini kuchunguza na kuweza kupika majungu yao na hatimae
> waihalalishie dunia kuwa Zanzibar kuna ugaidi, kuna kila dalili kuwa njama
> zao hizi zimeshindwa.
>
> Kuuliwa kwa Padre Mushi, kwa mfano ndiko kulikopelekea kuletwa makachero
> kutoka nchi kubwa kubwa ili kuja kutafuta ithibati ya kile kilichosemwa na
> Waziri wa Muungano Dr. Nchimbi kuwa Zanzibar kuna Ugaidi na kwa hivyo kifo
> cha Padre Mushi ni ugaidi. Kauli hii iliyotoka kinywani mwa kiongozi mkuu
> asiye na marifa wala hekima, anapozidiwa na jazba za chuki za kidini na
> usiasa wa ukoloni wa Muungano dhidi ya Zanzibar, haikuwa kauli ya kupuuzwa
> na haikuwa na nia njema kwa Zanzibar.
>
> Kama nilivyokwishatangulia kusema Mungu hamfichi mnafiki na haachi mjawe,
> kuja kwa FBI hapa visiwani na hata kuja kwa wale makachero waliobobea
> kufuatilia kupigwa risasi kwa Padre Mkenda hakukubaini jambo lolote
> linalohusiana na Ugaidi huo. Ukweli ukidhihiri uongo hujikunyata. Siku
> aliyopigwa risasi na kuuliwa Padre Mushi, nilipitisha uchunguzi wangu mdogo
> na nikasema nje ya utaalamu, kuwa upelelezi wowote juu ya tukio lile,
> hauwezi kuwatia hatiani Wazanzibari wa kawaida na hasa Waislamu.
>
> Nilisema hivi kwa sababu, hakuna Mzanzibari muislamu anaemiliki bunduki
> wala mwenye uwezo wa kuitumia hata akipewa, hasa kuitumia kwa ufanisi
> mkubwa na ufundi uliotumika kumuuwa Padre Mushi. Nasema hakuna. Hakuna
> Mzanzibari wa kawaida anaeweza kutumia bunduki kwa shabaha kali kama vile.
> Pili, kama yuko huyo Mzanzibar basi si raia wa kawaida na wala hana
> mfungamano na msikiti wala uislamu.
>
> Hana mfungamano huo kwa sababu hapa kwetu wanaojua kutumia bunduki
> tunawajua, na wenye bunduki wanajulikana. Pia naamini kuna raia wanaojua
> kutumia bunduki na walionazo lakini hawatoki hapa Zanzibar bali huja kwa
> majahazi na maboti yanayoleta mkaa, bangi, na bidhaa nyengine kutoka bara
> na kupitia bandari zetu za mkokotoni, Kizingo na hata Malindi.
>
> Wakishakuingia nazo bunduki hizo huzitumia kwa haja zao wenyewe zisizohusu
> waislamu na harakati zao. Huu ndio ukweli ambao FBI na hao makachero
> wabobevu wanaojuwa na hawatausema maisha kwani lengo lao sio
> hili.Ninachosema kwa sasa nawaomba Wazanzibari wenzangu kutojishuhulisha na
> shuhuli zozote za hujuma kama hizi, na tubakie na msimamo wetu wa kudai
> haki yetu kwa amani na utulivu. Nusura ya mwenyezi Mungu na ushindi viko
> karibu, na inshaalwahu tutashinda.
>
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>
>

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment