Monday 25 March 2013

Re: [wanabidii] WAISLAMU TUSHIKAMANE WOTE?

Abdallah,
Umeyapata wapi haya tena?
Kiasi fulani maelezo yanakanganya.





Walewale.



From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
To: Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Monday, March 25, 2013 9:57 PM
Subject: [wanabidii] WAISLAMU TUSHIKAMANE WOTE?

3:103:-  WAISLAMU TUSHIKAMANE WOTE?
 
     Ni rahisi kusema lakini ni vigumu kuyafanya hayo.Nini sababu ya kuwa vigumu kufanya hayo hapo juu? Zipo sababu nyingi sana lakini nitaeleza zile ambazo ni muhimu kwa mujibu wa Qur-an Karimu.

     Sababu ya mwanzo kabisa ni Elimu,nimeizungumzia Elimu kwanza kwa sababu elimu ndio ufunguo wa maisha kwa mwanaadamu,kwa hivyo basi Elimu ikiwa sahihi itakuonyesha njia sahihi ya maisha,maisha ambayo amekusudiwa mwanaadamu kuishi hapa duniani na muumba wake ambaye ni M/Mungu ambapo akiishi kwa Elimu hiyo hapa duniani-Akhera atalipwa pepo kwa kuwa aliishi kwa maelekezo ya Elimu ya muumba wake.

     Suala hili la Elimu ni nyeti mno na hapa ndipo shetani alipofaulu kutufanya tuwe tofauti mpaka leo,umuhimu huu wa Elimu tumeuona kwa M/Mungu kumuamrisha Adamu pale alipotolewa ktk pepo na kuambiwa ktk sura ya (2:3),shukeni humo ktk ardhi utakapokujieni uongofu(Elimu) watakaoufuata hawatakuwa na hofu wala hawata huzunika,na pia umuhimu huo tumeuona ktk sura ya (96:1) hapo tunaona ya kwamba Mtume Muhammad(S.A.W) anaamrishwa juu ya kusoma (Elimu) ili apate kufanya vile anavyotaka Mola wake.
     Tukianzia hapa kwa Mtume tutatafuta maswali juu ya mada yetu,je? Mtume na Maswahaba zake walishikamana au la?Je,ni Elimu gani waliyosoma hata wawe pamoja?Nafikiri hapa maswali yote majibu yake ni kuwa mtume na maswahaba walishikamana wote pamoja ktk Uislamu.

     Sasa ni Elimu gani waliyotumia?Mtume alifunuliwa wahyi ndani ya Qur-an tukufu na akawafahamisha jamii ya waarabu,mayahudi na manaswara,ktk jamii hizi walipatikana waliomuelewa Muhammad hawa wakawa maswahaba zake na wakashikamana pamoja hata kuupigania Uislamu kwa mali na nafsi zao.Na wapo ambao  hawakutaka kumuelewa ktk jamii hiyo kutokana na mazoea ya yale waliyokuwa wakiyafanya, Mayahudi na Manaswara wao walikataa kwa sababu ya Elimu walizokuwa nazo(Elimu za wanazuoni wao).

     Kwa maelezo hayo tumeona kuwa ni Elimu gani iliyofanya mtume na maswahaba zake kushikamana vizuri,nayo si nyingine bali ni Qur-an aliyoteremshiwa Muhammad(S.A.W),swali.je,leo Qur-an haipo?Jibu Qur-an inasomwa lakini cha kushangaza bado tungali makundi makundi,Ansar,Sunni,Ahmadiyya,Ibadhi,tablighi,Shia,Kadiria na mengine mengi tu,wapi tumekosea?je kukosea huku kumetoka wapi?

     Tutaanzia mbali kidogo,tuanzie kwa Adamu na Ibilisi,wakati M/Mungu anamuambia Ibilisi na malaika msujudieni Adamu,Ibilisi alikataa na M/Mungu akamlaani Ibilisi na tena akamuita Shetani,kuanzia hapo Ibilisi alichukua ahadi ya kupoteza kizazi cha Adamu isipokuwa wale wacha –Mungu nao ni wachache tu.

     Kitendo cha Ibilisi kuwa mcha Mungu na baadae kufanya kosa la kiburi  na akalaaniwa kisha akachukua ahadi ya kupoteza wengine si chake peke yake,Qur-an inatuonyesha juu ya mayahudi na manaswara jinsi gani walivyopewa vitabu na wakawa waongofu kisha wakaasi na baada ya hapo wakachukua ahadi ya kumsaidia Ibilisi ya kupoteza wanaadamu,ndio Qur-an inaonya kupitia kwa mtume Muhammad(2:120),ni mila gani hizo za mayahudi na manaswara Qur-an inaonyesha (1)-waliwafanya wanazuoni waungu badala ya M/Mungu; (2)-walifanya urafiki na makafiri(waliokufuru)-Warumi);-(3)-walikuwa makundi makundi kama sisi tulivyo sasa na mengine mengi.

     Kwa hiyo kundi hili lililochukua ahadi ya kumsaidia Ibilisi alipokuja mtume Muhammad(S.A.W) walimkataa hali ya kuwa wanajua kama ni mtume wa M/Mungu,maswahaba walifuata vizuri maelekezo ya Qur-an wakashikamana vizuri hata M/Mungu akamsifu kama wao ni umma bora kwa kutokea.

     Kwa ufupi wa maelelezo ni kuwa tumeihama(tumeiacha Qur-an) ndio maana mayahudi na manaswara wametuingiza ktk mila zao,-Ni vipi tumeihama Qur-an(25:30) hapa bila kufikiria  huwezi kujua-kwani utasema sisi tunaisoma kila siku misikitini,majumbani,madrasa hata kwenye simu zetu pia.

     Tuliza akili hii ni sehemu muhimu sana,kuihama Qur-an ni kutoitumia ktk maamuzi ya vitendo vyetu tunavyovifanya kila siku,na ndio maana M/Mungu ameiita Qur-an ni hukumu(36:2) hata ukitazama kava la juu la Qur-an utaona aya hii (36:2).

     Inakuwa vipi hukumu(maamuzi)/maelekezo-mfano wewe una jambo unataka kufanya hufanyi mpaka uangalie Qur-an inasemaje na ikisha toa hukumu/maamuzi unafanya,hapo utakuwa umeifanya Qur-an ni hukumu/muamuzi wa jambo lako na unafanya hivyo maadamu Qur-an ni maneno ya M/Mungu utakuwa umemtii M/Mungu na ukimtii M/Mungu ndio umemtii Mtume Muhammad(S.A.W) kwa kuwa maneno hayo yamepitia kwake,hivyo ndivyo mtume na maswahaba walivyofaulu wakawa kitu kimoja.

     Sivyo tulivyo leo,mayahudi na manaswara wamefaulu juu yetu,badala yake tumebaki kusema tu waislamu tushikamane-tutashikamana vipi kila mtu na kundi lake,N.B-unapokuwa na kundi ,wafuasi wanakuangalia wewe na ndio maana tukasema wamewafanya wanazuoni wao ni waungu badala ya M/Mungu unamuangalia mwanazuoni wako ukaacha kuangalia M/Mungu(Qur-an) umekwenda na imani ya kiyahudi na kinaswara,tunapozungumzia wanazuoni sio mashekhe wetu,hawa wanakariri Elimu za wanazuoni hilo ndio kosa lao.Angalieni Qur-an ndio jibu.

     Ni vipi mayahudi na manasara wamefanikiwa kutuhamisha kwenye Qur-an na kutufanya tukufuru kama wao?,.walichofanikiwa ni kutufanya sisi tusiiangalie Qur-an kama hukumu(maamuzi) ambayo M/mungu ameyateremsha kwa mtume wake,bali tuangalie hukumu(maamuzi) ya wanazuoni kama walivyofanya wao.Na kwa hili wamefanikiwa kuanzisha makundi(madhehebu) mbalimbali kama walivyokuwa wao,walichotaka wao ni sisi kufuata mila zao kama M/mungu alivyotahadharisha ktk Qur-an surat Baqara (2:120).

     Maudhui hii ni muhimu sana ikiwa tunataka kushikamana kwa ajili ya dini ya M/mungu kama alivyoagiza M/mungu (3:103),hili ni suala la kielimu sana linahitaji fikra kali(Akili) tena safi,kinyume chake mshikamano hauwezi kupatikana  kamwe kama ilivyoshindikana.

     Elimu ya Qur-an ndio nguzo ya mshikamano,sio elimu za watu kwani mtume na sahaba zake hawakufuata elimu za watu(wanazuoni),nadhani hapa tunaweza kujiuliza swali kwa nini wanazuoni wasemwe hivi?,wanachotakiwa wanazuoni(watu) ni kuieleza na kuitazama Qur-an inasema nini?

     Hapa inabidi tulifahamu kundi kuu la wanazuoni,hili ni lile la kiyahudi na kinasara ambalo lilimkataa mtume na Qur-an na baada ya hapa likafanya jitihada kubwa sana ya kuwakufurisha wanaadamu wengine kwa makusudi kama walivyokataa wao kwa makusudi hali wanajua kuwa aliyopewa mtume ni haki(Qur-an),hili ni kundi baya kabisa la wanazuoni,kundi jingine la wanazuoni ni wale waliozolewa na upumbavu huo wa kiyahudi kwa kukariri elimu ya kiyahudi(fatwa) na kuiacha Qur-an isitoe hukumu ya mambo yetu tunayoyafanya.

     M/mungu ni mjuzi wa mambo ya nyuma yetu na mbele yetu na ndio maana kwa kujua kuwa watakuja watu wataiacha Qur-an akaonyesha lalamiko kupitia kwa mtume surat furqan (25:30) (fikiria vizuri),kwa hiyo makosa ya wanazuoni wetu wa karne ya 20-21 ni kukariri elimu za wanazuoni wa kiyahudi na kutoa hukumu(maamuzi)kwa jamii hali ya kuwa Qur-an ipo na ina hukumu(maamuzi) ya kitu gani tunatakiwa kufanya,huyo ndiye M/mungu lakini watu wengi hawajui,nasema hivi kwa sababu tumezoea kusema kwa kukariri "unatakiwa kila kitu umtangulize M/mungu bwana",neno zuri tena la kweli lakini matumizi yake hatujui kwa kuwa tumelisema kama kaseti iliyorekodiwa,kwa hiyo kumtanguliza M/mungu ni kuangalia Aya(maneno) yake yanasemaje kisha tekeleza kile kilichosemwa na M/mungu na Aya(maneno) ya M/mungu si mengine bali ni Qur-an.

     Kwa hiyo tukifuata kanuni hii tutafanikiwa kwa kitu kimoja kwani Qur-an ni hiyo hiyo dunia nzima na M/mungu ameahidi kuilinda{surat hijri- (15:9) },lakini sio kufuata fatwa za watu kwani kila mtu anafikira zake,na kwa kufuata kanuni hiyo tutakuwa tunamuabudu(tunamtumikia) M/mungu ktk sifa yake ya 
AL-HAKIM na kama tunavyojua hakuna hakimu asiyetoa hukumu(maamuzi) sasa ikiwa M/mungu ni                  
AL-HAKIM,hukumu yake ni ipi? M/mungu ametuonyesha hukumu kuwa ni Qur-an ktk (36:2) surat Yasin,na tukikataa hilo M/mungu hatuongozi,kwani ili M/mungu atuongoze lazima tuifanye Qur-an ni hukumu(maamuzi).

     Mfano:-wewe una tochi unataka ikumulikie njia halafu tochi ile umeishika tu bila kuiwasha itakumulikia? Kwa  hiyo kule kujua kuwa una tochi mkononi mwako ni sawa na kuwa na Qur-an mkononi,na kule kuiwasha tochi ili ikumulikie njia ni sawa na kuisoma Qur-an kisha ikuonyeshe la kufanya na unapofanya kitendo kutokana na kuisoma kwa kuielewa makusudio na malengo na sawa na kuifuata njia,basi kama utakuwa na Qur-an halafu unaisoma bila kuielewa imekueleza nini ni sawa na kuwa na tochi ambayo hujui matumizi yake itawezaje kukumulikia njia? Hapo utakuwa unajisifu kwa jamii kuwa na tochi nzuri bila faida.

     Kwa hiyo leo waislamu tumefanywa hivyo na mayahudi na manasara  kwa kuwa na kitabu bora cha Qur-an tena kitabu cha mwisho kwa walimwengu wote lakini hatukitumii,sasa kitawezaje kutuongoza njia?

Ndugu zangu waislamu huo mfano tuuzingatie kwa kuufikiria kwa Akili za ziada bila hivyo tumekwisha,kwani jamii ndio hiyo inakwenda na maji kwa kuzolewa na tamaduni za magharibi kwa kuzidi ktk maovu,haya ni mafanikio makubwa ya mayahudi na manasara ya kutufanya tukufuru kama wao.

     Tuacheni Elimu za kukariri ambazo zimetujengea mazoea ya kututumainisha na pepo na kurithiana kwazo,hata waliopita kabla yetu waliyakataa ya M/mungu kwa sababu ya Elimu walizokuwa nazo(angalia mayahudi na manasara walivyomkataa mtume)

     Bila ya kuyafikiria haya niliyoandika na kuyatia akilini(sio kuyajadili kwa Elimu zenu) hatuwezi kuwa kitu kimoja(kushikamana) na tusubiri adhabu ya siku ya mwisho.
     Mafanikio

     Turudishe maamuzi yetu kwenye Qur-an ili ituongoze na tupate radhi za allah(M/mungu),hivyo ndivyo alivyoishi(alivyofanya) mtume Muhammad(S.A.W) na swahaba zake,tuache kauli za kusema Qur-an haieleweki bila kauli za wanazuoni,kama haieleweki itaongoza vipi,hayo ni maneno ya mayahudi na manasara ili waingize lao,hali ya kuwa M/mungu amesema ameifanya Qur-an kuwa nyepesi kufahamika,je M/mungu ni muongo,hapana sio muongo,basi tuzisomeni Aya za Qur-an na kuzifikiria vizuri zitatoa majibu zenyewe.

     Mfano:-watu wanasema;aliambiwa soma,lakini M/mungu hakumuonyesha cha kusoma,hili ni kosa kubwa sana na ndio balaa zote za mayahudi na manasara zilipotengenezwa ili waingize ilimu zao za kupotosha,M/mungu anamuamrisha mtume ambaye hajui kusoma wala kuandika asome ktk surat (96:1) hapa mtume au hata wewe ungeuliza nisome nini? Si hujui?-jibu M/mungu anatoa kwa kumuonyesha mtume cha kusoma ktk surat kahf (18:27),hapa Amri imetolewa na M/mungu(Qur-an) na majibu ametoa mwenyewe sio wanazuoni ambao wanatuambia mtume amesema tusome elimu yenye manufaa(tungo tata),Aamrishwe yeye atoe maelezo yeye hali alikuwa hajui,mtume hakuwa na sifa ya kumtangulia M/mungu kwani alishaambiwa ktk sura ya (10:109),hii ni mbinu ya mayahudi na manasara kutuzibia ili tuwafuate wanazuoni badala ya M/mungu kama wao,hivyo ndivyo Qur-an ilivyo hutoa majibu,tafsiri na maelekezo yenyewe,na huyo ndiye M/mungu lakini watu wengi hawajui.

N.B:-Sifa ya AL-HAKIM ni moja ya sifa za M/mungu ni sifa muhimu sana kwa wale wanaotaka kumuabudu(kumtumikia) M/mungu,kwani bila sifa hii,basi zile sifa zote za M/mungu hazina kazi,hii ndio nguzo ya sifa zote za M/mungu ukiacha kuitumia sifa hii umeacha Uislamu na umemkataa M/mungu na dini yake na wewe ni Mshirikina.

     Mfano wa sifa hii ni kama baba mwenye nyumba halafu hana maamuzi(hukumu) nayo,je,ni sawa kuwa hivyo?,kwa hiyo hakimu yeyote lazima atoe hukumu na hukumu ya hakimu(M/mungu ni Qur-an (36:2) (Yasin),na ndio maana mtume Muhammad alipoelewa juu ya sifa hii alitoa tamko ktk sura (6:114),sasa ikiwa mtume anahakikisha kuwa hivyo,mbona sisi tunaodai kuwa wafuasi wake tuna mahakimu wa asiyekuwa M/mungu ktk mambo yetu? Yaani maamuzi ya vitendo vyetu hayafuati maelekezo ya Hakimu wetu ambae ni M/mungu ,ambayo anayatoa kupitia Qur-an (36:2),hii ni hasara kubwa na sisi tutakuwa sio wafuasi wa mtume Muhammad(S.A.W).
Umuhimu wa sifa ya AL-HAKIM

     Sifa hii ya M/mungu ndio sifa ambayo inakufanya wewe uitwe Muislamu,ni vipi?-muislamu ni mtu aliyejisalimisha kwa M/mingu,sasa ni vipi kujisalimisha? Nitatoa mfano:-kwa mtu aliyeshikwa na Askari akaambiwa nyoosha mikono juu,kwa hiyo baada ya mtu huyo kutii Amri ya askari huyo ya kunyoosha mikono juu anachosubiri ni amri nyingine,ikiwa na maana huna maamuzi ya kufanya chochote ila maamuzi(hukumu)yatoke kwa askari huyo,hapo unaitwa umejisalimisha kwake(Askari),nimetoa mfano huo kukuonyesha jinsi ya kujisalimisha.

     Kwa hiyo basi kusilimu kwetu ni kujisalimisha kwa M/mungu kwa kunyoosha mikono juu na kusubiri amri yenye hukumu(maamuzi) ya M/mungu ambayo ni (36:2),tukianzia kwa mtume Muhammad(S.A.W) baada ya kumfahamu M/mungu alitoa tamko ktk sura (6:114) na akala kiapo kikubwa  ktk sura ya 6:(161-162) hapo akawa anasubiri maamuzi ya M/mungu ambayo alionyeshwa kuwa ni (36:2) (Qur-an ni hukumu),kwa hiyo utaona hapa mtume aliweza kumuabudu(kumtumikia) M/mungu ktk sifa hii ya AL-HAKIM na akawa hana hakima mwingine wa mambo yake,maswahaba walimfuata mtume na wakamtii kwa kuwa walijuwa hukumu sio yake bali ni ya M/mungu,na kwa hali hiyo wakawa kitu kimoja na wakapigania dini kwa mali na nafsi zao,na M/mungu akawasifia kuwa wao ni umma(jeshi) bora kuliko yaliyopita,huo ndio Uislamu lakini watu wengi hawajui,hawajui vipi?tujiulize?,vipi M/mungu mmoja,kitabu kimoja,kibla kimoja-wote waislamu-makundi(madhehebu) ya nini?(fatwa za wanazuoni hizo).

     Kwa hali hiyo sisi sio waislamu kwa kuwa tumefuata mila za mayahudi na manasara rejea (2:120) na sura 30:(31-32) ,kwa hali hii mtume anaambiwa na M/mungu sura (6:159),na huu ni ushahidi tosha juu ya nafsi zetu kwa kuwa tukiulizwa mtume na swahaba zake walikuwa dhehebu gani?jibu la! Sasa haya yametokea wapi? Sura (2:120),hii ni mila ya kiyahudi na kinaswara fikirieni vizuri ili tuepukane na Ushirikina huo tuwe Waislamu kama alivyokuwa Mtume na Swahaba zake.

     Turudini ktk Qur-an hiyo ndio fimbo ya makafiri,mayahudi na manaswara ambayo mtume na Swahaba zake waliitumia,au tunasubiri kitabu kingine kisichokuwa Qur-an kiletwe na M/mungu?

     Qur-an ni ukweli na ukweli umefika uongo umetoweka na uongo ndio wenye kutoweka,hapo M/mungu amemaliza ujumbe wake kwa wanaadamu mpaka siku kitakaposimama kiyama,kwa hiyo hakuna jipya la mwanaadamu litakalotokea ulimwenguni ambalo M/mungu hajalizungumzia ktk Qur-an.

     Iamini(ikubalini) Qur-an ni kitabu cha ajabu,acheni kuifanyia mzaha kwa kui-challenge,kuiletea upinzani.

                            Wabillah Tawfiq,wenu ktkUislamu(Fikiria sana)
                                                         
                                                                         
N.B:- AKILI&MATAMANIO V/S MUONGOZO WA KWELI(QUR-AN).

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 


0 comments:

Post a Comment