Sunday 10 March 2013

Re: [wanabidii] Vita dhidi ya Malaria Tanzania

Dada Anna,

Tatizo la humu ni moja tu, kupenda mijadala controversial ya 'watu' na siasa badala ya ile ya hoja za maendeleo na harakati za kuleta ustawi wa jamii
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

From: anna nyanga <luguanna@yahoo.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sun, 10 Mar 2013 07:14:02 -0700 (PDT)
To: wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Vita dhidi ya Malaria Tanzania

HK, tumia fursa ya kuwa kwenye mwanabidii kuhamasisha kampeni dhidi ya ugonjwa wa malaria.  
Wadau wote muhimu wapo humu! be pragmatic



From: Hermengild Mayunga <drmayunga@gmail.com>
To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Sunday, March 10, 2013 10:50 AM
Subject: [wanabidii] Vita dhidi ya Malaria Tanzania

Shared News From Blog
http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2013/02/Kilele-cha-Mlima-Kilimanjaro.jpg

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Mlima Kilimanjaro unaweza kutumika
vizuri zaidi kwenye vita ya kupambana na ugonjwa wa malaria kwa
wanamichezo na watu mashuhuri kuupanda mlima huo na kuchangisha fedha
za kusaidia kampeni ya kupambana na ugonjwa huo.Alitoa kauli hiyo jana
usiku (Jumamosi, Februari 9, 2013) wakati akihojiwa na waandishi wa
habari mara baada ya kushiriki mjadala kuhusu juhudi za Serikali
katika kupambana na ugonjwa wa malaria uliofanyika kwenye kituo cha
mikutano cha Sandton, kilichopo jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

Alisema katika majadiliano yake na baadhi ya wajumbe walioshiriki
mjadala huo, wengi waliunga mkono wazo alilolitoa la kutumia Mlima
Kilimanjaro katika kampeni za kupambana na ugonjwa huo.

"Nimeongea na baadhi ya wajumbe katika hafla hii hapa Johannesburg,
wengi wameliafiki wazo la kutumia Mlima Kilimanjaro kutangaza
mapambano haya… kila mwanamichezo atakayepanda mlima huu atatangazwa
kwamba ameshinda vita dhidi ya malaria na fedha atakayochangisha
itatumika katika kampeni ya kupambana na malaria barani Afrika,"
alisema.

Alipoulizwa ni kitu gani cha tofauti alichojifunza katika mjadala huo,
Waziri Mkuu alisema jambo kubwa aliloliona ni jinsi ya kutumia mbinu
mbadala za kupeleka ujumbe kuhusu mapambano dhidi ya malaria. "Kila
mtu ana dhamana ya kuchangia vita dhidi ya malaria. Hawa wenzetu
wameitisha viongozi wa makampuni makubwa kutoka Afrika Kusini na nje
ya nchi hiyo, wako wadau mbalimbali jioni ya leo walioshiriki mjadala
huu," alisema.

Akitoa mfano wa Tanzania, Waziri Mkuu alisema tangu mwaka 2000 idadi
ya wagonjwa wa malaria imekuwa ikishuka lakini vilevile idadi ya
wafadhili wanaochangia jitihada za kupambana na ugonjwa huo nayo pia
imekuwa ikishuka. Ndiyo maana nimesema kuna haja ya kutumia wadau
wengine kama vile Bunge, NGOs na Serikali za Mitaa ili kuona wanaweza
kusaidia vipi katika vita hiyo," alisema.

"Wenzetu hawa, (akimaanisha – Muungano wa Mashirika ya Kimataifa
yanayopambana dhidi ya Ugonjwa wa Malaria – United Against Malaria
(UAM) wametumia mashindano ya AFCON kupeleka ujumbe wa kupambana na
ugonjwa huu unaoua watu wengi Afrika sababu ni moja tu: watu wengi
wanapenda mpira wa soka iwe uwanjani au kuangalia kwenye luninga kwa
hiyo wanajua fika kuwa ujumbe ukitolewa pale utawafikia watu wengi
sana na kwa haraka zaidi. Sisi Tanzania tulishaanza na sasa
tunaangalia uwezekano wa kutumia basketball, netball na michezo
mingine kufikisha ujumbe huu," alisema.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge wanaopambana na Malaria (TAPAMA-
Tanzania Parliamentarians Against Malaria), Bi. Riziki Lulida ambaye
alikuwa miongoni mwa wajumbe waliofuatana na Waziri Mkuu Afrika
Kusini, alisema Tanzania bila Malaria inawezekana na wao kama Wabunge
wanaweza kwenda vijijini kutoa elimu kwa wananchi jinsi ya kujikinga
na ugonjwa huo.

Naye Dk. Hamisi Kigwangalla ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa TAPAMA
alisema atatumia fursa ya kushiriki mjadala huo kama njia ya kujifunza
mbinu mbadala za kuishirikisha jamii kwenye vita dhidi ya ugonjwa wa
malaria. "Leo tumeona wenzetu wakiwatumia watu maarufu kama Yvonne
ChakaChaka, Mark Fish – mchezaji wa zamani wa BafanaBafana na pia
Drogba yuko kwenye matangazo yao kuhamasisha wananchi watumie
vyandarua kujikinga na malaria… sisi pia tunaweza kutumia wasanii na
wanamichezo wetu kuelimisha umma kuhusu mapambano dhidi ya malaria,"
alisema.

Naye Mbunge wa Chonga, Pemba, Dk. Haroub Mohammed Shamisi ambaye pia
ni mjumbe wa TAPAMA alisema ushirikishwaji mkubwa wa jamii kwenye vita
dhidi ya malaria umesaidia sana kushusha viwango vya maambukizi ya
malaria kule Zanzibar.

"Zanzibar imepiga kasi sana katika vita hii na sababu kubwa
iliyochangia ni ushirikishwaji wa karibu wa wananchi kwenye kampeni
dhidi ya malaria. Baadhi ya wabunge tuliamua kuungana ili tupeleke
ujumbe huu kwa wananchi kwa urahisi ili tuweze kufanikiwa kwa haraka
zaidi," alisema.


John Bukuku
MIMI NI MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA NA KUPITIA
BLOG HII NINA IMANI TUTAWEZA KUPEANA HABARI MBALIMBALI ZA BURUDANI
ZITAKAZOFURAHISHA NA KUELIMISHA NAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI TUWEZE
KUFIKA TULIPOKUSUDIA
--
drmayunga@ores.or.tz
admin@ores.or.tz
info@ores.or.tz
www.ores.or.tz
www.twitter.com/drmayunga
Tel +255 784 520680
Tel +255 25 2600419
Fax +255 25 2600352

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.




0 comments:

Post a Comment