Sunday 10 March 2013

Re: [wanabidii] URAIS 2015 - TANZANIA ITAWEZA KUMBEBA LOWASSA ?

James,


Sijakosana naye na huenda yeye hanifahamu kabisa! Usianze kubashiri uwezo huo anao Mungu peke yake.

Pili, soma hoja yangu kuhusu Urais kwenye nchi za kiafrika kujua impact yake kwa nchi za kiafrika. Rais ni kila kitu.

Kuhusu mtu kubadiolika; kwanza tumia kiswahili sahihi, neno "mbeleni ni tusi" sema " .... za mbele" jaji! Kubadilika kwa mtu unatofautishaje na andiko langu kuhusu majaribio tunayoyafanya nchi zetu za kiafrika kwenye uongozi? Tafakari.

Niongeacho hapa ni maoni yangu na sina ubaya binafsi na mtu! Naona umesema hivyo kwa kuzingatia tabia ya watu kama sisi waTz wachache wanaoangalia "nani kasema jambo" badala ya " uzito au wepesi wa hoja iliyosemwa"! Ni dosari zetu ambazo zinatunyina uwezo wa kuchambua mambo eti tu kwavile hili limesemwa na Magesa ambaye unamdharau!
------Original Message------
From: James Malima
Sender: wanabidii@googlegroups.com
To: wanabidii@googlegroups.com
Cc: wanabidii@googlegroups.com
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] URAIS 2015 - TANZANIA ITAWEZA KUMBEBA LOWASSA ?
Sent: Mar 10, 2013 16:28

Tony,

Huwa naheshimu sana mawazo yako. Lakini katika hili, nahisi kuna la zaidi ambalo mlitofautiana na Mh. Lowassa, maana huoni lolote jema alofanya. Umesema watu hubadilika, kwa nini usihisi huyu nae amebadilika au huenda akawa na positive changes zitakazoliletea taifa manufaa hapo mbeleni?

Kweli hali ya sasa inatisha. Mambo mengi yanakwenda tofauti kabisa. Wapo wanaosababisha lakini ukiwasikia wanavyoongea, utadhani hawahusiki kabisa.

Mungu atusaidie nchi hii. Hayo makundi, tusipoyadhibiti mapema, yanaweza kutusababishia matatizo tusiyoyatarajia.

Nitafarijika pale viongozi watakapokuwa na sauti na kutenda haki kama zamani. Siku hizi, maamuzi ni tofauti sana na uhalisia ulivyo. Kilichonitisha zaidi ni kuona umesema hata haki ambago tunaamini hutolewa na mahakama, huenda pia isipatikane kulingana na mtu unavyoonekana.

Mungu inusuru nchi yetu.

Sent from my iPhone

On 10 Mac 2013, at 15:23, "Tony PT" <tony_uk45@yahoo.co.uk> wrote:

> Ephata,
>
> Unachouliza ni kunitaka niwe na uwezo wa kiMungu! Mtu hubadilika kulingana na majukumu na changamoto zilizo mbele yake. Mfano mzuri ni pale wewe kama mtoto unapoondokewa na wazazi na majukumu yote kuangukia kwako; kuma mawili yanaweza kukufika, kuwa jasiri na kutatua yanayokufika au kuwa wa hovyo na kukimbia majukumu ya kulea familia.
>
> Huwezi kumjua mtu akiwa chini ya mamlaka nyingine, lakini huyohuyo anaweza kuwa wa maana au akawa wa hovyo sana akibaki peke yake.
>
> Mfano: kwanini JK alipata 82% mwaka 2005? Si kwa sababu tuliona anao uwezo na kila mtu akatiwa matumaini makubwa kutoka kwake! Huyo huyo miaka 5 baadae akaonekana mtu asiye na ujasiri wa maamuzi mengi na mbunge wako wa ubungo akafika hadi kusema rais "legelege". Hivi umeshaongea na waliompa JK kura zao 2005 wakakuambia walifuata vigezo gani?
>
> Kunjua mtu wa kukuvusha kwenye matatizo leo kabla hajaonyesha uwezo wake ni kudanganyika. Hata kama Dk Slaa angeshinda 2010 au Mbowe 2005, hatungesema uwezo wao kabla ya kuwa marais.
>
> Afrika tunapenda kufanya mambo yetu kwa majaribio! Kwa wenzetu wanafuata track-record ya mtu na kufanya uamuzi wa kumpa kura mtu wanayeona ana kumbukumbu nyingi za mafanikio katika maisha na jamii kabla ya kuomba uongozi. Sisi ni kinyume, wanahabari kwa maslahi yao wanaanza kumpamba mtu hata bila kuwa na kumbukumbu yoyote ya mazuri na maovu, inategemea tu mapenzi ya kuaminishwa kwa fedha na uswahiba.
> ------Original Message------
> From: Ephata Nanyaro
> Sender: wanabidii@googlegroups.com
> To: wanabidii@googlegroups.com
> ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
> Subject: Re: [wanabidii] URAIS 2015 - TANZANIA ITAWEZA KUMBEBA LOWASSA ?
> Sent: Mar 10, 2013 15:02
>
> Tony
> Katika mtazamo wako huu huu wa Rais kuwa Taifa,je unadhani au unaamini
> kuna mtu wa mfano huo ndani ya ccm?
>
> On 3/10/13, Tony PT <tony_uk45@yahoo.co.uk> wrote:
>> Ephata,
>>
>> Katika afrika, urais ni muhimu sana kwavile huwezi kutofautisha Urais na
>> taifa. Kwa maana hiyo basi mie sijumuishi kuwa chama fulani k.v ccm wote
>> wameoza; la hasha! Rais kwa nchi za kiafrika ndiye kila kitu na akiwa wa
>> hovyo, nchi na mambo yake yanakuwa ya hovyo.
>>
>> Mfano mnaopenda kuutumia wa Rwanda, huwezi kusema kinachowasaidia kusukuma
>> mambo ni mfumo, sio kweli, ni Kagame! Kagame asipokuwepo leo akaingia
>> mwingine msishangae kuona mambo yakienda mrama! Afrika, rais ndiye nguzo,
>> nuru na tegemeo kuu la utaifa!
>>
>> Nchi za wenzetu mifumo ndiyo inayoongoza taifa na kinachofanyika taifa
>> likiongozwa na vyombo mahususi vya dola ndivyo vinasimamia mifumo na private
>> sector inaongoza uchumi. Serikali huingia na kutoka, hazileti mabadiliko
>> mengi ya kimfumo na serikali na kiongozi wake wakitaka kubadili mfumo
>> huchukua muda mrefu na wakati mwingine waasifanikiwe. Viserikali vya
>> kiafrika kila kukicha mambo mengine, hakuna uimara katika kila kitu.
>> Akiingia rais mzembe nchi inakuwa na institutionalized uzembe na akiingia
>> rais mwizi, kila mtu anaanza kuiba kila alipo! Ndio Afrika yetu ilivyo.
>> Sent from my BlackBerry® smartphone provide
Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Vodacom Tanzania.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment