Sunday 10 March 2013

Re: [wanabidii] URAIS 2015 - TANZANIA ITAWEZA KUMBEBA LOWASSA ?

Tony,

Huwa naheshimu sana mawazo yako. Lakini katika hili, nahisi kuna la zaidi ambalo mlitofautiana na Mh. Lowassa, maana huoni lolote jema alofanya. Umesema watu hubadilika, kwa nini usihisi huyu nae amebadilika au huenda akawa na positive changes zitakazoliletea taifa manufaa hapo mbeleni?

Kweli hali ya sasa inatisha. Mambo mengi yanakwenda tofauti kabisa. Wapo wanaosababisha lakini ukiwasikia wanavyoongea, utadhani hawahusiki kabisa.

Mungu atusaidie nchi hii. Hayo makundi, tusipoyadhibiti mapema, yanaweza kutusababishia matatizo tusiyoyatarajia.

Nitafarijika pale viongozi watakapokuwa na sauti na kutenda haki kama zamani. Siku hizi, maamuzi ni tofauti sana na uhalisia ulivyo. Kilichonitisha zaidi ni kuona umesema hata haki ambago tunaamini hutolewa na mahakama, huenda pia isipatikane kulingana na mtu unavyoonekana.

Mungu inusuru nchi yetu.

Sent from my iPhone

On 10 Mac 2013, at 15:23, "Tony PT" <tony_uk45@yahoo.co.uk> wrote:

> Ephata,
>
> Unachouliza ni kunitaka niwe na uwezo wa kiMungu! Mtu hubadilika kulingana na majukumu na changamoto zilizo mbele yake. Mfano mzuri ni pale wewe kama mtoto unapoondokewa na wazazi na majukumu yote kuangukia kwako; kuma mawili yanaweza kukufika, kuwa jasiri na kutatua yanayokufika au kuwa wa hovyo na kukimbia majukumu ya kulea familia.
>
> Huwezi kumjua mtu akiwa chini ya mamlaka nyingine, lakini huyohuyo anaweza kuwa wa maana au akawa wa hovyo sana akibaki peke yake.
>
> Mfano: kwanini JK alipata 82% mwaka 2005? Si kwa sababu tuliona anao uwezo na kila mtu akatiwa matumaini makubwa kutoka kwake! Huyo huyo miaka 5 baadae akaonekana mtu asiye na ujasiri wa maamuzi mengi na mbunge wako wa ubungo akafika hadi kusema rais "legelege". Hivi umeshaongea na waliompa JK kura zao 2005 wakakuambia walifuata vigezo gani?
>
> Kunjua mtu wa kukuvusha kwenye matatizo leo kabla hajaonyesha uwezo wake ni kudanganyika. Hata kama Dk Slaa angeshinda 2010 au Mbowe 2005, hatungesema uwezo wao kabla ya kuwa marais.
>
> Afrika tunapenda kufanya mambo yetu kwa majaribio! Kwa wenzetu wanafuata track-record ya mtu na kufanya uamuzi wa kumpa kura mtu wanayeona ana kumbukumbu nyingi za mafanikio katika maisha na jamii kabla ya kuomba uongozi. Sisi ni kinyume, wanahabari kwa maslahi yao wanaanza kumpamba mtu hata bila kuwa na kumbukumbu yoyote ya mazuri na maovu, inategemea tu mapenzi ya kuaminishwa kwa fedha na uswahiba.
> ------Original Message------
> From: Ephata Nanyaro
> Sender: wanabidii@googlegroups.com
> To: wanabidii@googlegroups.com
> ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
> Subject: Re: [wanabidii] URAIS 2015 - TANZANIA ITAWEZA KUMBEBA LOWASSA ?
> Sent: Mar 10, 2013 15:02
>
> Tony
> Katika mtazamo wako huu huu wa Rais kuwa Taifa,je unadhani au unaamini
> kuna mtu wa mfano huo ndani ya ccm?
>
> On 3/10/13, Tony PT <tony_uk45@yahoo.co.uk> wrote:
>> Ephata,
>>
>> Katika afrika, urais ni muhimu sana kwavile huwezi kutofautisha Urais na
>> taifa. Kwa maana hiyo basi mie sijumuishi kuwa chama fulani k.v ccm wote
>> wameoza; la hasha! Rais kwa nchi za kiafrika ndiye kila kitu na akiwa wa
>> hovyo, nchi na mambo yake yanakuwa ya hovyo.
>>
>> Mfano mnaopenda kuutumia wa Rwanda, huwezi kusema kinachowasaidia kusukuma
>> mambo ni mfumo, sio kweli, ni Kagame! Kagame asipokuwepo leo akaingia
>> mwingine msishangae kuona mambo yakienda mrama! Afrika, rais ndiye nguzo,
>> nuru na tegemeo kuu la utaifa!
>>
>> Nchi za wenzetu mifumo ndiyo inayoongoza taifa na kinachofanyika taifa
>> likiongozwa na vyombo mahususi vya dola ndivyo vinasimamia mifumo na private
>> sector inaongoza uchumi. Serikali huingia na kutoka, hazileti mabadiliko
>> mengi ya kimfumo na serikali na kiongozi wake wakitaka kubadili mfumo
>> huchukua muda mrefu na wakati mwingine waasifanikiwe. Viserikali vya
>> kiafrika kila kukicha mambo mengine, hakuna uimara katika kila kitu.
>> Akiingia rais mzembe nchi inakuwa na institutionalized uzembe na akiingia
>> rais mwizi, kila mtu anaanza kuiba kila alipo! Ndio Afrika yetu ilivyo.
>> Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Vodacom Tanzania.
>>
>> -----Original Message-----
>> From: Ephata Nanyaro <nanyaro04@gmail.com>
>> Sender: wanabidii@googlegroups.com
>> Date: Sun, 10 Mar 2013 14:32:45
>> To: <wanabidii@googlegroups.com>
>> Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
>> Subject: Re: [wanabidii] URAIS 2015 - TANZANIA ITAWEZA KUMBEBA LOWASSA ?
>>
>> Ndani ya ccm hakuna msafi samaki wote wameoza.Tatizo la ccm ni
>> mfumo,mfumo ambao wote walioko ndani yake wameharibika,hakuna
>> atakayesimama kwa tiketi ya ccm akajinadi kuwa ni msafi,ni kiwango cha
>> uchafu tu ndio kinatofautiana
>>
>> On 3/10/13, tikooza@yahoo.com <tikooza@yahoo.com> wrote:
>>> Tony
>>>
>>> Umesema vizuri ndugu yangu. Kati ya watu ambao hawana sifa ya kupambana
>>> na
>>> matatizo tulinayo kama taifa ni Yeye.
>>> Ila ni mmoja ya watu ambao maamuzi yake lazima yaambatane na gharama. Ni
>>> maamuzi yake mengi ni ya pupa.
>>>
>>>
>>> Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.
>>>
>>> -----Original Message-----
>>> From: "Tony PT" <tony_uk45@yahoo.co.uk>
>>> Sender: wanabidii@googlegroups.com
>>> Date: Sun, 10 Mar 2013 07:23:39
>>> To: <wanabidii@googlegroups.com>
>>> Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
>>> Subject: Re: [wanabidii] URAIS 2015 - TANZANIA ITAWEZA KUMBEBA LOWASSA ?
>>>
>>> Elisa,
>>>
>>> Aliyewasaidia waTz kupata maji ya Victoria si Lowasa, ni rais Mkapa
>>> kwenye
>>> ahadi yake ya 2000 kwa mkoa wa shinyanga. Wakati huo Lowasa alikuwa kama
>>> sio
>>> bench ni ofisi tofauti kabisa. Baada ya uchaguzi wa 2000 ndipo Lowasa na
>>> Dk
>>> Limbu wakaingia wizara hiyo.
>>>
>>> Utekelezaji wa mradi wa maji ulianza 2001 wakati wa Lowassa na Diallo
>>> kama
>>> NW.
>>>
>>> Kama nilivyosema awali, wengi mnaompigia jalamba huyu Mhe ni adui zake
>>> (kwa
>>> kujua au kutokujua) au ni wapinzani wa ccm (kwa kujua au kutojua. Kama
>>> ccm
>>> wakamteua Lowasa kugombea urais ataanguka asubuhi tu! Madhambi
>>> aliyowafanyia
>>> watanzania ni mengi afadhali wakuweke wewe Elisa hauna historia ya
>>> kuwakosea
>>> waTz.
>>>
>>> Sifa mnazompa lowasa hanazo, alibahatika kuwa kufanya kazi na wasaidizi
>>> makini na pia Rais makini. Wengi wetu tunasahau au hatujui Lowasa na
>>> matatizo yake ya nyuma: alipokuwa tume ya Loliondo, na alivyokula hela za
>>> waarabu na kuwaacha hadi leo wapo Loliondo badala ya ilivyotarajiwa na
>>> waTz
>>> (soma tume teule ya Bunge kuhusu Loliondo) ipo hansard za bunge. Pia
>>> alipokuwa AICC kama CEO alivyopoteza fedha za ujenzi wa staff na baada ya
>>> hapo alivyojinyakulia ardhi ya AICC na baadae kuuziwa Themi Hill Suites,
>>> na
>>> wengine walio jirani ardhi iliyokuwa ya AICC!
>>>
>>> Pia msaada wa ujenzi wa kiwanda cha vyandarua Sunflag, Sumitomo
>>> waliwekeza
>>> na serikali ya
> Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Vodacom Tanzania.
>
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment