Tuesday 12 March 2013

Re: [wanabidii] URAIA WA NCHI 2 – TUZUNGUMZE KWA UWAZI


(i) Je, kama u raia wa nchi 2 utakuwa na mamlaka miliki nya ardhi kote na pia kupiga kura kote? Nina wasiwasi Wabongo wanaweza kwenda huko kuoa mzungu au mtu wa huko, kurudi huku na uwezo wake kununua ardhi nao wakwe zake kuja kumiliki kiuwezo kuwanunua watu wageni wakajaa kwa njia hiyo maana kazaa na ni ndugu za wanawe. hii ya Uraia pande mbili imezigharimu nchi nyingine tujifunze kwanza. ukiwa kule ukiukana uraia wa TZ ukija huku unaweza kufukuzwa maana si wa huku kama ilivyowafika Wakenya  fulani baada Visa yao kuisha walikaa Airport na kutakiwa kuondoka nchini wao si wakenya.

(ii) Bado wapo wazungu wanamiliki mashamba/ardhi kubwa TZ. wao walikuwa wakoloni huku, kuishi miaka mingi na baadae kwenda kwao kufa. Wajukuu wanarudi sasa ni uwekezaji. Vile vile waarabu, wahindi wenye maekari ya ardhi kubwa bongo wapo kwani mwarabu alitawala wakati wa utumwa. Wapo Greeks Tanzanians etc na ya maelfu ya maekari. Uchao Waarabu ni Oman, wahindi Bombay, Europe, Canada.
Baadhi ya wakazi waswahili (Masuria au wafanyakazi wao wa zamani) na wanavijiji wengine wameishi katika ardhi za watu hawa na wanazeekea humo wao na wajukuu wao lakini ardhi si yao. Hawatakiwi kujenga vitu vya kudumu. Wanavuna nazi, korosho na mazao mengine wanakula.

Wapo wabongo ambao walipokombolewa utumwa waliweka katika ardhi ya madheheby ya dini fulani hata makanisa ardhi ambayo imepimwa na ina hati miliki ya madhehebu hayo. Hadi leo wapo humo na kuna baadhi wanatakiwa kuhama ili miradi ya taasisi hiyo ipanuliwe ni wakati wa uwekezaji sasa. Hamjatatua hili.

Kwa maoni yangu, tusidandie suala la Uraia wa nchi 2 kabla hatujatatua masuala ya Miliki Ardhi Nchini.

Na sasa tunafungua East Africa Community na mataifa jirani mengine tunaongeza. Tunao wachina na wazungu wanapamba moto kuoa pamoja na dadapoa ili tu wapate ardhi na Uraia wapate kuwekeza bila kufuata mashati ya uwekezaji ya TIC bali ya Uraia tu wa kuandikisha.

Haki zao za uraia wa Nchi 2 kama hao watanzania utakuwaje? Raia wa China na huku TZ kama sisi hapa TZ kuwa Raia na China kuwa Raia wa hapa. Kwa somo kunaliwa (China) na kwa mwali pia (Tanzania)-wana uwezo, wameoa kwetu, anapata ardhi anainunua, anampa talaka, anabaki amemiliki ardhi, anaoa mtu wa kwao. Tuangalie na haya. Utakavyo wewe haki sawa kwao na kwako pia uwape. Huko Ulaya nchi nyingine waliwapa masaa 24 waafrika au mgeni kuondoka baada ya kumuacha mke maana sasa hawawapi uraia wa kudumu baada ya kumuoa mtu wa huko. Wameona kijana mdogo anaoa bibi mzee au msichana anaolewa na libabu baada ya kupata Uraia-anamuacha anachukua dogo mwenzake nan kuishi huko kutumua kodi za watu. Ukimuacha akikushitaki-rudi kwenu. jee, nasi tutawafukuza na tuna vitoto vyao?

(iii) Ujangili wa uvamizi misitu unaoendelea na ujambazi mwingine unaofanywa na wageni kushirikiana na wenyeji ni kwa muingiliano namna hii mtu anaingia anaoa, anapewa ardhi na kufanya ujambazi. Wakimbizi kupewa uraia analeta wenzake wanaongezeka maana ni nduguze. Akimaliza kuharibu-anarudi kwao si raia wa huko na kijiji chao anakijua? Kama mbongo wa sasa Raia wa hapa anasaliti nchi anaingiza raia wa kigeni na majambazi. Jee, akiwa raia wa South Afrina, England, Somalia etc na Raia wa TZ hatotusaliti na hiyo mihela yake na kuleta Mafia wa kisiasa, mitandao ya wizi bank ya kuleta ushabiki wa uamsho KIDINI etc?

(iv) Bado hatujatatua masuala hata ya migratory people ndani ya nchi tunapigana kila leo-ltutaweza usalama wa Uraia nchi 2 sio kwa wabongo tu hata hao wageni kama inavyotakiwa kwa sasa.

Mtu analima kwake Umasaini, Usukumani kila eneo la ardhi yake anazalisha mazao na mifugo michache huko. Wasukuma-mpunga ktk majaruba, mihogo, mtama mwekundu etc. Wanauza mchele TZ and outside TZ. Anachimba madini, anaoza katoto anaongeza mifugo. Anaitawanya apendavyo na kuonea wengine huko kuwapiga na kulishia mashamba yao. akifika huko anakata misitu anachoma mkaa, anauza mbao, anaongeza mifugo kwao na hapo alipo. Akimaliza-anahamia kwingine. alianzia Changanyikeni, akaenda Goba, Makongo, Salasala, Kigamboni, Kisarawe, Rufiji sasa anaingia Lindi, Mtwara. Kata miti, uza mbao, mkaaa peleka nyumbani, nunua mifugo uonekane tajiri, zagaza mifugo peleka Ruaha, kilombero, Kilosa. Sababu-Mimi Mtanzania, nina haki kwenda kokote kule na kuishi. Uharibifu wa mazingira na tabia hizi tunafumbia macho ili tusikose KURA na zitatumaliza.

(v) Kama tunashindwa kuweka uangalizi wa hawa wa nchini humu chaotic migratory system watu kupigana na kuuana, jee huo uangalizi wa makini kwa hao wanaorudi wenye hela na koo zao zilizotoka huko tutaweza kama unavyoona wewe Yona?

Hawa wa hapa ukifanya tracer studies unakuta alikotoka kupo, ana ardhi kubwa huko kwaoi analima na wala halishii mifugo mazao yake!! Ana mifugo ya ngo'mbe elfu 4-10; mbuzi 1000 maana ndio anauza mara kwa mara, kondoo 500, punda 6, wake 10, watoto 80, wajukuu 300 na hawasomi kama alisomesha ni vijana wa kiume 6 tu. Wengine anafuga mifugo hiyo si yake bali akifuga kama kibarua wa kuhamahama analipwa mifugo kadhaa kila mwaka na ana ruhusa ya kunywa na kuuza maziwa tu kama daily pay. Kisingizio si ardhi pekee, kufuga ki-600AD badala ya kisasa penye ongezeko hata la watu ndani ya familia yake sio la nchi pekee.

Na kama wakoloni wasingeanzisha protected forest and wildlife areas kwa kulinda ile misitu ya babu zetu wakiabudia mizimu (kulinda natural resources kwa imani ingine kutishia watu wao) sijui Tanzania ingekuwaje-Jangwa kuliko Somalia na Mali maana tunaichakachua kwa visingizio vya kuonewa ardhi kubwa kuhifadhiwa wakati tuliyonayo viziwi tunaimaliza kuwa jangwa na misitu hifadhi tunaichakachua badala ya sustainable use. Na tuandamane ila hizi ni issue zinatuhusu maana watendaji ni sisi. Na tuombe uraia wa nchi mbili-majambazi tutaficha sisi na ardhi tutauza kinyemela kisha kulalamika.


--- On Tue, 12/3/13, Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:

From: Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>
Subject: [wanabidii] URAIA WA NCHI 2 – TUZUNGUMZE KWA UWAZI
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Tuesday, 12 March, 2013, 20:03

Ndugu zangu

Kuna hili suala la Uraia wa Nchi mbili yaani mtu anakuwa Mtanzania
anapoenda Ufaransa kuishi na kupata uraia wa huko basi ana uwezo pia
wa kuendelea kuwa na ule wa Tanzania na kuendelea kuwa na haki
nyingine zote kama Mtanzania .

Suala hili limekuwa linaumiza vichwa vya wengi haswa kwenye suala la
ulinzi na usalama wengine wanaogopa kwamba maadui zako wanaweza
kutumia fursa hiyo kukumaliza kwa kupandikiza watu wao wenye uraia wa
nchi mbili .

Kwa upande mwingine kuna faida zake kwa maana kama mtu ameondoka
akachukuwa uraia mwingine ana uwezo wa kurudi kuwekeza na kufanya
maendeleo bila kikwazo chochote kama raia mwingine wa nchi husika .

Katika hili mimi naona uraia wa nchi mbili uruhusiwe watanzania wawe
na uwezo na uhuru wa kubaki na uraia wao pindi wanapokuwa na uraia wa
nchi nyingine ila wawekwe kwenye uangalizi maalum kwa siku , miaka
kadhaa kabla ya kuruhusiwa kabisa .

Sijui wenzangu mnaonaje .

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment