Tuesday 19 March 2013

Re: [wanabidii] RE:Wakikuyu wanatwaa ardhi Arusha?

Wana wa Bidii,

Huwa nafurahia sana mada kama hii hasa juu ya hofu yetu kwa Wakenya na unyakuzi wa ardhi, mwaka 2010 nilikuwa Arusha kwenye kongamano la masuala ya ardhi tukapata fursa kutembelea kijiji kimoja wapo welekeo wa Namanga kujifunza namna ambavyo wanashughulika na masuala ya haki za ardhi hasa mambo ya mpango bora wa matumizi ya ardhi, tukiwa na Kamishina wa Ardhi wa Kanda ya Mashariki wakati huo. Mwenyekiti na timu yake walitupa maelezo mengi mazuri na tukafurahi kuona welewa wao ulivyokuwa mkubwa. Nikaamua kuuliza swali la kizushi, hivi wageni kwa mfano majirani zetu Wakenya wakija hapa kijijini vipi wanaweza uziwa au hata kupewa kipande kama kipo? Jibu tena kwa furaha tele lilikuwa ndio na tukaambiwa tena hawa wanakuja na Rambo zimejaa fedha huwa tunawaauzia!!!!! na isitoshe ndio njia nzuri ya kudumisha Jumuiya, unaona hawa wenzetu walivyokuwa mbali kijumuiya, bila shaka wakifuatilia mjadala huu watatushangaa sana.

Ikatulazimu tuanze tena kutoa darasa upya, mbona hyo huko ni kawaida kabisa! tena yasemekana Mteule Uhuru ana vipande vya kutosha huko, na bila shaka kwa tetesi aina hii yatupasa na yawapasa wahusika wafanye kazi yao na sie watafiti ni eneo la kutupia macho. Kitu kingine wengi tunafikiri sheria yetu ni madhubuti namna hyo, hivi hawa Wakenya mnaowataja si ndio naambiwa kwa uwekezaji ndio nambari 1 hapa kwetu? sasa wanawekeza hewani? wengine wapo katika mashamba nk, na wengine ndio wamepata vipande vya ardhi kupitia kwa dada zetu, niliona hii sehemu moja baada ya kukuta wahudumu wanaongea lafudhi ya Kenya kuwahoji nikaambiwa kweli watokea huko na kazi sampuli hyo ilipaswa kufanywa na wabongo! 

Sio Arusha tu, maeneo yote unayofahamu prime areas watafika na sidhani kama tunaweza wazuia, moja ni kwa kuingia ubia na wabongo wachache wenye uchu kama jamaa mmoja niliyemkuta vijiji vya Rufiji kuuliza nikaambiwa ati kuna kampuni anasaidia kufanya mpango ipate ardhi nilipoambiwa jina moja kwa moja ilikuwa kampuni yenye mahusiano na wajukuu wa Lord Delamere bila shaka mnakumbuka yule aliyeshtakiwa huko Kenya kwa kosa la kumtwanga Mwananchi aliyekuwa ati ame tresspass shambani kwake. Mie nadhani mwarobaini wa haya yote ni  KATIBA MPYA, ilivyo sasa sheria inayosimamia rasilimali ardhi ni sheria ya kawaida tu na pili ina mianya ya kutosha kuwezesha mtu yeyote wa nje achilia mbali Kenya kujipatia ardhi kwa njia halali na hata haramu na wala asifikishwe kokote na hata akipelekwa mahakamani bado aonekane ana haki, pana kesi iliamriwa majuzi haya yalitokea hapa Dar, Mama ni Mtanzania mwenye asili ya Ugriki kafariki mwanae mrithi si Mtanzania?!

Bila shaka wadau wa masuala ya ardhi wamefikisha ujumbe na sie wengine tusome hayo makabrasha rasimu itakapokuja tuangalie hasa kwenye rasilimali ardhi ni kwa kiasi gani tumejihakikishia ulinzi, tutaendelea kutafuta mchawi sijui Kenya, Rwanda, Burundi kumbe wenyewe ndio wachawi.

Wasalaam.
Mdau wa ardhi inayoendelea kuondoka.


From: alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, March 19, 2013 5:55 PM
Subject: [wanabidii] RE:Wakikuyu wanatwaa ardhi Arusha?


Chambi na Wasimbeye,
Chambi aksante kuliona hilo. Mimi binafsi nitofautiane na wa-Simbeye juu ya mawazo yake. Japo sheria hairuhusu mgeni kununua ardhi hatupaswi kuwaacha wachukue ardhi alafu baadae ndipo tuende kuwapinga mahakami. Tukiacha ifikie hapo tutapata shida sana mbeleni, hasa ukizingatia udhaifu wa vyombo vyetu vya kutoa haki kama polisi na mahakama kutokana na RUSHWA. Kumbukeni kuo hao Wakenya Kwa sasa wanatumia pia KETE AU UJANJA wa kuoa dada zetu ili wapate haki za-Watanzania hasa Ardhi. Kimsingi hawana haja ya kuwaoa ila wanataka kuhararisha kiu yao ya ardhi. Ikiwezekana tunapaswa kukaza sheria kua wanapowaoan dada zetu ardhi iandikishwe kwa jina la mwanamke.

Chamsingi ndugu zangu tunapaswa kuwafundisha watu wetu juu ya umhimu wa ardhi hasa katika kipindi hiki ambapo ardhi inatafutwa na mataifa mengi. Wakenya wameshindwa kutatua masuala ya ardhi internally-maana wameacha watu wachache kujimilikishia maeneo makubwa; ndio maana matukio ya mapigano juu ya ardhi Kenya ni mengi sana . Kwa mtizamo wangu nchi nyingi tulizojiunga nazo kwenye hii EAC na hasa Kenya lengo lao kubwa nikutumia EAC kutatua matatizo yao ya ndani hasa suala la ardhi. Yatupasa tuwe macho sana. Watanzania tunatakiwa kufumbua macho na kuona nje ya BOX kinachoendelea. Mara nyingi viongozi wanasaign mikataba ambayo itatuacha solemba mbeleni kama taifa.
Alexander


From: Finnigan wa Simbeye <f_simbeye@yahoo.com>
To: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Sent: Tuesday, March 19, 2013 2:10 PM
Subject: Re: [Mabadiliko] Wakikuyu wanatwaa ardhi Arusha?

Chambi,

Wameliwa hao, ardhi siyo swala la Jumuiya na sheria yetu inakataza mgeni kumiliki ardhi, watanunua lakini mwishowe watu watawarudi baada ya kwenda mahakami. Wanaweza kupata ardhi kama wawekezaji kupitia TIC. Waache waje nami nawashauri Watanzania mlioko na ardhi Arusha wauzieni then mwende mahakamni hawana chao!!

wa Simbeye



--- On Tue, 3/19/13, Chambi Chachage <chambi78@yahoo.com> wrote:

From: Chambi Chachage <chambi78@yahoo.com>
Subject: [Mabadiliko] Wakikuyu wanatwaa ardhi Arusha?
To: "Wanazuoni" <Wanazuoni@yahoogroups.com>
Date: Tuesday, March 19, 2013, 2:02 PM

Mfuatiliaji wa kwa karibu wa masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anasema kuwa katika miaka ya 70 baada ya Arusha kufanywa makao makuu ya jumuiya hiyo, Wakikuyu wengi walinunua/walitwaa ardhi hapo. Hivyo, Arusha ikaanza kuwa kama sehemu ya Kenya na fedha ya Kenya ikawa ndio inadaiwa/inatumika katika mahoteli, maduka n.k. Kwa mujibu wa maelezo yake, hali hii ilikoma baada ya Tanzania kufunga mpaka wake na Kenya katika mtafaruku wa kuivunja jumuiya hiyo.

Mdau huyo anasisitiza kuwa tukio hilo lilisababisha Wakikuyu warudi/wakimbilie kwao Kenya. Sasa anaona wanarudi kwa kasi sana na anahisi Watanzania hawana wasiwasi kabisa. Anashauri watafiti wa masuala ya ardhi watathmini kwa kina ni kiasi gani cha ardhi huko Arusha kimeshatwaliwa na Wakikiyu. Hofu yake ni kuwa ushindi wa Uhuru Kenyatta unaweza kusababisha hali hii izidi hasa katika muktadha wa kuiimarisha Arusha kama makao makuu ya Jumuiya mpya ya Afrika Mashariki. 

"Kwa kuwa Arusha sasa imekuwa kitongoji cha Nairobi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ni vyema kutathmini ardhi inayotwaliwa na Wakikuyu" - Mdau Mfuatiliaji
--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
 
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 
--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
 
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 




--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 


0 comments:

Post a Comment