Wednesday 20 March 2013

Re: [wanabidii] RE:Wakikuyu wanatwaa ardhi Arusha?

Sisi wa ajabu hata mipira tunashindwa, mbio kukimbia tabu ndani ya nchi yetu tunashindwa hiyo kilimanjaro marathon.  Mazoezi ya mpira yanaanza siku chache kabla ya shindano. Hata kuamka ukimbie mbio ndefu daili ili kiwanjani ukimbize mpira kwa kazi-mpaka uwekwe kambini, ulishwe, serikali ituwezeshe!! Sio kwamba uamke daily mbio kila siku-NO, unabugia pombe na chips daily mpaka msimu wa mashindano. Kisha-serikali ituwezeshe! Yaani ipite kila nyumba ikuamshe ukimbie ili ushinde marathon nawe unajijua ni mkimbiaji au unataka ukimbie? Na budi ujifunze kukimbia na viatu ili uvizoee maana kijijini umezoea pekupeku. Ukishinda-si unapanda chati na pia kupata hela? Uza kuku mmoja upate kiatu cha mtumba.

Pamoja na kuwa ninaipenda nchi yangu na utanzania-lakini ninaona, sisi waTZ tuna matatizo kichwani.
Angalia afanyavyo Waziri wa Uchukuzi au Mangufuli. Adui watakuwa wale wanaosafirisha kimagendo na maofisa faidika sio mwananchi wa kawaida. Kwa wananchi-wao kwa wao, ndugu mmoja kuuza ardhi ya ukoo kifisadi. babu au mmoja ni mwenyekiti anauza ardhi kwa wageni na ndugu hamna usemi mnamuogopa. Tumefikia kuogopana ndani na nje ya kaya na community.

Tunaweza kuendelea bila wageni kama matajiri wa nchi hii aidha waliupata utajiri kwa haki, na bila haki wataungana na kuunda kampuni kubwa na uchumi na kufufua viwanda vilivyofungwa ambapo wengine wakipewa nanatengeneza chupa badala ya nguo na recycling magazeti kupata used papers badala kutoa magunia ya mkonge. Nao matajiri wamekaa kichukichuki tu labda kuonekana ktk kuchangia mashindano ya mpira na miss Tanzania. Inafurahisha unapoona ktk TV wafanyabiashara wamejenga kituo cha polisi, zahanati, nyumba za walimu kama tulivyoona majuzi hapa. Itafurahisha pia kuona watanzania na wageni wao hawaharibu misitu na ardhi ktk kuchimba madini kiriri, mifugo na kutaka miti. Tajiri wanaunda kampuni na kuajiri vijana wapewe mafunzo ya kiufundi ndani na abroad (scholarship ya Mengi, Abood, Hood, Bakresa, Sabodo Fund). Au wanaunda Foundation kama hiyo ya Clinton Foundation, Millenium Challenge Account (George Bush) Akga Khan Foundation zenye miradi mikubwa ya maendeleo duniani. Yao iwe ya TZ tu. Tutafika. Tujitahidi. 

--- On Tue, 19/3/13, alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com> wrote:

From: alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com>
Subject: Re: [wanabidii] RE:Wakikuyu wanatwaa ardhi Arusha?
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Tuesday, 19 March, 2013, 17:57

Hildegard,
Hakuna kipindi ambapo Tanzania tunatakiwa kua na Migration Department inayowajibika ipasavyo kama kipindi hiki ambapo sera za utandawazi zinapaliliwa sana, pamoja na hiki kitu kinaitwa 'EAC'.

Pamoja na ukweli kua hatuwezi kuiendeleza nchi bila kuwashirikisha wageni tukumbuke pia kua swala la UZAWA NIMUHIMU sana. Nchi zote zinazingatia hilo, ukiwa Ulaya huwezi pata kazi ambazo wazawa wanuwezo nazo, ndio maana wa-africa wengi Ulaya wanaishia kufanya kazi za hadhi ndogo (sio prefessional job).

Tanzania na watu wake kwa sehemu kubwa tumeathiriwa na sera za ujamaa na kujitegemea ambazo zilitufundisha undugu kitu ambacho ni chamsingi sana. Ila tukumbuke kua watu wengi tunao shirikiana nao hawana huo undugu tunao wafanyia. Na  ndio maana ukiangalia sana hata nchi zao wanakotokea hawapendani wao kwa wao-ukabila na kuuana kwa misingi ya ukabila ndio yamejaa. Sasa kama ndio hivyo je! watatupenda sisi wa-Tatnazania? Tunapaswa kuliangali hili jambo kwa umakini mkubwa. Nionavyo watatuletea matatizo zaidi huko tuendako.
Alexander

From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Tuesday, March 19, 2013 5:35 PM
Subject: Re: [wanabidii] RE:Wakikuyu wanatwaa ardhi Arusha?

Alexander,
Jiulize-mfugaji kutoka Burundi ameingia na mifugo vipi tunayoiona katika TV akakaa na kubughudhi wenyeji wa kijiji hicho kwa maelfu wao wachache tu.

Kutoka nayo kwao, yupo kijiji fulani, kitongoji fulani kijiji hicho au msituni analima, anachunga, anakata miti, anachoma mkaa, anawatuma vibarua vya kulika na kukata miti, kubeba magunia-Kabang, kaingiaje hapo?

Ukifuatilia-mtu anakuambia hii ni customary land yangu nina uhuru nayo kumuuzia nimtakae nina shida ya hela na hii si yako. Mwingine anaoa msichana kinamna, anapata ardhi, anahamia, anakaa naye, anamuacha analeta watu wa kwao. Ulimpa mwenyewe ardhi kama mkwe. Akili kukichwa na vitambulisho ukamtafutia kwa rushwa.

Na ndio unaweza ukafika kijiji fulani ukauta kuna Raia wa kigeni kaoa kabinti wana maekari ya ardhi. Anatembelewa na watu kibao eti wageni wake kutoka kwao ulaya. Kumbe wale ni watalii, hana udugu nao hata ni mtandao. Wanamlipa yeye hela, wanaingia wanatumia magari yake kwenda kutembea mbugani wanakodi kwake. Utalii wa kisiri na huyo kadadaa anaiuza nchi.

Mpaka majasusi yameshakamatwa nchini hapa likitafutwa miaka na interpool. Moja likisakwa USA black lakini Jamaican Origin. Hili lilihamia eneo la vijiji vya Mto Ruvu Wilaya ya Same. Likawa linalima hapo, linatoa ajira watu kujipendekeza kwake. Usiniulize mengi, si uongo. DC anakwenda kutembelea vijiji na kilimo cha umwagiliaji anaona kajumba na rasta huyo akauliza ni nani yule anafanya nini-ahaa huyu mtu wetu mwekezaji anatusaidia sana hapa!! Alikwenda akamuohi machale yakamcheza. Akalifuatilia, kisha kuwauliza US Embassy kama wanamfahamu huyu mtu muwekezaji Jamaican aliyepo hapo ambae ni Raia wao-Ambassador mwenyewe alisema naja huko huko huyo wanted ni hatari. Alifika Same na jamaa masaa 24 kabebwa kapeleka alikotakiwa.Non-persona grata  hii iliwapata wazungu 2 mmoja Kijiji cha Kisiwani na mmoja Maore/Gonja. Nilimsifu DC Peter Kangwa-yupo Moshi kwa sasa. Nao hao masaa 24 hadi leo hawajarudi na mmoja alijenga nyumba hapo Kisiwani lipo. Hao wakifanyakazi za NGO lakini walikuwa maalun, fidhuli wanyanyasaji, dharau hata kwa viongozi, watafiti, kuchochea mambo na kugombanisha wanandoa kwa mafunzo ya gender yasiyo maadili. Wakibebwa na wanakijiji waliokuwa wanajipendekeza kujipatia kuomba visent. Walikukutana na mtu apendae taifa lake Peter Kangwa -Hadi leo hawajarudi mjumba wa kisiwani upo.

Mtwara kuna wasomali na biashara zao. Majumba ya NHC Dar unaona yamefanyiwa extension kuwekwa restaurant, maduka ya spea etc unashangaa mtu amepanga lakini amebadili design. Tumelala. Utayaona Jangwani Fire area, Upanga etc.

Kuna hadithi za wahamiaji kujazana humo kwa jamaa zao waliowaleta toka bombay, Somalia etc wanapika mavyakula ya hoteli hawaonekani nje bali nje ni vijana wetu kugawa chakula. Baada ya muda-wanamudu kuhamia na kununua majumba/ardhi kujiweka kibiashara bila kupitia TIC. Hawa wawekezaji uchwara bila benefits kwa jamii ni wengi.

Utayaona haya- wameuza Ardhi Mafia kwa wageni kinyemela wanalia wenyewe sasa uonevu-hawasikii. Milingoti imejaa Kiwa, Lindi, Bagamoyo watu wamenunua ardhi sana baadhi ni kutoka nchi jirani kupitia migongo ya vijana wetu. Kijana mbongo ananunua kwa niaba.  Utatofautishaje Mkurya na Mkikuyu, Mhaya na Mganda, Mnyarwanda na Mha? Anasema nduguye!!. Anamunulia, anaishi bila vibali yeye yake ni 10% tu anapata. Sasa Wachina ndio wanaoa vibaya kama vijana wetu wanachooa majimama mazee ili apate kujengewa aukate. haya ndio maendeleo. wageni watapata ardhi kwa mbinu nyingi kama sisi tunavyotorokea kwanda na kukaa nchi zao kwa mbinu nyingi.

TUCHUKUE HATUA sote tuwajibike tusidanganyike kwa tamaa ya mafao ya muda mfupi.

--- On Tue, 19/3/13, alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com> wrote:

From: alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com>
Subject: [wanabidii] RE:Wakikuyu wanatwaa ardhi Arusha?
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Tuesday, 19 March, 2013, 14:55

Chambi na Wasimbeye,
Chambi aksante kuliona hilo. Mimi binafsi nitofautiane na wa-Simbeye juu ya mawazo yake. Japo sheria hairuhusu mgeni kununua ardhi hatupaswi kuwaacha wachukue ardhi alafu baadae ndipo tuende kuwapinga mahakami. Tukiacha ifikie hapo tutapata shida sana mbeleni, hasa ukizingatia udhaifu wa vyombo vyetu vya kutoa haki kama polisi na mahakama kutokana na RUSHWA. Kumbukeni kuo hao Wakenya Kwa sasa wanatumia pia KETE AU UJANJA wa kuoa dada zetu ili wapate haki za-Watanzania hasa Ardhi. Kimsingi hawana haja ya kuwaoa ila wanataka kuhararisha kiu yao ya ardhi. Ikiwezekana tunapaswa kukaza sheria kua wanapowaoan dada zetu ardhi iandikishwe kwa jina la mwanamke.

Chamsingi ndugu zangu tunapaswa kuwafundisha watu wetu juu ya umhimu wa ardhi hasa katika kipindi hiki ambapo ardhi inatafutwa na mataifa mengi. Wakenya wameshindwa kutatua masuala ya ardhi internally-maana wameacha watu wachache kujimilikishia maeneo makubwa; ndio maana matukio ya mapigano juu ya ardhi Kenya ni mengi sana . Kwa mtizamo wangu nchi nyingi tulizojiunga nazo kwenye hii EAC na hasa Kenya lengo lao kubwa nikutumia EAC kutatua matatizo yao ya ndani hasa suala la ardhi. Yatupasa tuwe macho sana. Watanzania tunatakiwa kufumbua macho na kuona nje ya BOX kinachoendelea. Mara nyingi viongozi wanasaign mikataba ambayo itatuacha solemba mbeleni kama taifa.
Alexander

From: Finnigan wa Simbeye <f_simbeye@yahoo.com>
To: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Sent: Tuesday, March 19, 2013 2:10 PM
Subject: Re: [Mabadiliko] Wakikuyu wanatwaa ardhi Arusha?

Chambi,

Wameliwa hao, ardhi siyo swala la Jumuiya na sheria yetu inakataza mgeni kumiliki ardhi, watanunua lakini mwishowe watu watawarudi baada ya kwenda mahakami. Wanaweza kupata ardhi kama wawekezaji kupitia TIC. Waache waje nami nawashauri Watanzania mlioko na ardhi Arusha wauzieni then mwende mahakamni hawana chao!!

wa Simbeye

--- On Tue, 3/19/13, Chambi Chachage <chambi78@yahoo.com> wrote:

From: Chambi Chachage <chambi78@yahoo.com>
Subject: [Mabadiliko] Wakikuyu wanatwaa ardhi Arusha?
To: "Wanazuoni" <Wanazuoni@yahoogroups.com>
Date: Tuesday, March 19, 2013, 2:02 PM

Mfuatiliaji wa kwa karibu wa masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anasema kuwa katika miaka ya 70 baada ya Arusha kufanywa makao makuu ya jumuiya hiyo, Wakikuyu wengi walinunua/walitwaa ardhi hapo. Hivyo, Arusha ikaanza kuwa kama sehemu ya Kenya na fedha ya Kenya ikawa ndio inadaiwa/inatumika katika mahoteli, maduka n.k. Kwa mujibu wa maelezo yake, hali hii ilikoma baada ya Tanzania kufunga mpaka wake na Kenya katika mtafaruku wa kuivunja jumuiya hiyo.

Mdau huyo anasisitiza kuwa tukio hilo lilisababisha Wakikuyu warudi/wakimbilie kwao Kenya. Sasa anaona wanarudi kwa kasi sana na anahisi Watanzania hawana wasiwasi kabisa. Anashauri watafiti wa masuala ya ardhi watathmini kwa kina ni kiasi gani cha ardhi huko Arusha kimeshatwaliwa na Wakikiyu. Hofu yake ni kuwa ushindi wa Uhuru Kenyatta unaweza kusababisha hali hii izidi hasa katika muktadha wa kuiimarisha Arusha kama makao makuu ya Jumuiya mpya ya Afrika Mashariki. 

"Kwa kuwa Arusha sasa imekuwa kitongoji cha Nairobi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ni vyema kutathmini ardhi inayotwaliwa na Wakikuyu" - Mdau Mfuatiliaji
--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
 
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

0 comments:

Post a Comment