Monday 11 March 2013

Re: [wanabidii] Re: URAIS 2015 - TANZANIA ITAWEZA KUMBEBA LOWASSA ?

Nimemwelewa Ephata baraabara.
CCM wameshajitengenezea kizazi cha sumu, ukiwa mwanachama wa chama
hicho that mean unaambatana na kukubaliana na hayo yote yanayotendeka
ndani yake, kama uko against that mean haupo nao!! labda kadi yao tu!
Ni nini kitakachomfanya mtu msafi apate nafasi na kipaumbele cha
kugombania nafasi ya urais ndani ya watu wanaoamini tofauti na yeye?

Ndege wanaofanana huruka pamoja!! Hata vijana wa sasa CCM wana maono
yanayofanana na CCM yenyewe, kuna aliyesoma UG na akawa anaishia
kuhonga afanyiwe assignment na mengineyo, yeye maisha yake ni
kuhangaika na masherehe ya harusi na CCM yake. Angalia mawazo ya
vijana wengi walio ndani ya CCM, wao huamini wako upande sahihi na
hakuna anayetaka kukosolewa. Hawawezi hata kupima utendaji wa chama
chao kwa miaka 25 iliyopita na kupata jibu wapi tulitakiwa tuwepo,

Tumechoka na chakula kimoja, tunahitaji mabadiliko, Zambia
wamewezaje!! Kama CCM wanaamini wao ni wazuri na hawahitaji kujieleza
sana, vyema wakawaachia wengine tuone ubaya wao. Thamani ya kitu
huonekana ukikikosa.

Lowassa ni mnyama mbaya kama walewale wengine CCM, Nikipewa jibu kwa
nini anang'ang'ania urais kwa kutumia pesa nyingi kutengeneza mizizi
ntatulia, na pia mbona hakumbushii utendaji wake yeye binafsi bali
wengine ndio mnamsaidia!! mwacheni atape tape kivyake.

--
*"Anyone who conducts an argument by appealing to authority is not using
his intelligence; he is just using his memory." Leonardo daa Vinci
*

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment