Saturday 16 March 2013

Re: [wanabidii] Re: FIDIA BARABARA YA SERENGETI-SERIKALI YETU INAWAZA NINI?


Sijapata muda wa kusoma wapi uwanja wa ndege wa Kimataifa utajengwa serengeti. Lakini ninafahamu kuwa kuna uwanja Loliondo ambao ndege za kukodi na za hunter na nyinginezo zikitua. Huo uwanja upo maeneo ya mbuga za wanyama ambao ilikuwa ni hatari kutua hapo kutokana na wanyama kuwepo uwanjani. Mwarabu OBC wa kampuni ya uwindaji huko, pamoja na mafao mengine aliyokitoa ni kuukarabati uwanja huo na kuweka fence (kama bado ipo).

Kama umewahi kuwenda Loliondo kutokea Arusha au Mugumu-Robanda basi utaelewa jinsi maendeleo yanavyokuwa magumu bila barabara ya kudumu.

Mbona Ukitoka South Africa kwenda Botswana unapita mbuga za wanyama na barabara ya lami. Ukitoka Sirari-Kisumu kwenda Nairobi uwe mwangalifu-Wanyama pori. Na sio kila maendeleo yapitapo ni serikali tu ilipe fidia sio nasi wakati mwingine tuchangie. 

Hata CIUP ya Mijini (DAR) hufanya hivyo kuwafanya baadhi wachangie ktk kuboresha miundo mbinu la eneo kwa kukubali Kiosk au kachumba kabomolewe bila fidia kama mchango wako badala ya tena kuchangia e.g. elfu 3 au kumi za kufika 20% ya total cost ya uboreshaji miundombinu-barabara, nguzo za umeme, soko, public toilet, mitaro ya maji ya mvua.

Ukiangalia kwamba nyumba zipo bondeni (Tandale Mtogole) na zipo mjengo wa L na ukitaka kuondoa maji ni mifereji kila baada ya nyumba. Hii ni gharama kubwa GVT wala donor haiwezi. Hivyo kunaamuliwa strategically mifereji ipite wapi na kuchangia ili gharama isiwe kubwa.

Inategemea na uvunjaji na kinachovunjwa kwa ukubwa na thamani yake. Kila kijiji huko Loliondo/Serengeti vinasifika kuwa na NGO za kigeni. Mbona maendeleo duni. wapo kazi yao instigation of conflict na tumboni street Mmasai yupo pale pale? Hao ndio waliotia chokochoko Ihefu/Kilombero. Na miladi ya maendeleo kuhisaniwa Ihefu na mashirika ya nje. Ilifika serikali ikaona basi-mazingira yanakwisha mchezo hakuna waondoke. Donors na NGO nyingine tata. Baadhi walifikia mpaka kuhamasisha eti Mbuga ya Serengeti wapewe Wamasai na Mkomazi pia ndio haki zao za binadamu wanazotetea. Imekula kwao hadi leo!!  Ila huwasikii kusema-Mikumi National Park wapewe Warugulu na Wasagala, Ruaha wahehe (Wakaseme wapewe Wamasai na Miradi ya Mbomipa etc); Hawasemi Seleou Kusini wapewe wangoni. Hao wakenya wakitangaza Serikali ipo kwao Kenya. GVT imefanya juhudi ya kuitangaza ipo TZ. Sasa hao ndio wa kutetea Wamasai na barabara wakati wageni wakilala kwao kuja kuangalia wanyama na kurudi kenya hela inakuzamia? Loliondo Misitu imekwisha kukatwa malundo ya mbao za mloliondo unakuta mpakani kubebwa kwenda Kenya pia biashara za rombo na maeneo mengine mpakani nao. Hao wanautetezi hasa na nchi hii na wakazi wake au kujaza tumbo? Mbona kwao ardhi na misitu ni mali binafsi maeneo mingi, ukabila na mipambano kwetu ndio watetezi.

Wamasaai nao wanataka maendeleo. Warudi kwao hizo NGO za kigeni maana nao kwao wanamatatizo ya jamii kibao. Kwani Yellowstone N.Park haifikiwi na barabara za lami bali vumbi tu? Mbona misitu mikubwa miji yao na wanyama wanavuka barabara za lami na hata mbwa mwitu/bweha kuingia majumbani kutafuna mtoto. Lami na taa za kuwaka mbona hazizuii mbweha, dubu kuingia majumbani. hata kinguchiro kinavamia uwanja wa mpira na kuuma watu. Sisi lami ndi tatizo wanyama watakufa?

Wangejua hao wakenya-Conservation biology ktk research zake imeonyesha wanyama wapo wengi jirani na makazi ya binadamu kutokana na tegemezi binadamu anafanya modification ya ardhi inawapa varieties za majani ya lishe. Wapo wachache ndani ya mbuga kabisa. Ndio kukaanzishwa academic area/sector  iliyozaa sera na strategies za  Community conservation/Wildlife conservation with community participation kuondoa dhana ya Yellowstone model ya total exclusion ya binadamu. Na ndio maana tuna mikakati ya WMAs (Wildlife management Areas) na kufundisha wildlife Scouts/Community or village scouts; tented camps kijijini etc. Waache wanyama waishi na binadamu. Binadamu alinde wanyama ila afaidike na uhifadhi (benefit sharing). na hata ukiwa Rhino Lodge au hoteli za kitalii-usiku wanyama wenye watoto wanajaa hapo uwanja na kuzunguka hoteli ili kukimbia kuliwa porini. Ukijenga bwawa la maji ya mifugo-umewaita kuja kunywa na kuhamia hapo. Ni risasi zitakaowakimbiza sio barabara ya lami mradi tu kuwe na control ya trafiki na kutupa uchafu hovyo na uwindaji haramu. Wakenya watuache!!

Ndugu zetu wamasai wakubali mabadiliko na waamue yanayowafaa kwa kushirikiana na viongozi wao wa mila, serikali na wabunge waliowachagua.

Tusisahau pia, hata katika maisha ya mbali vijijini kuna ubadhilifu na watu wenye ubinafsi na ufisadi. Ndio maana ktk mila na desturi unakuta mjomba, babu, baba mdogo, shangazi anadhulumu mali na kuwaacha mayatima na mjane wanateseka kisa-Mila kumbe ubinafsi.

Wakati inatungwa Serendeti Regional Conservation Strategy-1994, Sisi tulipita hoteli za kitalii  wilaya zinazozunguka Mbuga ya Serengeti nje na ndani ya Mbuga, hadi Loliondo, Maswa GR, Grumeti etc na vijiji yake. Tuliangalia hela za Halmashauri za GVT na zile zitokazo uhifadhi-makampuni ya uwindaji na NCAA- kama mafao ya wananchi waishia ndani na nje ya hifadhi. Mamilioni ya NCAA na hela za toka Hoteli tulichukua nakala ya cheki-hundi kutoka mahoteli-Kituko ukiangalia matumizi vijijini na baadhi ya wilaya. Hata katika grassroot level-jamii inayotetea kuwa inaonewa- tulikuta ufisadi katika uongozi wa mila na kuhojiwa hawataki wanapandisha mori.  Mid 1990 humo ndani ya Serengeti walifukuzwa wahusika wa NGO fulani kutokana na kuhamasisha uchochezi ktk ya GVT/Mbuga ya Hifadhi na wakazi.  Baadhi yao walifika UK kutoa mada na kuhamasisha DFID isitoe Grants na hela nyingine TZ. Waliitaka hivyo kwa kesi ya Mkomazi na bila ya shaka kuondolewa watu Ihefu. Hizi NGO ni za kuangalia.   

Utaona pia desturi zetu. Wanavijiji wakiona mhoji ni Mtanzania, wakazi maeneo mengine huwa wema wasikivu na kujadili vitu kiuhalisi. Akifika wa NGO hasa za mataifa ya wageni-utaona wanapamba moto hawaonyesi mema ya GVT na misaada, project zake ilizozigharimia bali ni shutuma tu ili wapate fedha zaidi. Akija mhisani mwingine-yaani ni balaa, hakuna msaada wowote ni zero maisha yao yote. Matokeo ni marudio ya miradi isiyoendelevu, kupoteza hela na watu kuonyesha miradi sio halisi kwa wahisani/wasaidiaji. Bora kuwa na shukrani. Mradi wako anaonyeshwa huyu na yule. Siku mkikutana wote hapo na kuna ukaguzi basi ninyi donors mtaona maajabu. Intersectoral collaboration, coordinated planning ni muhimu na kugawana maeneo ya miradi msirudie rudie eneo moja. Kuna haja ya kupunguza power ya watu wa nje kuingilia mambo yetu nchini na kuchanganya waanchi. Ona safari ya Mh Tibaijuka ilivyoonyesha uvamizi wa mbuga, kulima mazao, kukata miti etc. Sasa huo uharibifu wa eneo ni serikali na barabara tu? Hiyo overgrazing, extensive farming na ukataji miti ni kitu gani?

Hivyo-tangulia kufanya utafiti wa kina (Insitututional survey) upate data na ufahamu wa eneo, kisha ndio ufike kijijini kupata primary data. Ajabu tuliona-vijana (wenye influence wa vyama vya harakati vya ndani na nje-NGO) wanaweza kukemea mzee anayesimama kuongea ukweli. Mila zimebadilika.

Tujitetee wenyewe wakenya watetee yao. Hata wamasaai wanataka maendeleo. Umbali ni mkubwa mno ukitoka Loliondo kwenda pande zote au NCAA na kata ziishisho waannchi kwenda Mugumu, Musoma, Mwanza au Arusha. Mchanga, tope na kukwana kutaongeza vifo vya akina mama. Barabara ni muhimu. Wakenya wakatatue matatizo ya squatter areas kwao na land use conflicts, tribalism etc. Watuache.

+255762544553/754763803

--- On Sat, 16/3/13, Yona Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:

From: Yona Maro <oldmoshi@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] Re: FIDIA BARABARA YA SERENGETI-SERIKALI YETU INAWAZA NINI?
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Saturday, 16 March, 2013, 18:16

Mbona kuna hata mashtaka mengine dhidi ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa serengeti sio barabara tu na hatuna ujanja ni sisi wenyewe tumekubali kuingia kwenye jumuiya hizi na hata mikataba mengine ya biashara za kimataifa 


Kuhusu friends of serengeti hao wanaofadhili miradi ya maendeleo checki http://friendsofserengeti.org/

2013/3/16 <chachamairi@gmail.com>
Bw. Maro!
Naelewa si vema kujadili suala ambalo lipo Mahakamani, lakini nimesikitika sana kusikia taarifa hizo kupitia kwako kuwa kuna NGO ambayo imetoa fedha kwa baadhi ya wananchi wa serengeti, ili wasidai barabara!

Naweza kusema kuwa huo ni ulaghai na utapeli ongeza usaliti dhidi ya wana serengeti! Maendeleo bila miundo mbinu ya barabara? Hata mtoto wa chekechea hawezi kudanganyika na upumbavu wa aina hiyo!

Katika shauri hilo, ni nani anayewawakilisha wakazi wa serengeti? Naomba hao walioandika proposals na kilaghai na kuchukua fedha za wazungu kwa maslahi yao binafsi, huku wakiwadanganya kuwa wamezitoa kwa wakazi wa serengeti, wakome kutumia fursa hiyo kutunyima maendeleo yetu na vizazi vyetu! Wakumbuke iko siku tutalazimika kuwatoa kafara kama wakina Ken wa Jimbo Ogoni huko Nigeria!

Tunaomba serikali yetu iendelee na mchakato wa mradi huo wa ujenzi wa barabara, huku serikali ikihakikisha haki za watu waliofuatwa na barabara na kufanyiwa tathmini ya mali zao, wanapata haki zao kwa mujibu wa sheria!

 ----------
Sent from my Nokia phone

------Original message------
From: Yona Maro <oldmoshi@gmail.com>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, March 16, 2013 8:15:33 PM GMT+0300
Subject: Re: [wanabidii] RE: FIDIA BARABARA YA SERENGETI-SERIKALI YETU INAWAZA NINI?

Ndugu Mairi

Hili suala liko mahakamani na waliopeleka suala hili mahakamani ni NGO moja
ya nchi jirani ambayo imefadhili miradi kadhaa ya maendeleo kwa wananchi
wanaoishi karibu na maeneo ambayo barabara inategemewa kujengwa ili
wasiweze tena kudai hiyo na pengine hata kuuonyesha ulimwengu kwamba
maendeleo yanawezekana bila barabara hiyo kupitishwa mbugani , Sasa tuache
sheria ichukuwe mkondo wake .

2013/3/16 <chachamairi@gmail.com>

> Naomba kuweka hoja hii wazi mbele ya Wanabidii, ili kupata mtazamo wa
> watanzania wengine, na labda kupata ushauri nasaha kwa pande zote husika.
>
> Awali, nitoe maelezo kuwa, mnamo mwezi Julai 2010 ilifanyika tathmini kwa
> Wananchi waliokuwa wameguswa na mradi huo wa barabara kwa nyumba zao na
> mali nyingine kuwekewa alama ya X kama ishara kuwa sasa hawaruhusiwi
> kufanya maendelezo ya aina yoyote ikiwemo ukarabati wa nyumba!
>
> Wakati huo, yalitolewa maelekezo kutoka kwa viongozi kadhaa wa kitaaluma
> na kisiasa kuwa, fidia ingelipwa ndani ya kipindi cha miezi sita.
>
> Kwa niaba ya waathiriwa wa mradi huo wa barabara, nasikitika kuandika
> kuwa, mpaka sasa hakuna fidia iliyolipwa, na hakuna maelezo wala maelekezo
> kutoka kwa viongozi wataaluma na wasiasa kwa waathiriwa nini cha kufanya!
>
> Linalosikitisha zaidi ni kuwa, baadhi ya nyumba sasa zimeanza kutengeneza
> nyufa na kuanguka, huku wenye nazo wakiogopa kuingia gharama ambayo
> haitambuliki na tathmini iliyokwisha fanyika mwaka 2010!
>
> Wanabidii wenye taaluma ya sheria, naomba waone umuhimu wa kuwashauri
> wahusika wa pande zote, yaani serikali itoe tamko juu ya mradi huo na
> tathmini hiyo. Aidha, watoe ushauri kwa waathiriwa nini cha kufanya ili
> kutetea haki zao ambazo kwa sasa zimecheleweshwa, kitendo ambacho ni sawa
> na kuzipoteza!
>
> Naomba kuwasilisha!
>
>  ----------
> Sent from my Nokia phone
>
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>
>


--
www.wejobs.blogspot.com Jobs in Africa
www.jobsunited.blogspot.com International Job Opportunities
www.naombakazi.blogspot.com

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.



--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.





--
www.wejobs.blogspot.com Jobs in Africa
www.jobsunited.blogspot.com International Job Opportunities

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment