Sunday 17 March 2013

Re: [wanabidii] Re: FIDIA BARABARA YA SERENGETI-SERIKALI YETU INAWAZA NINI?


Na ndio maana Africa VITA kila siku ipo kuoneana na kudhalilishana. Mitazamo yetu ina matatizo. Kuna kitu ndani yetu ambacho sijui kitabadilikaje afrika na TZ tupate kwenda mbele kwa amani. Ona wanavyoharibu  DRC kuonea watoto akina mama na akina baba. Yaani awatie vilema, kubaka na kuambukiza ukimwi-kudhalilisha mzazi mbele ya watoto na ndugu, kuwafanya kupotesa mali na identity yao wanatangatanga maisha kisha wakuchague uwe kiongozi wa nchi. Angalia Libya, Misri-wamepata nini? Mali, Nigeria kinachoendelea. Syria-havisemeki.  Hawaoni mifano na sisi hatuoni. Tusipozingatia sheria za ujenzi, kilimo, ufugaji, ulinzi wa mali asili, ardhi mijini na vijijini itakula kwetu. Sio viongozi pekee wenye matatizo, na sisi jamii tumo.

Nani ktk familia yake asiyejua kujenga kando ya barabara ni hatari, accident, lori kuparamia, kifo au kilema? Kuwa, kuwa kuuza ardhi hovyo, kuuza mali halafu ukahamie mahara pabovu ni gharama ya maisha. Aliyepitiwa na mafuriko Jangwani, akapanda juu ya paa, akapoteza family members hajui ubaya ya kuishi hapo. Aliye kariakoo aliyeona mafuriko ya mabondeni, anawezaje tena kuuza nyumba ya vyumba sita kwa millioni 500 hadi billioni 1 iliyokuwa ya gharama ya 60,000/= NHC ilipojemngwa 1970s halafu ahamie Mchikichini, Jangwani bondeni? hela hii wakigawana ndugu waliorithi nyumba kila mtu millioni 200 tuseme akienda mkuranga, mlonganzila kibaha, bunju atafanya mangapi ya maana. Atapata eneo na kishamba cha kulima mbogamboga, atanunua bajaji anazotaka  kwa milioni 6 anapata ngapi hata na pickup ndogo ya kuikarabati kupelekea mboga na matunda sokoni DSM; mbuzi na ng'ombe wa waziwa walili watatu, nyumba nzuri na kusomesha kajukuu. Kiongozi wa Taifa anaingiaje hapa kumsababishia matatizo kama si yeye mwenyewe na kubweteka akili na mwili. Mchiriku na dhahabu, khanga za kujionyesha, vileo na kuhamia lodging aibiwe na pesa kama ni baba anatumwa na nani? haoni wivu wa maendeleo kwa wenzake?

Unakarabatiwa eneo lililokuwa linaleta maji ya kinyesi na taka kujaa ndani ya nyumba. Kisha unauza unahamia bondeni zaidi-Kiongozi aliyefanikisha hili kutokea hata mkapata na daraja la kupita juu mafuriko yasiwazuie watoto kwenda shule (lipo Sunna jangwani) anahusije kukufanya wewe usahau tabu ya kujaa maji ya vinyesi ndani ya nyumba-uuze, uhamie kwenye kinyesi zaidi? Unaona kabisa kipimo cha ukomo wa barabara na jiwe limewekwa na kiongozi/GVT-unaling'oa, unajenga barabarani palipokatazwa. Likibomolewa hasara ni ya Kiongozi au wewe uliyempa rushwa muhusika upate Title Deed. Itakula kwako. Mwenye macho haambiwi tazama.

Imefika wakati sisi waafrika ktk kaya/familia zetu tujikanye. Tuongee na watu wetu kuwapa maarifa na maadili. Ama sivyo tutakuwa masikini daima kutokana na vitendo vyetu plus na vya viongozi sio waadilifu. Na ndio maana, kutokana na pumba kichwani baadhi yetu Mume kambaka mdogo wako-unamtolea dhamana kumtetea. Mdogo wako kalawiti katoto kako-unamalizia nyumbani kisiri badala ya kumpeleka akalambe miaka.kafanya hivyo jirani yako-unachukua senti yaishe ila mtoto keshakuambikizwa na kuharibiwa kisaikolojia. Kakupiga kakukata kidole au mkono-unamsamehe unarudi huko huko na ndugu na jamaa wanakushinikiza rudi huko huko. Hapa ni serikali au jamii na mitazamo yake licha ya mafundisho ya GVT na vyama vinginevyo ya haki za binadamu ila ushirikiano na familia/jamii mdogo. Na hivi ndivyo unavyopata kuona mfano Mara Region inamifugo mingi, kahawa, ziwa, madini lakini inaongoza ktk poverty index, mila potofu za ukosefu wa haki za binadamu na mapigano ya kuuana daima, ina wanajeshi wengi mpaka wastaafu, police na wanasheria. Jiulize-Kulikoni?

Unaona kabisa misitu ikikatwa maji yanakosekana-unawaahidi kuwapa msitu na kuwaruhusu wagange njaa kwa kukata miti kuuza mbao na mkaa badala ya kuhimiza kilimo na ufugaji endelevu na alternative livelihoods kama kilimo cha mbogamboga na ufugaji nyuki misituni huko.

Unawaona wanachezea mercury katika maji wanywao wao, mifugo na tunywao sisi-ipo kuwatembelea huko majichoni wachimbaji wako wakuone unawapenda kumbe unawasaidia kukisogeza kifo. Mercury ni 'Neurotoxin', watakufa, kupata matezi ya mwili, kuzaa watoto matufe; nywele kudondoka, kupata kichaa na kitetemo cha mikono, mwili kama parkinsons disease na asiweze kufanya kazi tena. Hivyo jimbo/kata  lako mchaguliwa litaishia. Mimi huweka picha humu za watoto, akina mama, watu wazima akina baba, vijana wanachezea mercury mtoni mito inayoingia Lake Victoria-Geita, Kahama, biharamulo huko Mugusu, Nyangarata, Nyamigele etc. NGOs kama AMREF zimewaelekeza, wajiunge na SACCOS, wapate mikopo wanunue  vifaa vya kisasa vipo wasichezee mercury-NIL, wagumu kuelekezeka kwani Imani za Kishirikina zimetanda. Kila mtu ana kigozi au kifaa chake cha kupata utajiri. Mbona hata magazeti ya TZ yanatangaza vifaa hovyo vya utajiri  BILA AIBU, bila Kujali Utaifa kuwa wanafanya Imani hizo kuwa scientific maana hata gazeti inazitambua. Likifungiwa gazeti la namna hii-Tutailaumu serikali ila kuacha  kuweka matangazo ya ushirikina? Unaweka ktk nyumba yako ukumbini kuonyesha video chafu na umezaa una watoto au ulezi. Una utajiri huo ni mradi wa mama wa kipato. Ni wewe uliegeuza baraza za kutuo cha basi/daladala kuwa meza za chakula, kituo cha bus kuwa soko mabasi pa kupita hakuna abiria wanateseka pa kusimama. Ni kupigana na mgambo kila mala uhame ukakae Makumbusho au machinga building ambako soko ni jeupe mmehamia barabarani. Ni kupigana na mgambo hadi lini? Ifike mahala sisi binadamu tubadilike.

Bila kubadilika kiakili GVT haitoweza kitu. Hata sheria ikiwa kali kiasi gani binadamu lazima abadilike aitii amasivyo ukali wake utaishia kuleta vita sio mabadiliko ya maisha. Jela zitajaa atawalisha nani? GVT haiwezi kuajiri askari idadi sawa na wakazi wa kila kata ili kuweza kupambana nao. Ni sisi bianadamu pia kutii sheria ili iwe rahisi kwa serikali na watumishi wake kutimiza wajibu wao.

Tunapotishia kuwaua mgambo-askari, kuwapiga kwa kuwavamia wanapoondoa bidhaa barabarani-watachukua rushwa daima ili yaishe aondoke asiuawe mtaani maana unaishi naye jirani. Wajamii tunaumia tuonayo yanayoendelea na ni lawama tu pande moja bila kujiona vibanzi vyetu pande zote mbili ili kuwe na mabadiliko chanya.


--- On Sun, 17/3/13, Ephata Nanyaro <nanyaro04@gmail.com> wrote:

From: Ephata Nanyaro <nanyaro04@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] Re: FIDIA BARABARA YA SERENGETI-SERIKALI YETU INAWAZA NINI?
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sunday, 17 March, 2013, 20:51

Ndio gharama za viongozi kuwa ombaomba hata kutawala wameshindwa

2013/3/17 Jovias Mwesiga <ngonzy@gmail.com>
Mi niseme tu mahala popote penye bara bara kuu hakustahili malipo ya
fidia wekeni siasa pembeni labda tu kama kuna re alignement of route
hiyo ni kitu kingine. Mnaitukana serikali mnageuka mnailaumu si sawa


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment