Wednesday 13 March 2013

Re: [wanabidii] MBINU ZAO CHAFU ZIMEDUNDA!

KIGWANGALA BWANA!!
 
Mi nakuomba wewe mh kigwangala utusaidie sisi wananchi wenzako kuandika makala za kitaalamu zitakazosaidia hospitali zetu zisilaze wagonjwa sakafuni kama ilivyo sasa!!!

2013/3/14 <hkigwangalla@gmail.com>
Mrema,

Katika mfumo tulionano ni kweli unategemea serikali ije ikusaidie mtaji wa kuanzisha biashara yako ama shamba lako?

Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

From: Herment Mrema <hmrema11@hotmail.com>
Date: Wed, 13 Mar 2013 20:42:07 +0000
Subject: RE: [wanabidii] MBINU ZAO CHAFU ZIMEDUNDA!

HK

Mbinu sahihi za kuboresha uchumi wetu zimeandikwa sana lakini inaelekea hakuna anayesoma, kusikiliza wala kujali hatma ya nchi hii. Mwarobaini wa kupambana na umaskini wa Mtanzania ni kumjengea uwezo mkulima mdogo kushiriki kupanga bei badala ya kupangiwa bei kwenye inputs na outputs markets.  Hii itatokea ikiwa mkulima anakuwa na kilimo biashara na kujua gharama za uzalishaji, kusindika na kuuza na bei ya anachokiuza ikiwa ana uhakika wa ubora wake, thamani yake, mlaji, ameongezea thamani ya kutosha, uzito wake na wingi wake.

Hili ni jibu rahisi mno la kupambana na umaskini. Kwa wale ambao hawaamini ninachosema wawasiliane na mimi kwa ufafanuzi zaidi. Sasa kama majibu ya matatizo yetu ya umaskini wetu wa akili, roho na mfukoni tunayo kwa nini hayachukuliwi na kutumika kupambana na umaskini na watawala?. Wote tunajua kuwa Tanzania bila umaskini inawezekana na hatuna sababu ya kuwa na umaskini uliokithiri kwa sababu tunazo rasimali lukuki.  Sasa nini hasa tatizo la kutokuendelea ikiwa kweli watawala wana nia njema na nchi yetu hii na watu wake?. 

Haya maneno ya chuki yanatokana na hasira na kuchoka na umaskini wa kujitakia na tafadhali elewa hivyo.

Tafakari

Herment A. Mrema

Date: Wed, 13 Mar 2013 18:52:34 +0200
Subject: Re: [wanabidii] MBINU ZAO CHAFU ZIMEDUNDA!
From: esulle17@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com

Hi habari wala haina uchochozi wote wote kama mtu unaelewa mantiki yake nini. Mbinu chafu zinazotumiwa na vyama ndivyo vinavyorudisha nyuma maendeleo yetu kama taifa. 

2013/3/13 Mohamedi Mtoi <mouddymtoi@gmail.com>
HK.
CCM kuna madaktari na maprofesa walio bobea lakini kila kukicha deni
linazidi kupaa kulikoni mpaka mimba mnaacha zidaiwe?! mbona huji hapa
kuandika makala za kukuza uchumi? kaa kimya mwenetu.

On 3/13/13, xavery njovu <njovucom@gmail.com> wrote:
> DR HK
>
> Unashangaa  nini  hii si ni baba kaenda kazini.  usipoenda  kazini unajua
> watoto watakufa njaa
>
> Regards
> xn
>
> 2013/3/13 <hkigwangalla@gmail.com>
>
>> Mtu una akili na uwezo wa kuandika, kwa nini msiisaidie nchi kwa kuandika
>> habari za kiuchumi na kijamii zitakazoijenga Tanzania ya kesho? Uchochezi
>> huu na ujenzi wa chuki dhidi ya chama tawala vina faida gani kwa nchi
>> yetu?
>> Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania
>> ------------------------------
>> *From: * Gikaro Ryoba <rgikaro@yahoo.com>
>> *Sender: * wanabidii@googlegroups.com
>> *Date: *Wed, 13 Mar 2013 06:06:15 -0700 (PDT)
>> *To: *wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>
>> *ReplyTo: * wanabidii@googlegroups.com
>> *Subject: *[wanabidii] MBINU ZAO CHAFU ZIMEDUNDA!
>>
>> ENZI zile za Luteni Yusuph Makamba, CCM walikwepa sana kutumia polisi
>> moja
>> kwa moja. Hata hawakuwaamini kabisa polisi. Mfano, nakumbuka jinsi
>> Makamba
>> wakati wa uchaguzi mdogo wa 2008 kule Tarime alipotangaza kwamba polisi
>> wa
>> Tarime mchana ni CCM, lakini usiku wanageuka kuwa CHADEMA.
>>
>> Nadhani hiyo ndiyo iliyowapa akili walipokwenda Busanda hawakutaka tena
>> kushughulika na polisi. Wakakusanya wavuta bangi kwenye mitaa ya Manzese
>> na
>> kuwapa mazoezi kisha kuwapeleka Busanda wakiwa wamevalia kininja na kazi
>> yao ikawa moja tu: kutembeza kipigo kwa kila aliyejidai kuipigia debe
>> CHADEMA.
>>
>> Walitembeza ubabe mpaka wakatangazwa washindi wa uchaguzi ule Busanda.
>> Wakati CHADEMA bado hawajashtuka wakaenda na mbinu hizo hizo Biharamulo
>> na
>> kwenyewe wakatangazwa kwa nguvu kuwa washindi.
>> Mbinu nyingine ninayoikumbuka sana ni ile ya kununua wapinzani. Nakumbuka
>> walivyomnunua Tambwe Hizza na Frank Magoba kutoka CUF, Aman Kabourou na
>> Shaibu Akwilombe kutoka CHADEMA na wengineo.
>> Tambwe akapewa kazi ya propaganda kuipiga CUF na upinzani kwa ujumla.
>>
>> Akwilombe kazi ilikuwa moja tu ya kuwaonesha Watanzania kwamba CHADEMA ni
>> chama cha watu wawili tu: Mtei na Ndesamburo. Nakumbuka ilivyokuwa kwenye
>> uchaguzi mdogo wa Tarime 2008. Makamba akapanda jukwaani, akawaambia Wana
>> Tarime: "Mnaponyoosha vidole viwili hewani eleweni maana yake nini. Maana
>> yake CHADEMA ni chama cha watu wawili, yaani Mtei na Ndesamburo.
>>
>> Sasa nitamleta jukwaani Shaibu Akwilombe ili awathibitishie hilo".
>> Akwilombe akapanda jukwaani na kuanza kuhutubia: "Ndugu zangu watu wa
>> Tarime, mara ya mwisho nilipokuja Tarime, nilikuwa na Mbowe, Zitto, …."
>> Mara Makamba akamkatisha akisema, "Akwilombeeee, ninachotaka mimi
>> uwaeleze
>> kwamba chama cha CHADEMA ni cha watu wawili". Akwilombe akasema: "Nakuja
>> huko mheshimiwa katibu mkuu". Akaendelea: "Waheshimiwa Wana wa Tarime,
>> wakati huo nilikuwa Naibu Katibu mkuu wa CHADEMA". Makamba akaingilia
>> kati
>> tena, "Aaaha! Akwilombe waeleze CHADEMA ni chama cha nani?". Ilikuwa kama
>> kichekesho vile, mgosi bwana!
>>
>> Lakini kama kuna kazi kubwa aliifanya Makamba ni kuimarisha kitengo cha
>> makao makuu cha propaganda. Kile kitengo kazi yake ilikuwa kupika
>> majungu,
>> uongo, uzushi, na kila aina ya kashfa kwa wapinzani na kuzisambaza kila
>> leo.
>>
>> Bahati mbaya alipoondoka, katika kile kinachoweza kutafsiriwa kama kutaka
>> kufuta kabisa nyayo zake, waliomfuatia walikifuta kitengo kile na kumfuta
>> kazi yule mgosi mwenzie aliyemweka pale.
>> Waliofuatia walikuja na mbinu ya kutumia polisi. Wanakwenda wanazuia
>> maandamano ya CHADEMA, wanaua watu ili wananchi waogope kuambatana na
>> chama
>> hicho. Tena wakawa wanapiga propaganda kwamba chama hicho ndicho
>> kinachowaua watu.
>>
>> Mungu si Athumani, kule Iringa wakati wanamuua Mwangosi kamera ya
>> mwandishi ikawanasa na kuwaumbua.
>> Mwisho, ikabidi mwenyekiti wako wa taifa awatangazie viongozi
>> waliokurithi
>> kwamba wasitumie polisi maana Watanzania wamekwisha kuwashtukia na sasa
>> kadiri wenzao wanavyouawa na polisi ndivyo wanavyozidi kukiunga mkono
>> chama
>> cha cha upinzani.
>>
>> Wakaja na ya kutumia mawaziri wa serikali. Wakataka kurejea ya mwaka 47
>> ya
>> kuwapeleka mawaziri mikoani kutangaza jinsi serikali ilivyofanya mambo
>> mengi mazuri. Wakaishia kuzomewa na mradi huo ukafa kifo cha mende.
>> Sijui kwa nini hawajamuuliza Makamba maana hata hiyo mbinu aliwahi
>> kuijaribu mwaka 2007 kunadi uzuri wa bajeti ya Zakhia Meghji, wakaishia
>> kupopolewa mawe!
>>
>> Hivi karibuni wakaja na mbinu ya mwaka ambayo ni ghali sana, lakini kama
>> mgonjwa yuko ICU unafanyaje?
>> Nayo ni mbinu ya kununua muda wa hewani kwenye vituo vyote vya
>> televisheni
>> nchini na kutangaza jinsi serikali ya awamu ya nne ilivyoleta maendeleo.
>>
>> Hiyo ndiyo mbinu aliyoingia nayo Kapteni mstaafu Abdullahman Kinana.
>> Naona
>> kama kapteni kuna vitu anafanya ambavyo vinaonekana vya kitoto vile!
>> Yaani
>> mwananchi asione maendeleo kwa macho yake pale kijijini anapoishi ama
>> mtaani anakoishi ama kwenye mji anaoishi mpaka wewe uje umwoneshe picha
>> kwenye kioo cha runinga?
>> Je, ukichukua picha za Dubai ukazitumia kuwadanganya watu wa Musoma
>> kwamba
>> ndivyo mji wa Kigoma Ujiji unavyoonekana leo?
>>
>> Mimi sijui kama hata kuna wananchi katika enzi hizi za dijitali wataacha
>> kuangalia mdahalo wa wagombea urais wa Kenya wakaenda kuangalia porojo za
>> Kapteni Kinana.
>>
>> Hiyo mbinu nayo imekufa. Hela za chama zinaendelea kuteketea lakini
>> ukitaka kujua hivyo vipindi haviangaliwi na watu japo wanajitahidi kutoa
>> matangazo 'live' ya Bunge na kuweka vipindi hivyo, hebu waulize wanapokea
>> maoni mangapi kwa siku ya wananchi wanaoshukuru kwa kuoneshwa maendeleo
>> ya
>> 'picha'?
>>
>> Mbinu ya hivi karibuni kabisa ambayo nayo imeingia mchanga ni ya kutumia
>> uongozi wa Bunge. Spika na Naibu Spika wawabane kabisa wapinzani
>> wasipumue
>> na kupata nafasi hata kiduchu ya kupenyeza hoja zao zenye nguvu.
>> Ha ha ha ha! Hiyo nayo imeingia mchanga. Umati uliojitokeza kwenye
>> mkutano
>> wa CHADEMA Jumapili pale Mwembeyanga kupinga uongozi wa Bunge sijui
>> wanautazamaje. Tunaaminishwa kwamba Makinda ameshapigiwa simu 200 na sms
>> 400 za kumpinga alichokifanya bungeni na kumtaka ajiuzulu.
>>
>> Sijui kama ni kweli lakini muhimu ni kwamba hata hiyo nayo 'imebumba'.
>> Wafanyeje sasa, wameshajaribu hata kurudia mbinu za Makamba lakini
>> imeshindikana.
>>
>> Moja, mbinu ya kununua wapinzani imechuja. Wazungu wanasema ni obsolete
>> (imepitwa na teknolojia). Siku hizi hakuna tena wapinzani wa maana
>> wanaodiriki kununuliwa na kuja CCM.
>>
>> Ndiyo maana kina Kafulila na Danda Juju walioichoka CHADEMA walikwenda
>> NCCR. Siku hizi ni bora kutoka chama kimoja cha upinzani kwenda kingine
>> cha
>> upinzani.
>>
>> Wamegundua kwamba mnapowarudisha kwenu mnawapepea joto kwa muda mfupi tu
>> halafu mnawatupa jalalani.
>> Wamejifunza kwa yaliyomkuta Lamwai, Kabourou, Akwilombe, Hizza, Magoba,
>> Ngawaia, Nsanzugwako, Shitambala na wengineo.
>>
>> Wamerejea CCM na kuuawa kisiasa, hawasikiki tena! Nani tena atafanya huo
>> mchezo? Mimi nilishaazimia siku yakinishinda CHADEMA, kuliko niende CCM
>> ni
>> bora niache siasa.
>>
>> Mbinu ya kutumia maninja nayo imekwama kwa kuwa CHADEMA sasa wana Red
>> Brigade kali kuliko Green Guard.
>> Waliishuhudia Igunga na Arumeru Mashariki mpaka wakasema CHADEMA Igunga
>> iliingiza magaidi kutoka Libya na Arumeru Mashariki walileta Mungiki.
>>
>> Pia wakati wao wamekifuta kitengo cha propaganda na kumkabidhi Nape kazi
>> ya propaganda, CHADEMA wameimarisha Kurugenzi ya Habari na Uenezi.
>>
>> Siku hizi Nape yuko bize kusambaza propaganda, Mnyika yuko bize kusambaza
>> habari njema za matumaini kwa Watanzania kupitia CHADEMA.
>>
>> Ama kweli siku ya kufa nyani miti yote huteleza. Pole Kapteni Kinana.
>> Luteni Makamba wanakukumbuka sana ila wanaona aibu kukurudisha!
>>
>> --
>> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
>> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must
>> be
>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
>> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>> ---
>> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
>> "Wanabidii" group.
>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
>> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

> --
> XAVERY  LANGA  NJOVU
>
> 0783 662681
>
> " IT IS MORE IMPORTANT  TO  USE YOUR  MIND TO THINK  THAN TO USE IT  AS  A
> WAREHOUSE  OF  FACT"
>
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>
>

--
"Tukosoane, Turekebishane, Tuwajibishane, ndipo Tusameheane". Regia Mtema.
--
Mobile: +255 (0) 713 24 67 64
Alternative: +255 (0) 784 24 67 64
Skype: Mohamedi.Mtoi
Twitter: @mohamedimtoi
Facebook: http://www.facebook.com/mouddymtoi
--

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment