Monday 11 March 2013

Re: [wanabidii] Kero na Ushauri kwa mnaotafuta kazi


Sio kukojolea bango to au chini ya bango au kiwambaza mpaka kinatoboka hii si tatizo kwao wahusika. Wanaondoa mifuniko ya mabomba taka (sewer pipes) na kujaza uchafu au kuacha wazi. Mvua ikinyesha na maji kujaa na kuzagaa barabarani wanatumbukia watoto au tunatumbukia wakubwa na kufa au kuumia vibaya. Ila, mvua ikiisha hatufanyi kitu cha kurekebisha.

Tunasahau. Kuna konda/dreva wapiga debe kukaa ndani ya daladala ukaenda haja ndogo ukaitia ktk chupa ya plastiki ukaitupa nje. Watoto waendao shule huokota ili kujaza maji ya kwenda nayo shule.

Bado kuna nyumba za kupanga na maisha magumu mjini lakini raha ni kusema upo DSM city. Chumba kimoja baba na watoto wakubwa na vurugu zote wanasikia.

Hii ndogo sana, kila baada ya nyumba tatu mijini ni Bar jirani na nyumba za makazi viti mpaka barabarani kupitako mabasi na malori. Wakishalewa-chooni mbali haja ndogo ni hapo kiuchochoroni. Nyumba ya pili watoto wapo dirishani wanaangalia lijibaba linakwenda haja. Au, anakwenda katika mti wa umeme, space ya barabara kati yenye majani hapo anakwenda haja na pande anayoelekezea kuna watoto na watu wazima wanauza biashara hata hadi usiku. Maadili hayo.

Nyumba nyingine Video ndio mtaji wa kipato. hii sasa bongo imezagaa. Video nyimgine hazifai kuonwa na watoto lakini kila nyumba ina bango nje la video ya leo. Watoto na wakubwa wanaangalia pamoja mabusu ya ajabu ajabu hata kama si sex lakini hayafai na picha za ngono huonyeshwa. Fika DSM, Igogo Mwanza City, vijijini mfano Kisanga-Kilosa, machimboni haya ni matatizo ya Jamii.

Tumesoma, tupo jirani na mambo haya, yanatukera lakini yanaendelea. Why? Peleka pua yako utumie sheria aadhibiwe uzikwe usionekane-Kisasi. Tunaogopa kufanyiziwa kwa kuchukua sheria maana tunatishiwa na wewe hakimu utakoswakosa kama si wewe mwanao. Haya ndio maendeleo ya waafrika-visasi kama sheria inatumika kikamilifu.

Wanakwenda Choo kikubwa pembeni ya Vyanzo tegemewa vya maji, kuchafua vyanzo vya maji kwa madini mabaya, kuingiza mifugo inakunywa, inaweka kinyesi na mikojo-Sema usikike utapigwa Mkuki uliwe na fisi porini.

Na inyeshe mvua DSM-kina mtu anafungulia choo mnaogelea maji ya kinyesi. Ana saluni-maji kemikali anamwaga barabarani. Watoto wanakanyaka bila viatu mvua ikija tunaogelea wote kemikali na maji yan kinyesi. Bado kutupa mataka ktk mitaro wazi daily. Mvua ikija-maji hayaendi, yanafurika na uchafu wa aina zote yanajaa ndani ya nyumba yake tunaathirika.  hapo sasa ni KELELE na kuita waandishi wa habari.  Mvua ikikatika-anaendelea kutupa tena taka, chupa za plastiki, viroba vya konyagi, kondomu, majivu ya kukaanga chips, viroba vya taka ngumu zisizooza yanayoziba bomba za maji taka za chini ya ardhi pamoja na michanga, nywele alizonyoa watu saluni anatia mtaroni na makorokoro mengineyo.

Kama kipofu vile au hakuona ilivyomuathiri mafuriko yalivyojaa juzi tu na vinyesi na taka za aina zote ndani ya nyumba yake.

Hilo Bango si kitu kama uchafu kama huu ulivyomtesa tena kwa marudio kila mvua inyeshapo-HAUONI  bango ni 'simple'.-VIPOFU lakini wana macho na akili timamu. Hulka ya uchafu, mimakusudi na kichwa ngumu si rahisi kubadili ndugu yangu.

 
--- On Tue, 12/3/13, Jovias Mwesiga <ngonzy@gmail.com> wrote:

From: Jovias Mwesiga <ngonzy@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] Kero na Ushauri kwa mnaotafuta kazi
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tuesday, 12 March, 2013, 3:26

Hawa watu wanaoweza kukojolea bango kubwa lililoandikwa kwa miandishi
mikubwa " USIKOJOE HAPA" sitashangaa kutoweza kusoma yanayotakiwa ili
waombe kazi. Pengine ni mapokeo toka elimu tuliopewa imetuandaa kukata
nyanga sana basi unaonekana kipanga kweli kweli hata vitu simple we
just end up complicating them for no good reasons. Mtu katoka chuo
juzi CV 7pages, real?! Umemfikiria atakaeisoma pia au umeandika tu.
Mie nikushukuru kwa hili angalizo muhimu ila sina uhakika kama bandugu
watasoma manake nalo ni tatizo kwa sasa labda tuombe majina fulani
yachangie hii mada pia just mzaha kidogo

On 3/11/13, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:
> Ninaomba niliweke hili wazi lakini ninaomba lisichukuliwe personal
> zaidi, ni katika kuelimishana na kushauriana kwa mawili matatu
> yanayoweza kuwa katika uwezo wetu.
>
> Naumia sana ninapoambiwa au kusoma post za vijana wenzangu kuwa
> wanatafuta kazi na hawapati au wana-apply sana na hawaitwi hata kwemye
> interview hata moja.
>
> Kama wiki moja iliyopita nilitangaza nafasi za kazi ambazo mimi
> mwenyewe ninazi-monitor application zake (naomba ruhusa yenu nisifanye
> reference ya tangazo hilo), tangazo langu lilikua na maelezo ya kina
> sana juu ya taasisi yetu, aina ya kazi na mazingira ya utendaji kazi.
> Kwenda mbele zaidi nilielekeza namna ya tutuma maombi kwa kirefu
> zaidi, na nikatoa njia mbili tofauti za utumaji wa maombi kama moja
> wapo ingekua na ugumu wake. Mwisho nikaweka namba ya simu pale chini
> kwa lengo la kumsaidia mtu mwenye shida ya ziada kabisa (nashukuru
> walionipigia kwa kutaka maelezo ya ziada).
>
> KERO: Unaachaje kusoma tangazo ulielewe badala yake unapiga simu
> kuniambia umeona namba yangu nikueleze tangazo linahusu nini? Ina
> maana huwa tunaangalia contacts tu katika matangazo ya kazi? Mbaya
> zaidi application procedure iko pale document za msingi unazotakiwa
> kutumia zipo pale lakini bado unafanya unachojiskia wewe... kweli
> mwajiri ahangaike kuiangalia application yako? Unakuta mtu ameombwa
> ajaze application form na ipo pale unaweza kujaza online au
> ukadownload ukajaza, lakini yeye kwa kujiamini kwake ANATUMA cv yake
> then anakwambia "NAOMBA UNIFIKIRIE".. Unakuta mtu ana CV nzuri na
> unahisi kabisa huyu mtu ni ASSET, lakini kama hajui hata namna ya kuji-
> organize yeye mwenyewe, atamfanyia nini mwajiri labda?
>
> Anyways, ninayo mengi ya kushauri vijana wenzangu katika kutafuta
> ajira, lakini naombeni tuwe makini. Tusiwalaumu waajiri kwa kashifa za
> UPENDELEO au KUJUANA. Kwa namna fulani sisi pia tunahusika
> kujipunguzia alama katika ushindani. Katika soko la ajira la sasa
> UMAKINI wa mtafuta kazi ni kitu ambacho kila mwajiri anaangalia tangu
> siku ya kwanza. Niliweza kuwajibu baadhi kwa email zao kuwa wafuate
> utaratibu wa kuomba, lakini naamini kabisa sio kila mwajiri ana muda
> wa kupoteza na watu wasiojielewa.
>
> ---
> andernormans
>
> Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2NGE2JdVQ
>
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>
>

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment