Monday 11 March 2013

RE: [wanabidii] Kero na Ushauri kwa mnaotafuta kazi


Ndugu Abdallah Hamisi

Ninashukuru sana kwa email yako na itasaidia vijana wengi kama watatafuta muda wa kusoma kwani wengi wao hawana muda huo.  Sababu kubwa ni kuwa awakutayarishwa ksoma na kote walikopitia tangu darasa la kwanza mpaka chuo kikuu hawajawa na hamasa ya kusoma na kujua ila wanachokitafuta na maksi na cheti tu basi. Na zaidi ya hapo wamekata tamaa na wanatafuta wa kumlaumu kwa matatizo yao badala ya kupambana nayo.  Bahati mbaya sana na waalimu wenyewe wako pale kutafuta maslahi yao kama ni chuo ni research, consultancy na project management zinazolipa na hawana muda wa kufundisha wala kuhakikisha vijana wao wanasoma.

Hayo ni matatizo ya msingi tunayopata na ttunatakiwa kuyaelewa ili tujipange binafsi na kwa pamoja tubadilike kwani mwisho wa siku ni hawa vijana wanapata shida ya kujiajiri wala kuajiriwa.  Ninakuhakikishia nitashangaa kama nitapata comments zaidi ya moja ya kukubali nilichosema au kukataa ili tujifunze.  Habari ndio hiyo na ndio maanayake.

Tutafakari

Herment A. Mrema

> Date: Mon, 11 Mar 2013 12:21:37 -0700
> Subject: [wanabidii] Kero na Ushauri kwa mnaotafuta kazi
> From: hamisznz@gmail.com
> To: wanabidii@googlegroups.com
>
> Ninaomba niliweke hili wazi lakini ninaomba lisichukuliwe personal
> zaidi, ni katika kuelimishana na kushauriana kwa mawili matatu
> yanayoweza kuwa katika uwezo wetu.
>
> Naumia sana ninapoambiwa au kusoma post za vijana wenzangu kuwa
> wanatafuta kazi na hawapati au wana-apply sana na hawaitwi hata kwemye
> interview hata moja.
>
> Kama wiki moja iliyopita nilitangaza nafasi za kazi ambazo mimi
> mwenyewe ninazi-monitor application zake (naomba ruhusa yenu nisifanye
> reference ya tangazo hilo), tangazo langu lilikua na maelezo ya kina
> sana juu ya taasisi yetu, aina ya kazi na mazingira ya utendaji kazi.
> Kwenda mbele zaidi nilielekeza namna ya tutuma maombi kwa kirefu
> zaidi, na nikatoa njia mbili tofauti za utumaji wa maombi kama moja
> wapo ingekua na ugumu wake. Mwisho nikaweka namba ya simu pale chini
> kwa lengo la kumsaidia mtu mwenye shida ya ziada kabisa (nashukuru
> walionipigia kwa kutaka maelezo ya ziada).
>
> KERO: Unaachaje kusoma tangazo ulielewe badala yake unapiga simu
> kuniambia umeona namba yangu nikueleze tangazo linahusu nini? Ina
> maana huwa tunaangalia contacts tu katika matangazo ya kazi? Mbaya
> zaidi application procedure iko pale document za msingi unazotakiwa
> kutumia zipo pale lakini bado unafanya unachojiskia wewe... kweli
> mwajiri ahangaike kuiangalia application yako? Unakuta mtu ameombwa
> ajaze application form na ipo pale unaweza kujaza online au
> ukadownload ukajaza, lakini yeye kwa kujiamini kwake ANATUMA cv yake
> then anakwambia "NAOMBA UNIFIKIRIE".. Unakuta mtu ana CV nzuri na
> unahisi kabisa huyu mtu ni ASSET, lakini kama hajui hata namna ya kuji-
> organize yeye mwenyewe, atamfanyia nini mwajiri labda?
>
> Anyways, ninayo mengi ya kushauri vijana wenzangu katika kutafuta
> ajira, lakini naombeni tuwe makini. Tusiwalaumu waajiri kwa kashifa za
> UPENDELEO au KUJUANA. Kwa namna fulani sisi pia tunahusika
> kujipunguzia alama katika ushindani. Katika soko la ajira la sasa
> UMAKINI wa mtafuta kazi ni kitu ambacho kila mwajiri anaangalia tangu
> siku ya kwanza. Niliweza kuwajibu baadhi kwa email zao kuwa wafuate
> utaratibu wa kuomba, lakini naamini kabisa sio kila mwajiri ana muda
> wa kupoteza na watu wasiojielewa.
>
> ---
> andernormans
>
> Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2NGE2JdVQ
>
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>

0 comments:

Post a Comment