Monday 11 March 2013

Re: [wanabidii] Jeshi la Polisi mkoani Kagera limefanikiwa kuwaua majambazi saba


Bora walivyouawa. Wangekamatwa wazima na kuingizwa rumande familia zao zingewawekea dhamana bila ya kuangalia madhara waliyofanya na kujieleza wenyewe waliiba wapi na kuua wangapi mahala gani na wangetoka na kutorokea kusikojulikana.
Haki nyingine za binadamu-tata.

Kwani wanaishi nyumba gani kiasi kwamba jamaa zao wasijue kuwa hao ni majambazi? kama ni wageni-wanamakazi kijijini au lodging bila ya hata kushitukiwa na wenyeji? Labda baadhi yao ni wageni na inaweza kuwa wameshauziwa ardhi kijiji fulani na kuonzwa-sifa yetu kama kawaida bongoland 'Mwanangu kaolewa na Mburundi!'.'Kaolewa na Mkongomani!! tunawajaza wenyewe nchini baadae kulalamika tunaonewa na wageni wanatunyanyasa-wamechukua ardhi, wanalima mashamba makubwa na kuharibu misitu bila kujali. Mihela yote waibayo na dhahabu etc kwa nini wasinunue vifaa na kuja na wataalamu wao kama wawekezajihimba madini rasmi. Mbona sera ya madini ipo wazi kwa ngeni na mwenyeji? Cha kushangaza-wataiba leo benki hii, kesho mgoni ule etc. mamilioni yote hayo wanapeleka wapi? Wanawekeza au anasa tu? kama ni mimi ningeiba mara moja tu na kuwekeza ktk utajiri kisha kuokoka nikasali sana na kuanza kutoa mkisaada kanisani, misikitini na katika ajira za vijana na walio na mahitaji muhimu ili Mungu anisamehe. Ingawaje si rahisi ni kujidanganya maana ukiiba urudishe ndio upate msamaha (ndio narudisha kihivyo) Kuua ni dhambi ya mauti haina msamaha. Wao kuiba na kuua daily mbigu gani wataingia?

Na bado, tunajaza wahamiaji haram ndani ya makontena na majumba yetu. Wabongo bwana hatari!!

Na kama hao ni wageni toka Burundi wangekuja kweli na SMG? Naona wangekuja na LMG lenye miguu ya pweza na limkanda lililozunguka kiuno la meta tatu risasi kibao ndani ya bakuli lake na hizo zilizotajwa ni nyongeza tu. Mbona wana silaha za kutisha zaidi ya SMG na LMG? Hao ni wabongo tu. Ina maanisha basi-askari wetu kwa sasa wapewe silaha kali zaidi na nchi iongeze helikopta kuweza kuwazingiwa majambazi wa namna hiyo, wahamiaji haram porini, majangiri na sio tu kutegemea magari kukimbizana nao wakati wao wanajibanza vichochoroni na majumbani. Haja ya kusaidia kuwakimbiza kupitia anga ni muhimu.

Wapeni askari viatu vizuri na sare za kubadili zisizobana waweze kukimbia vizuri maana wanafanya kazi nzuri. pamoja na mapungufu ya baadhi ya askari-hao wapongezwe na wazawadiwe na huo mgodi na serikali kama motisha.

Inabidi tuwe kama China. Umuhimu wa kuwa na askari wa kimo kirefu (Mara inashinda suala hili sio Morogoro); wembamba wasio na matumbo/vitambi maana kukimbizana na majambazi si mchezo au kukimbia waandamanani wanapokimbiza askari. China sasa inamtaka askari mnene mwenye kitambi-aachie ngazi. Kiwe Kigezo kwetu pia na kuwapigisha gwaride daily. Ingefaa warejeshwe ktk makambi yao kama ilivyokuwa ukoloni wasikae Uswahilini maana huko ni chips, beer, pilau na kuongezeka vitambi no gwaride daily labda kero za empowered women at home na za baba mwenye nyumba kudai kodi kabla ya mwezi kuisha. Wakiwa kambini-hawatoweza kukwepa zoezi la mbio daily na kuongezeka vitambi na nguo kubana. Tuwape hongera sana na wazawadiwe. Mungu ibariki TZ.

--- On Mon, 11/3/13, Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:

From: Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>
Subject: [wanabidii] Jeshi la Polisi mkoani Kagera limefanikiwa kuwaua majambazi saba
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, 11 March, 2013, 17:40

Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Kagera.*

Jeshi la Polisi mkoani Kagera limefanikiwa kuwaua majambazi saba
wakati wa mapambano makali ya kurushiana risasi na Askari wa Jeshi la
Polisi wakati majambazi hao walipokuwa katika harakati za kuvamia
mgodi wa Tulawaka ambapo baada ya kupekuliwa walikutwa na bunduki
mbili za kivita aina ya SMG, mabomu matatu ya kurusha kwa mkono,
risasi 156, magazine tano, simu mbili pamoja na fedha za Burundi franc
800.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment