Wednesday 6 March 2013

Re: [wanabidii] HASARA ZA MOTO ANALIPA NANI?


Pata MSONGO ndugu yangu Kessy na MSONGO utaongezeka soon mwisho tutakupeleka India kwa matibabu maana msongo ni mbaya kwa afya yako.

Matukio bado yaja, yaje tu yatubadilishe akili na utendaji wetu sasa sio baadae maana majumba na biashara zinaota kama uyoga. Kubomoa nyumba daily ni kutangaza vita vibaya kati ya serikali na watu wake. Tumebomoa mara ngani na bado vimerudi? Why sisi watanzania tu watukutu na usalama ni wetu? Inakera.

Mara nyingi nami humu huonyesha utata/Usongo wangu na kusema-Jamani tuna macho ila hatuoni tu VIPOFU. Nataja maeneo yaliyopimwa mpaka ya World Bank funded Sites and Services (Sinza, Tegeta Tangi Bovu etc) na mengineyo.

Kijiji cha Mzee Nyerere-Mwenge kilivyokuwa kimepangika na maeneo ya kucheza watoto, eneo la Ofisi ya Ushirika etc nyumba design moja. Magomeni, Mburahati, Tandika huko Temeke Ilala-kumepimwa  kukajengwa nyumba za NHC. Ikaja Squatter upgrading na mfanio Buguruni na maeneo mengine badala ya squatter demolition kama zilivyofanya nchi nyingine zinazoendelea.

Tumetoka huko na NHC na Register of Building; Nyumba za vyumba 6 na zile ndogo; Tumeingia  EPM (environmental planning (for protection) and management); Tukaingia SUDPF chini ya UNDP-habitat (Strategic Urban Development Framework). Bongoland ikavuma na miradi ya Habitat-Sustainable Cities Duniani.

Sasa tupo katika Community Infrastructural Upgrading (CIUP) chini ya City Council na Halmashauri yake. Pendezesha unplanned areas na maji, umeme, water user associations (WUA), vyoo vya kulipia, barabara na mifereji ya maji ya mvua na mapicha yake hadi ya uwanja wa fisi mifereji safi nikayaweka humu ya DSM. Mapicha ya WUA (matangi ya maji)  Mazese kwa Jongo, uwanja wa Fisi, Kibaha, Bagamoyo. Wapi efforts za mkopo mkubwa wa rehabilitation of Sewerage and Drainage System of DSM kukaundwa DSD baadae DSSD sasa Dawasa na Dawasco. pamoja na matatizo yao hao wote, mikopo na shughuli hizi urban towns za bongoland- Wananchi sisi wa bongoland ni VIPOFU na tutaangamia. Hatushauriki-tunajiua, hausikii wala kujifunza-Tunajiangamiza.

Kote kulikopimwa na mtu ana hati amebadilisha matumizi mwenyewe, amejenga ameziba njia na kila mtu anajenda anaziba pa kupita hata pa usalama wake mwenyewe. Kulikopimwa kukaa vizuri ni MAKOROKORO, DSM ni Mji wa makorokoro kila kona. toka kona moja kumezibwa maduka hakuna pa kupita hata wakati wa hatari ni duka, nondo ni vichochoro sio barabara. Kuunganisha vyoo ktk open drain na mapicha ya matende wanaonyeshwa. Kuchukua mifuniko kutumia kuuza kama chuma chakavu na manholes kutumbukiza viroba vya uchafu-maganda ya viazi vya chips, magome ya miti ya vinyago etc ili usilipe mcahngo wa uzoaji taka wa CBO yako mtaani. Kiongozi wa mtaa na kamati wakikuita kukupa ukweli na kukupeleka kwa wahusika-unaanza kutishia na bastoma, na vitisho vingi. Wachafu, wachafu. Tumeziba njia, tumebananisha eti kuganga njaa-ubishi mtupi. Vinchi vidogo vinatushinda kwa utii wa sheria.

Hapa pamebananishwa majengo ya kuganga njaa ni maduka, kuna saluni, internet, bar ya vileo, next hoteli ndefu ya ghorofa kichochoroni nje kuna moto unawaka nyama choma mafuta ya moto yanaruka na joto kubwa next to a pharmacy ambayo inadawa za kuripuka.Inafuata duka la madawa ya mifugo, la vyakula lina mafuta ya taa, ya kupita, inaingia duka la vipipa vya gas, linakuja duka kichochoro la magunia ya mitumba la nguo na zahanati jirani yake.

Akili finyu kama hapo pana flammables na mtu nje anachoma mahindi, mabasi ndio njia yao ya kukatiza na jirani kuna petrol station. Bomoa leo, wahamishe kesho wanarudi!! na wewe mmomoaji si unakaa mtaa jirani na police umepanga uswahilini-itakula kwako atakuletea vibaka wakukate mapanga. Ndio maana watendaji huachia kwa kuogopa kufa, tunafanya tutakavyo au tunawapa rushwa watuache.

Bado hayo maghorofa-husema iko siku watu watachupa kutoka juu hatuna helikopta ya zima moto. Mnajenga ghorofa 50-80. Umeme wenyewe ndio huu wa maandamano ili utose na maji ndio hayo pia. Kisha, kiwanja cha kubeba nyumba moja iliyokuwa na NHC vyumba zita sasa ina ghorofa nene, zito, refu na yanazidi kujaa. Jee, carrying capacity ya ardhi ambayo inachimbwa poa boreholes na wahusika kupampu maji ipoje? Mmepima uwezo wa ardhi au ni kujali kupata hela na ufahari wa mizigo ya nyumba. Mnaweka mipasuko ardhini, mtatumbukia na majumba yenu na kutoka msitegemee mpaka waje kutoka South Africa kama ile MV Bukoba. Mito mikubwa inaingia Dar kupita chini ya ardhi. Kazi ni kupampu na kufanya ardhi iwe na mapungufu na majumba yapate ufa kwa kuondoa balance chini tupate ahali za maghorofa kwanza ujenzi umechakachuliwa.

Huko Mbezi Low Density areas ndio balaa, plot imezibwa yote badala ya kujengwa 40% imejengwa 100%. overload katika mfumo wa maji safi, maji taka, umeme, solid waste disposal. Mtu mmoja kwa siku hutoa kilo moja ya kinyesi. makisio ya 20%  kwa mwaka ya upana wa sewer pipe yamepitwa mara 100% kwa ujazo wa plot 100%, kinyesi chenyewe cha ugali mgumu na matambala humo ktk mfumo vitaacha kukwama visifurike barabarani? Bado taka zinazotupwa ktk open drains. AIBU.

Kama hujui kujilipia BIMA ya Afya na BIMA ya maisha na BIMA ya Nyumba au mali zao Kessy-Itakula kwako huo moto wa weleding next door ya moto wa Chip na wa saluni utakapolipuka halafu usingizie-TANESCO. Ni ukipofu hatuoni au???

Kama una kiwanda, biashara, gari etc-BIMA ya ofisi na biashara na mali zako inauzwa. Jihami kabla ya hatari. Mtu unakiwanda cha viwaka moto kama madawa-utakosaje Bima? Likianguka box la madawa tu linaweza kiripuka. Au-WAMEIBA, wanafanya shoti ya umeme kuwake ili iwe kisingizio-jee, hujapata hasara kiwandani au dukani hapo? Nchi hii ni Bongoland kwa vile watu wanaakili pia ya kuiba kiujanja.

Kuanzisha course ya diploma na sasa degree ya Public Health Engineering na Wizara ya Ardhi katika Chuo Chake cha Ardhi-Ardhi Institute huko nyuma sasa ni University of Lands; kuanzishwa kwa NEMC na Wizara hiyo ya Ardhi na Maendeleo Mijini na kwa DSD/DSSD in 1978-1983 ilitokana na nmambo haya ya usafi wa mji na mazingira. Hata hizo SUDPF, Sustainable Cities ya Mama Kimei akiwa manager mmojawapo, CIUP ya sasa ni masuala ya mipango miji na usafi. Mipango misuri lakini watu wake tupoje sijui. Miji sasa ni makorokoro, garage kila kona, openpace yote ya watoto kucheza-garage, welding ya gate za nondo na madirisha-kisingizio Kujiajiri. Wacha tuwake, madeni ya mikopo tutalipa au tujinyonge, kama tunaona na kujifunza, tukifanya repair na ujenzi mpya -hatutobananisha tena ili gari za uokoaji ziweze kumudu kupita kuzima moto au sisi wenyewe kumudu.

Zingatia building regulation ktk kuhifadhi viwakavyo kusiko joto na uwe na mitungi ya zimamoto na milango ya hatari-pa kutokea. Usichangaye vitu viwakavyo/kuripuka na mapishi yatoayo joto. Nunua Bima. Usikubali kubananisha majengo kama mabehewa ya train. kumewaka Tegeta, Sinza na kutaendelea kuwaka. Tuendelee kuchanganga pia njia ya malori ya mafuta-tankers, containers na magari ya abiria badala ya kuyafanya yapite pekee hayo malori njia ya nje ya mji ya pekee. Yatakuja kuanguka na kuripua mji kama sio eneo kubwa na hatuna uwezo wa uokoaji na uzimaji-Foleni ya magari na nyumba mpaka barabarani-tatizo.

Building regulations zinakutawa uwe na smoke detectors, alarm system na mfumo wako wa kuzima moto uanze automatikali kwenye jengo inapofiti kiwango fulani cha heat na system yako ya njia za hatari zifunguke watu watoke za kawaida zifunge. Hao mainjijia wa majengo ya viwanda, taasisi na maghorofa wamesomea ujenzi wapi? Kama una Bima na umejiunganisha kwa kampuni fulani ya zima mpto, mara alarm ikianza kulia kwako, inatakiwa ilie na kule, wao wataona na wanajua nyumba na mtaa wake wanakuja strait. Kama ni kupima vifaa vyako-budi uwaambie kuwa leo chuoni/kiwandani kwako unafanya fire drill. Watakuja lakini wakijua ni zoezi tu. Kama tuankwenda ktk maendeleo ya ghorofa-Budi tuzingatie building regulations. Usasa tunataka lakini pia tunataka tubaki-chokoraa, mbanano wa majumba na etc haiji Kessy!! Tutawaka tu daily na tutazimia-inasaidia? Utajilipa mwenyewe sio serikali.

TUFUNGUKE macho na akili, tujifunze kutoka makosa yetu.





--- On Wed, 6/3/13, Sylvanus Kessy <frkessy@yahoo.com> wrote:

From: Sylvanus Kessy <frkessy@yahoo.com>
Subject: [wanabidii] HASARA ZA MOTO ANALIPA NANI?
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, 6 March, 2013, 10:54

Ndugu Wanabidii
siku za karibu kumetokea ajali za mara kwa mara za Moto. Morogoro kulitoka moto uliojeuka kuwa sumu watu wakazirai hadi kupelekwa hospital. Mwezi huu pia viwanda kadhaa Dar vimelipuka kwa moto. Jana kiwanda cha Sunda investment na Hawk Security system navyo tulishuhudia vikiteketea.

Swali langu ni kwamba hizi hasara zinasababishwa na nani au nini, na ni nani atalipa na je anayepata hasara ni nani? Au inabaki kusemwa ni hasara basi?

Du, jamani nisaidieni; napatwa msongo mwili wa matukio haya!

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment