Tuesday 12 March 2013

Re: [wanabidii] GARAMA KUMSOMESHA MWANAFUNZI KWA MWAKA NI SH. NGAPI?


Cost per capita itakuwa hela atowayo mzazi tu? Sidhani. Lazina mtu afanye hesabu ya mshahara wa walimu kwa idadi yao kwa shule, maji, umeme na gharama za huduma nyingine kila shuye ya kata kwa mfano kisha ugawanye kwa namba ya wanafunzi. Halafu upate ratio kuona mzazi anachangia kiasi gani. Na hivyo ni kwa miradi mingine mfano wa maji mahala fulani. unaanzia katika exploratory studies-drilling to find water-kila mashine iliyotumika na gharama za mishahara ya waliohusika, kupima maji mpaka kumaliza kufunga borehole, kuweka mantangi, mambomba, umepe kupampu maji na pampu house nyenyewe mpaka maji kufika yanakotakiwa-bomba zote ktk vituo vya umma kijijini. Kisha gawanya na catchment/targeted population say wanakijiji wote wa kata idadi 10,000. Cost per head kiasi gani. Wanakijiji walitakiwa kuchangia capita cost 20% ni kiasi gari selikali ilichangia per head ukitoa hiyo 20%? Hata kama unauguza mgonjwa hospitali mpaka apone. Gharama si ile fee ya hospitali tu-muda wako ambao ulitumia kwenda kurudi na kupanga foleni hospitali (nurse anabofya simu) upo hapo ungefanya mangapi ya kupata kipato? Nauli uliotumia na kuwalipia nauli wengine, chakula kupeleka hospitali mpaka kutoka mgonjwa hospitali na kuuguza mpaka apone.

Kutokuangalia gharama hizi kunatufanya wakati wengine tusione michango ya wengine hata wanaotulea au kutusaidia. unaona hakusaidii lakini toka upo mdogo hadi leo unakula unalala bure. au kutokuwa sensitive na wajibu wetu-kumsomesha mtoto kumpa vifaa una mifugo kadhaa kuchangia mbuzi mmoja shs 50,000/= jengo la shule na vifaa vya mtoto hutaki. lakini unakunywa pombe daily, kuvuta sigara na kusafiri hapa na pale kujiburudisha unakodi pikipiki kijijini kwa mwezi  daily expenditure 5,000 x 30 days 150,000/= na bado hela za mahawara. Hizi huzioni ila unaona 20,000/= ya mchango wa Kata tu.

Kuna watu waliopewa maji safi bure/mradi wa maji hawataki kulipia maji eti mzungu au shirika limetoa facilities hizo kwao bure na kugharimia wao kila gharama. DC anawaelekeza uhumimu wa kulipia maji kwa ndoo-hawataki. Sasa usipolipia  senti 50 leo handpump itakapoharibika au bomba kuharibiwa mtatengenezaje? Operation and maintenance atafanya nani (huyo aliyotoa maji bure) kama sio water user association (WUA) yenu au water committee kuchukua hela hiyo ya maji kutoka bank account yenu kumlipa fundi atengeneze? Wanaandamana hawataki eti walipewa maji bure (tumewaona ktk ITV). Hii ni kutokana na ushirikishaji duni wa wahusika na kutokuwa na mkataba nao, kuweka maazimio na kutiliana mkataba.

Na hata mitaro inapoziba kwa wao wenyewe ktk mtaa kuputa taka na mafuriko kuwadhuru wao maji mpaka ndani ya nyumba-Serikali itusaidie, inaachia maji yanatuama hayatembei inaathiri watoto na sisi wakubwa-changia gharama-No, mjisimamie. Unaunganisha maji taka mtano wazi yanaingia maji hayo ndani ya mamboba ya maji ya kunywa yaliyopasuka na unaona jirani anafanya hiyo mnamuangalia nawe unaona unaua wanao kwa uchafu huo-huwajibiki serikali igharimie. Ila ataumwa mtu hapo uhangaike hizo gharama curative (sio preventive) unazotoa huzioni.

Tumebweteka sasa na hata kuchangia elimu tumebweteka. Ila kuvaa mitumba ghali na kuchangia arusi na sherehe za gharama-twaweza na kwa sasa kuna kima cha chini unaambiwa ni 30,000/= au 50,000/= ndio kima cha chini. Na kwa mwaka unapata kadi kibao nini mchango wa kata 20,000/= cash?



--- On Tue, 12/3/13, Sylvanus Kessy <frkessy@yahoo.com> wrote:

From: Sylvanus Kessy <frkessy@yahoo.com>
Subject: [wanabidii] GARAMA KUMSOMESHA MWANAFUNZI KWA MWAKA NI SH. NGAPI?
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Tuesday, 12 March, 2013, 7:54

Ndg wanabidii
wote mmeshuhudia anguko la kiwango cha Elimu Nchini kutokana na kufeli watoto zaidi ya asilimia 75 ya wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka Jana.

Hali hii inasikitisha kwa kila mtu mwenye mapenzi mema na Taifa letu la Tanzania.

Kwa kupitia mtandao huu ninaomba kama kuna anaweza kufanya mahesabu na kujua Taifa linatumia GARAMA GANI kumsomesha mwanafunzi kwa mwaka, na hatimaye kwa miaka 4. Kwa njia hii tunaweza kufungua macho ya Taifa na pia wanafunzi wenyewe wajue wameliletea Taifa hasara kiasi gani. Na pia itasaidia watu kujua gharama halisi za Elimu kwa kila mtoto. Kwa hali ilivyo sasa kuna hatari ya kudhani kuwa mtoto husomeshwa katika shule ya kata sh 20,000 kwa mwaka. Na hivyo kwa kidato cha 1 hadi 4 ni sh 80,000/-

Naomba anayeweza kufanya hesabu hizi atuwekee kwenye mtandao huu wa jamii. Au Wizara husika ifanya kazi hii.

Naomba kuwakilisha. 

Kessy

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment