Wednesday 13 March 2013

Re: [wanabidii] BUNGE LISILOKUWA NA MENO!

NI KWELI TUMECHAGUA WENYEWE KUWA MASIKINI na viongozi wengi wanafanya watakavyo kwa kuwa wanajua sisi wananchi hatuna la kuwafanya,niwatolee mfano, juzi kule mwembe yanga waziri Temeke wa maji Mheshimiwa Maghembe alisema mishemishe za maji ziko katika hatua za mwisho na mabilioni yametengwa kwa kazi hiyo, sasa tuangalie hapa dar kuna dalili ya maji kupatikana karibuni? ule ni uongo katika nchi zingine huwezi kuahidi jambo kubwa kama hilo harafu hakuna kitu then bado upo unasema wewe ni waziri wananchi wanakuondoa, tumelewa AMANI tusimlaumu mtu, wabunge wa CCM ndo wanaotuletea shida zooote hizi hakuna wa kukwepa. Hebu jiulizeni jamani tuna mito mingi kuliko nchi nyingi duniani eti lakini hatuna maji!!!. tuna misitu iliotukuka lakini eti watoto wetu wanasoma wamekaa chini, tuna dhahabu kila kona ya nchi hii eti lakini sisi ni masikini wa kutupwa, tuna wanyama mapori na mapoli kuliko nchi nyingi duniani eti lakini sisi ni hohehahe wa ukweli!
   Tuna maziwa makubwa na madogo, bahari na milima yenye sifa but eti sisi ni mafukala! tuna ardhi na mabonde yenye rutuba lakini eti tunalia njaa tunasaidiwa na japani, kweli sisi wajinga!!!!!
 
2013/3/13 Jovias Mwesiga <ngonzy@gmail.com>
Kila mstari wa hii habari unatia hasira. Pengine umefika muda
tujinyoshee vidole wenyewe. Wabunge wetu wanafanya kinyume na
tulichotegemea toka kwao. Wanasinzia na hawahudhurii vikao kibaya
zaidi hawaibani na kuishauri serikali kuondoa kero zetu. Kuna mtu
aliuliza hapa jukwaani kwanini watanzania masikini. Haikupita hata dk
1 mh. Zitto akajibu in short "wamechagua kuwa hivyo" unaposoma jibu la
namna hiyo unamuona mbunge huyu akiwa na hasira na amekatishwa tamaa
na anaowapigania na ndivyo ilivyo kwetu wote tusiopenda yanayotokea bt
tatizo ni mwananchi na ubwege wake. Watanzania tumekuwa na kasumba ya
kutoelezana ukweli kwa ukali kisa ati luga ya ustaha na ustarabu ndo
inatakiwa guyz nchi zilizoendelea hakukuwepo upumbavu wa kubembelezana
angalieni akina Obama na wapinzani wao lugha wanazotumia mbele ya CNN
then leo watanzania walala tunaambiwa tuelezane taratibu. Mie mbunge
wangu akimtandika spika ngumi kwa upuuzi wake wa kuendesha bunge niko
radhi nikavamie duka niwekwe jela nae ilinimwambie kafanya vyema.

On 3/13/13, Gikaro Ryoba <rgikaro@yahoo.com> wrote:
>
>
> KIKAO
> kilichomalizika­ cha Bunge kimetuacha tena na mawazo mapya na wengine wetu
> kuturudisha nyuma miaka mingi.
>
> Kwa namna mambo
> yalivyokwenda inaelekea Spika Anne Makinda na naibu wake, Job Ndugai, bado
> wanaamini katika zile zama za chama kushika hatamu.
>
> Hizi ni zile
> zama ambapo kiongozi wa chama katika ngazi yoyote alionekana mwenye mamlaka
> makubwa na katika ngazi ya taifa ilifikia mahali wanazuoni wakaanza
> kulumbana
> kati ya chama na Bunge ni kipi chenye maamuzi ya mwisho na watu wa aina ya
> Pius
> Msekwa walitetea sana hoja ya chama kushika hatamu.
>
> Kwa wakati ule
> wa chama kimoja hilo halikuwa jambo la ajabu sana. Lakini katika mfumo wa
> vyama
> vingi anapotokea yeyote akadhani chama chake kina nafasi kubwa kuliko nguvu
> ya
> wananchi basi ajue ana mawazo mgando na uwezo wake wa kufikiri unatia
> shaka.
>
> Tumewahi
> kulalamika hali hii ya wabunge kuendekeza vyama vyao kwa viwango vya
> kuwasaliti
> wapiga kura wao.
>
> Na wanaoangukia
> katika mtego huu mara nyingi ni wabunge wa Chama Cha Mapinduzi ambao bila
> weledi wanadhani wana jukumu la kuibeba serikali ya chama chao hata kama
> kwa
> kufanya hivyo wanazima hoja za msingi za kuwakwamua wananchi.
>
> Na jambo hili
> hujionesha mara nyingi wabunge hao wanapopewa nafasi ya kuzungumza bungeni.
> Huanza kwa mapambio na kutoa sifa ambazo kwa hakika unaweza kusema
> wanaivika
> serikali kilemba cha ukoka.
>
> Wanajipendekeza­
> kiasi cha kusema wanaunga mkono hoja za serikali asilimia mia kwa mia
> lakini
> kabla ya kumaliza hotuba lazima watazungumza matatizo ambayo kama wanajua
> maana
> ya asilimia mia kwa mia basi wasingekuwa tena na nyongeza kwenye hotuba
> zao.
>
> Inawezekana
> kabisa wabunge hasa wa Chama Cha Mapinduzi wanalazimika kuwa na chembe
> chembe
> za unafiki kutokana na ukweli kwamba kitumbua chao kinategemea maamuzi ya
> chama. Hii pia ni kwa wabunge wa vyama vingine lakini leo sina mjadala
> kuhusu
> hao wengine.
>
> Baada ya kuona
> na kusikia yaliyotokea bungeni katika kikao kilichomalizika­, inafika
> mahali
> unathubutu kuhoji ikiwa wabunge wa CCM na viongozi wao wanafikiri kwa akili
> zao
> wenyewe na kwa manufaa ya waliowapigia kura au bado wamezama katika kusema
> "zidumu fikra za mwenyekiti".
>
> Hoja kama ya
> John Mnyika kuhusu tatizo la maji si hoja inayopaswa kubezwa na mtu yeyote
> anayejigamba kuwa na akili timamu. Asiyejua tatizo la maji ni fisadi
> aliyejitenga na kuishi peponi bila kujua raia wa kawaida wana matatizo
> gani.
> Kwa jambo hilo tu linatosha kumuondolea sifa ya kuwa kiongozi tena
> mwakilishi
> wa watu. Wabunge wanaoshangilia au kuzomea kwa kuangalia mtoa hoja badala
> ya
> kufanya tafakuri ya hoja wameingia bungeni kwa makosa.
>
> Wangestahili
> zaidi kufanya kazi nyingine yoyote inayohitaji kupayuka bila kutia akili.
> Yapo matukio
> mengi mno ambayo Bunge la sasa hivi limeonekana dhahiri kuibeba serikali
> badala
> ya kufanya kazi yake ya kuisimamia na kuibana. Na kuna mtiririko wa matukio
> ambapo Bunge limetafuta sababu za kiufundi kuzuia mbubujiko wa fikra huru
> kujadili jambo.
>
> Bunge limetumia
> visingizio kama suala la kuwapo mahakamani au serikali kuwa inashugulikia
> jambo
> na kuzima hoja za msingi ambazo bila shaka zingeifanya serikali ijikute
> imesimamia vidole gumba!
>
> Katika mazingira
> hayo Bunge limegeuka kuwa ngao ya serikali kupitia kwa watu aina ya William
> Lukuvi wanaonekana kuifurahia mbeleko hiyo.
>
> Ukimdekeza sana
> mtoto anaweza kuwa mjinga. Hali si tofauti sana kwa serikali. Kama serikali
> inafahamu kwamba haiwajibiki na haitawajibishwa­ na chombo chochote lazima
> itabweteka na matokeo yake wengi tayari tumeanza kuyaona.
>
> Kama serikali
> inafahamu kwamba Bunge limegeuka baraza ambalo hata likitoa maelekezo
> imebaki
> ni utashi wa serikali kuyatimiza au kuyakataa. Na mijadala mikubwa ambayo
> kimsingi ingetikisa nchi imeachwa kunyauka bila chochote kutokea.
>
> Na kama Bunge
> halina uwezo au linajinyima uwezo wa kuiwajibisha serikali, uwepo wa Bunge
> ni
> maigizo na ni afadhali lisiwepo kabisa.
>
> Unaweza
> kujiuliza kwa viwango hivi vya kuzuia uchokonozi bungeni kumekuwa na faida
> gani
> hasa katika kuendesha nchi yetu? Kama viongozi wa Bunge ndio vinara wa
> kuzuia
> fikra pevu za kuikosoa serikali kwa kujidai wanatumia kanuni basi ni heri
> kutokuwa na kanuni hizo.
>
> Ni bahati mbaya
> mno unapoona anayeongoza Bunge akifikiri kwamba wajibu wake wa kwanza ni
> kwa
> chama chake. Na aina hii ya Bunge limefanya hata baadhi ya mambo ya
> kisheria
> kuwa kama maigizo tu.
>
> Chukulia mfano
> wa kumthibitisha waziri mkuu bungeni. Kimsingi katika Bunge la aina ya
> Bunge
> letu, rais akishamteua waziri mkuu hoja ya kuthibitishwa bungeni imebaki
> kama
> igizo tu.
>
> Na hata waziri
> mkuu anapokuwa bungeni tumeshuhudia mara kadhaa akipewa kinga na spika ili
> asijibu maswali ambayo yanaonekana kama kumtundika msalabani.
>
> Na haya
> yanafanyika kwa sababu tayari kuna udhaifu mkubwa unaofahamika katika
> serikali.
> Na udhaifu huu unatokana na ulegelege wa Chama Cha Mapinduzi ambacho
> kiukweli
> kimeshindwa kuunda serikali thabiti. Imekuwa serikali inayojikuta imewekwa
> kwenye kona na wapinzani.
>
> Imekuwa serikali
> inayojaribu kufurukuta ili walau ionekane ipo na kuzima kashfa moja baada
> ya
> nyingine. Ni katika Bunge la aina hii ndiyo maana serikali inaweza
> kuchomoka
> katika mambo ya aibu kama kusafirisha wanyama, kuficha hela nje ya nchi,
> kutowajibika kwa mauaji ya raia bila kujali wana hatia au la.
>
> Ni Bunge la aina
> hii ambalo linaweza kunywea pale hoja nzito inapojibiwa kisiasa kwa kusema
> serikali ipo katika mchakato au serikali ni sikivu au pambio lingine lolote
> liwalo. Ndipo tulipofikishwa na wabunge wetu.
>
> Nguvu na mamlaka
> ya Bunge yamebaki katika kurasa na maandishi ya katiba bila nguvu hizo
> kujidhihirisha katika utendaji. Ndiyo maana hata watendaji wengine wakijua
> kuna
> udhaifu huo wameweza hata kuwatuhumu wabunge kula rushwa.
>
> Ndiyo maana
> Bunge hili ambalo linapaswa kuwakilisha wananchi linashindwa kuhoji pale
> risasi
> ya serikali inapotumika kunyofoa uhai wa mwananchi.
>
> Ni Bunge ambalo
> halina nguvu au linajipunja lenyewe nguvu zake, linaweza kufanya kazi ya
> propaganda za kuisifu serikali badala ya kuinyooshea kidole pale
> inapoharibu.
> Na kama Bunge
> letu halitafanya juhudi za makusudi kuvunja ndoa yake na serikali basi kazi
> ya
> Bunge itakuwa haina maana na ni afadhali waende likizo isiyo na malipo.
> Nawasilisha.
>
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>
>

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.



--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment