Thursday 21 March 2013

Re: Re: [wanabidii] TATIZO LA ZITTO ZUBERI KABWE NI NINI ?

Naomba uniitie Yona huko aje ajumuishe mada hii. najua angalau tumeijadili vya kutosha na pahala tusipokubaliana tumepaon na tunapokubaliana.
napenda taratibu ambayo Yona haitumii sana ya kujumuisha mada anazoleta. najua haogopi kuonyessha msimamo wake katika kuhitikisha.
Inapendeza kuona tunao viongozi makini na wanaotofautiana. Hii ni afya njema kisiasa na hata kijamii.

--- On Thu, 3/21/13, ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk> wrote:

From: ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>
Subject: Re: Re: [wanabidii] TATIZO LA ZITTO ZUBERI KABWE NI NINI ?
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, March 21, 2013, 3:29 AM

Muhingo
 
Mimi nafikiri mada hii inapitia kwenu kwa sababu mbili kuu. MOJA: wenzake wanauona uwezo wake mkubwa wa kuangalia mambo na kuyafanyia kazi na kuyatafutia majawabu. Wanauona uwezo wake mkubwa na hivyo kuwa na woga huenda wa kupanga au kujadiliana naye kwa hoja za moja kwa moja.
 
MBILI: kwa upande wa mahasimu nje ya CDM wanazo sababu mbili kuu, moja ambayo na mimi naweza kuwemo ni kule kukubali uwezo wake mkubwa alionao wa kuona mambo, lakini sasa huwezi kumwambia moja kwa moja isipokuwa kutumia njia ambayo inaweza kumsaidia kujua na kugundua mapungufu aliyo nayo ili ayafanyie kazi kisha autumie ujuzi wake kwa ajili ya taifa hili.
 
Ya pili kwa upande huo huenda ni kutaka wenzie ndani ya kundi lao wamchukie jambo ambalo silipi asilimia kubwa sana hasa kwa sababu ambazo nimewahi kusikia mwenyewe akisema. Aliwahi kusema MBUNGE kazi yak ni kuwaletea wananchi maendeleo na kuwashawishi kushirikiana hilo limefanyika na maendeleo kwa Kigoma sasa yanaanza kuonkana, je sasa niseme kwamba hakuna kitu wakati barabara naziona?
 
Wapo waliomwambia wewe pinga tu ndio upinzani huo, kwa kweli hoja hii hakuijibu. Aliyasema haya siku moja akiwa Nguruka na vijana wengi wakiwa wamemzunguka.
 
Yawezekana kweli ikawa kwamba hayuko na wenzake lakini kwangu mimi naiona hoja hii itakuwa kweli tu, kwamba wenzie huenda hawajamulewa zaidi kutokana na tofauti kubwa waliyo nayo katika uwezo wa kuelewa na kutafakari mambo ya kitaifa na kijamii. 
 
K.E.M.S.
From: ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, 21 March 2013, 2:58
Subject: Re: Re: [wanabidii] TATIZO LA ZITTO ZUBERI KABWE NI NINI ?
Kwa ujumla Zito ni mwiba kwa timu yake.
Anazo Character nzuri katika timu kama ulivyosema. Hizo ni 'Functional behaviour' katika team building. Lakini naziona na 'NonFunctional' ambazo zikipakwa manukato zitanukia kama unavyoonesha kusema. Kweli kwa mfano hakushiriki kugomea vikao fulani vya bunge na alitumia njia za kisayansi. lakini kama unaona uhusiano wako na hasimu wako ni mchungu wakati uhusiano wa mchezaji wako na hasimu huyo ni mtamu sana unawezakufanya wanachofanya wenzake. Nasita kulegeza katika hilo licha ya ushawishi ninaouona.
Naelekea kukubaliana na wanaomshuku kuwa huenda akawa hayuko nao.
Lakini nafikiri kwa kuwa wanaye wanastahili kutafuta namna bora ya kumtumia. Ndiyo maana hujawasikia wakimlalamikia directly ila wanapitia kwetu kama na ambao wanamtetea wanapitia kwetu pia. Unafikiri kwa nini kuna mada hii-hasa kwa kupitia chanel iliyotumika(?!?) --- On Thu, 3/21/13, ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk> wrote:

From: ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>
Subject: Re: Re: [wanabidii] TATIZO LA ZITTO ZUBERI KABWE NI NINI ?
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, March 21, 2013, 2:27 AM

Muhingo,
 
Mimi nafikiri hili ni tatizo la kitanzania zaidi au niseme ni la kisiasa zaidi, kwamba mtu akipendwa na hasimu wako basi unapoteza sifa zote za kuwa mwenzi unayeaminika au unayetumainiwa. Mahali pengine ungeweza kuweka uataratibu wa kuangalia ni kitu ganai kutoka kwake unaweza kukitumia kwa manufaa yako. Kwa mfano mtu anaweza kuwa mhamasishaji mzuri katika kuanziasha jambo fulani lakini siyo mzuri katika kulisimamia na kuliendeleza. Ukimuachia mtu kama huo atalisambaratisha lile alilolianzisha.
 
Ninamuona kwa upande mwingine Zitto yuko huko, kwamba yeye anazo sifa za kuanzisha na ku-maintain, wale walioko kwenye timu yake wana sifa au ya kuanzisha tu na wengine kuendeleza tu hawana zote mbili. Kwa hiyo hili linawapa shida sana wakishindwa kujua huyu mwenzetu yukoje.
 
Jambo lingine ni stahili ya vurugu ambayo wanayo wenzake, japokuwa naona hata yeye anaanza kuizoea japokuwa anaipitisha kwa hoja (fuatililia sakata la Gesi ya Mtwara).
 
Lakini jambo lingine huenda ni asili ya mtu mwenyewe alikotokea. Watu wansema Waha ni wabishi (Niko tayari kukosolewa), hawashindwi jambo, lakini  wana hulka au wanapenda kujaribu mambo mazito na makubwa, jambo hili nalo wengine wanadhani hii ni hulka tu ya watu wakubwa na kwa kufanya hivyo wanamuona kama bwana mdogo anakosa heshima kwa wakubwa na chama chake.
 
Ukichanganya mitizamo hii utaona kuwa inaweza wakati mwingine kuwa vigumu kuwa mshika mzuri wa timu yake ya sasa. lakini anakubalika katika jamii na hata wapiga kura wake pia.
 
K.E.M.S.
From: ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, 21 March 2013, 2:05
Subject: Fw: Re: [wanabidii] TATIZO LA ZITTO ZUBERI KABWE NI NINI ?

Ezekiel.
Nafikiri nimekuelewa na umeijadili mada yenyewe.
Naweza kukiri kutofautiana nawe kidogo. Team hutofautiana kufuatana na Task iliyo mbele yake.
Lakini timu tofauti zina maadili tofauti bila kujali kuwa mchezaji aweza kuwa katika timu mbalimbali. Muhimu ni yeye kuyasoma maadili ya timu kufuatana na malengo yake.
Nakumbuka kwa mbali kuna mchezaji wa Yanga aliwahi kutimuliwa kwa kukutwa amevaa jezi ya Simba. Kama nimekosea basi ni mtu kuvaa jezi ya simu hasimu.
 
Kuna malalamishi halali (kwa mfumo na mwenendo wa kisiasa tulio nao) kuwa Zito anakuwa karibu na mahasimu wa CHADEMA. Hata hapa jamvini humu Zitto hutetewa na wahasimu wa CHADEMA (Sina tabia ya kutaja ila kuna atakayetaja). Hii haionyeshi kuwa yeye yuko CHADEMA 100%. Infact kama si populality aliyojijengea kutokana na hoja ya Buzwagi huenda angeishaenguliwa.
 
Kwa hiyo uzuri wake akiutumia kwenda pinda na maadili ya Team work ndani ya chama chake anajikuta anapitia haya yaliyoletwa na YONA mmoja wa wale wanaoonekana kuijadili negatively CHADEMA hasa Dr Slaa (Yona usikasilike).
Kweli kama ulivyosema kuwa anasoma maoni haya, na kwa kuwa ana uwezo wa kuelewa tunachoandika na tunaachomaanisha basi lazima atafaidi mjadala huu na hasa wale wanapogusa mwiba ulipoingilia.
Elisa  --- On Wed, 3/20/13, ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk> wrote:

From: ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>
Subject: Re: [wanabidii] TATIZO LA ZITTO ZUBERI KABWE NI NINI ?
To: "wanabidii@googlegroups com" <wanabidii@googlegroups.com>, "elisamuhingo@yahoo.com" <elisamuhingo@yahoo.com>
Date: Wednesday, March 20, 2013, 1:48 AM

Muhingo nadhani umesema vizuri hapo hasa TEAM work spirit. Kimtizamo naona Zitto anaweza kufanya kazi na wengine, ukiona hata ambavyo amekuwa anashirikisha wabunge wenzake katika Kamati aliyopewa kuiongoza hapo nyuma mimi niliona aliwashirikisha vizuri.
Tatizo ninaloliona mimi wakati mwingine ni timu unayopewa kufunga nayo magori. Katika timu aliyomo haitaki uelwa wake, hasa tu pale alipotaja kuwania Urais basi timu ikaanza kumkataa. Hapa ni sawa na kusema kwenye mpira mchezaji wa nafasi ya ulinzi atafute kufunga goli halafuwachezaji wa mbele waanze kumlaumu na kisha waseme huyu hafai kabisa.
Hata hivyo kwa kuwa anasoma sana hapa jukwaani naamini taanza kuifanyia kazi. Lakini mh timu yenyewe anayotakiwa kufanya nayo kazi haimuhitaji huenda anakubalika na upande wa pili... ni mtizamo wangu tu kaka MUHINGO.
Sent from Yahoo! Mail on Android
From: ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>;
To: <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: Re: [wanabidii] TATIZO LA ZITTO ZUBERI KABWE NI NINI ?
Sent: Wed, Mar 20, 2013 2:53:41 AM
Mimi nionavyo Zitto ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kupambanua mambo, kujieleza nakadhalika.
Lakini naona kana kwamba ana tatizo la kufanya kazi katika TEAM.
 
Tusidhani wale wanaomweleza kama alivyolileta Yona ni wabaya wote. Sidhani.
Hebu tuliangalie hili kwa kuyachunguza yale wayasemayo wanaomuandika kama asemavyo Yona katika hoja ya msingi na tuuangalie mwenendo na matamshi ya Zitto. Tutaliona tatizo lake na huenda kama ni mtu anayepokea Feedback akafanya mabadiliko na kukifaa CHAMA chake na Taifa kwa ujumla.
Watu wenye akili na uwezo mkubwa wakati mwingine hukwama katika kufanya kazi kwenye team.
Si kazi ndogo kufanya kazi kwenye team. Mahala pengine unahitaji kuwasubiri wenzako na hii 'ikakuchelewesha'.
 
Hatwendi peke yetu katika kazi ya wengi. Katika Team pamoja na malengo ya kila mtu-tuna malengo ya Pamoja. Mfunga goli hutegemea walinzi na wengine. Mtu ukitaka kuanzoa mwanzo wa uwanja mpaka golini utafanya wote mfungwe. Hebu tuangaie huko na tunaweza kumsaidia kabwe kama ndiyo nia ya mleta mada.
 
Elisa Muhingo --- On Tue, 3/19/13, Tony PT <tony_uk45@yahoo.co.uk> wrote:

From: Tony PT <tony_uk45@yahoo.co.uk>
Subject: Re: [wanabidii] TATIZO LA ZITTO ZUBERI KABWE NI NINI ?
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tuesday, March 19, 2013, 10:38 AM

Kitila, Hili unasema ni kweli hasa ukichanganya na ushamba, umaskini, wivu, na kutojituma inazidisha chuki za akina sie! Ni balaa la kijamii!
Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Vodacom Tanzania.
From: Kitila Mkumbo <kitilam00@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tue, 19 Mar 2013 19:52:01 +0300
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] TATIZO LA ZITTO ZUBERI KABWE NI NINI ?
Ukitulia vizuri ukaangalia mbele na nyuma utaona kwamba katika jamii yetu tuna tabia ya kuchukia watu wenye uwezo, hasa wa kiakili. Tangu tukiwa mashuleni watu wanaonyesha uwezo mkubwa darasani na wanaofanya sana bidii huwa wanachukiwa na kutengwa. Hilo linaendelea hadi katika jamii na linajionyesha waziwazi pale ambapo huwa tunajikuta tunachagua viongozi bora viongozi na kuwaacha wale wanaoonekana wana uwezo. Mtu anayeonekana ana uwezo atapigwa vita kila kona hadi 'aishe' kisiasa. Ni nadra katika jamii yetu mtu mwenye uwezo sawasawa akapenye katika uongozi. Ndivyo alivyokwama SAS, na ndilo jambo analohangaika nalo ZZK na yeye amekuwa na ngozi nzito kwelikweli!!
2013/3/18 Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>
Ndugu zangu

Katika siku za karibuni tumeona vitisho , kashfa , dharau na aina
nyingine za dhihaka dhidi ya mwanasiasa kijana mhe zitto kabwe na hata
wakati mwingine unasoma kwenye mitandao ya kijamii safari zake binafsi
au mikutano binafsi ikichapishwa kwa maana ambayo sio sahihi .

Mpaka sasa hivi sijawahi kuelewa tatizo la Zitto Kabwe ni nini mpaka
anaandamwa ndani ya chama chake kwa siri siri na hata kwa uwazo tu
toka kwa baadhi ya viongozi na wanachama ambao ungetegemea wawe ndio
kichocheo ya maelewano ndani ya chama na nje .

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

-- Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. --- You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group. To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com. For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.    

0 comments:

Post a Comment