Wednesday 9 January 2013

[wanabidii] Wazanzibari wasema - " Ahsante Chadema"!

Default Wazanzibari wasema - " ahsante chadema"!

Dear All,
Wazanzibari wameishukuru CHADEMA kwa dhati kabisa kwa kumfunga na kumziba mdomo yule mwanachama wao anaeitwa Mzee Mwanakijiji ambae alikuwa akikebehi na kusema kuwa hauna mantiki yoyote Muungano wa Mkataba unaotaka serikali tatu.
Shukrani hizo zilitolewa jana baada ya Chadema kuwasilisha waraka wa maoni juu ya Katiba Mpya kuhusu Muungano - maoni ambayo ni sawa na yale ya Muungano wa Mkataba ambao Wazanzibari ndio wanaoutaka.
Tarehe 16 December, 2012 lile blogu la Wazanzibari lijulikanalo kama Zanzibar Ni Kwetu (ZNK) lilichapisha barua moja kutoka kwa Mzee Mwanakijiji ambayo ilibeza mantiki ya kuwepo kwa Muungano wa Mkataba ambao jana chama cha Mzee Mwanakijiji kiitwacho Chadema kiliupendekeza kwa kutaka Muungano wa Shirikisho kama ule wa European Union ambao ndio ulikuwa nyimbo na ngoma ya Wazanzibari siku zote hizi.
Katika barua hio, Mzee Mwanakijiji aliwasulubu Wazanzibari kwa kuandika kuwa..."hoja wanayoitoa ni ile ya kutaka Zanzibar kwanza, dola kamili, ikiwa na mamlaka yake yote. Hoja hii kwa Kiingereza inaweza kufupishwa kwa maneno mawili tu "FULL SOVEREIGNTY" yaani "HAKIMIYA KAMILI". 
Aliendelea Mzee Mwanakijiji..."Katika historia ya dunia jamii za watu zinapodai 'DOLA KAMILI' wakimaanisha dola yenye hakimiya kamili maanake ni kuwa jamii hizo zinatawaliwa na wengine....", aliandika Mzee Mwanakijiji.
"Chama cha Mzee Mwanakijiji (Chadema) jana kiliwasilisha mapendekezo kadhaa kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba; mojawapo ilikuwa ni kutaka kuwepo kwa Serikali ya Tanganyika, ambayo itakuwa HAKIMIYA KAMILI na MAMLAKA KAMILI ya Rais. Suala kwa Mzee Mwanakijiji ni hili: Chadema kutaka serikali yenye hakimiya kamili kwa Tanganyika, je, Tanganyika inatawaliwa na nani?". Aliuliza Mzanzibari mmoja alipokuwa akihojiwa na Wagagagigikoko, huku akiwa hana mbavu kwa kucheka kama vile Mzee Mwanakijiji alikuwa mbele yake.
" Mzee Mwanakijiji can now see the meaninglessness of his earlier assertions when he now refers to the official stand of his own party", aliendelea Mzanzibari huyo, huku akionywa kutotumia kimombo katika mahojiano hayo.
"Hayo hayo waliyoyatamka Chadema ndio ambayo tunayasema sisi Wazanzibari kila siku. Tukisema sisi tunafanyiwa nongwa na tunaelezwa tutoke na tutalipwa TSHS Bilioni 400, sasa leo Mzee Mwanakijiji atasema nini baada ya chama chake mwenyewe kuyatamka rasmi hayo hayo, tena hadharani? Atakiaga bye bye chama chake au vipi?". Aliendelea kuuliza Mzanzibari huyo.
"Strategy yetu Wazanzibari wote hivi sasa ni kukipigia kura Chadema katika 2015, kwasababu tunajua kuwa sisi na Chadema tunakuenda kwa pace moja." Alimalizia huyo jamaa.
Juhudi za kumtafuta Mzee Mwanakijiji kwa simu ili kumuuliza nini 'mantiki' ya mapendekezo ya Chadema au nini ilikuwa tofauti baina ya Muungano wa Mkataba na huu wa Shirikisho wanaoutaka Chadema hazikufanikiwa, kwani simu yake ilikuwa imezimwa. 
"Vyenginevyo, sisi Wazanzibari tutamsaka Mzee Mwanakijiji mpaka tumpate ana kwa ana ili atuombe radhi kutokana na barua zake za nyuma za kiburi alizokuwa akizitawanya kila pahala kuhusu juhudi zetu za kuigomboa nchi yetu", alimalizia msomaji mmoja wa Zanzibar Ni Kwetu.

Chanzo: Jamii Forums.

0 comments:

Post a Comment