Monday 28 January 2013

[wanabidii] UFAFANUZI WA TARATIBU ZILIZOFANYWA NA BAVICHA NA KUPELEKEA KUNIVUA UANACHAMA WA CHADEMA MIMI MTELA ALLAMU MWAMAPAMBA

CHAMACHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO

(CHADEMA)
Mtela Allamu Mwampamba

S.L.P 66

Mbeya

19-01/2013

KATIBU MKUU,
CHADEMAMAKAO MAKUU,
S.L.P.31191,
DAR.ES.SALAAM
Ndugu,
YAH: UFAFANUZI WA TARATIBU ZILIZOFANYWA NA BARAZA LA VIJANA(BAVICHA) NA KUPELEKEA KUNIVUA UANACHAMA WA CHADEMA MIMI MTELA ALLAMU MWAMAPAMBA.
Kichwa cha habarai cha husika,Mimi Mtela Allamu Mwampamba ambaye ni mwanachama wa CHADEMA. 
Nimesikia kwenye vyombo vya habari kwambani mevuliwa uanachama wa CHADEMA na kamati tendaji ya BAVICHA-TAIFA.
 Tar.8.10.2012 nilipokea barua kutokakamati ndogo iliyoundwa na kamati tendaji ya BAVICHA yenye kichwa cha habari nanukuu"YAH: WITO MAALUMU" yenye lengo la kubaini nini chanzo cha migogoro bainaya viongozi na wanachama.

Siku hiyo hiyo ya Tar.8/10/2012 nilikutana na wajumbewa kamati ndogo hiyo iliyoundwa na kamati tendaji BAVICHA tTaifa na tukafanya majadiliano ya kubaini nini chanzo cha migogoro baina ya viongozi na wanachamana tukakubaliana kwamba mahojiano yetu yatakuwa ni siri na ripoti yakeitawasilishwa katika kamati tendaji ya bavicha taifa pindi itakapo kutana.Mimi Mtela Mwampamba nilitoa ushirikiano sawia kwa kamati ndogo hiyo iliyoundwa na kamati tendaji ya BAVICHA.

Ta.28/12/2012 nilipokea barua kutokakwa katibu mkuu wa bBAVICHA taifa yenye kichwa cha habari nanukuu" YAH: MAELEZOYA KINA JUU YA SHUTUMA DHIDI YA BAADHI YA VIONGOZI WA BAVICHA NA WANACHAMA".Barua hiyo ilinitaka nitoe maelezo yangu juu ya tuhuma nilizozitoa mtandaoni napia ikanitaka nitoe maelezo na vielelezo ya ziada juu ya yale niliyoyasemakatika kamati ndogo ya kamati tendaji ya BAVICHA niliyofanya nayo mahojiano tarehe.08/10/2012 na nikaagizwa niyawasilishe BAVICHA Tar.31/12/2012 yawezekufanyiwa kazi.

Tar.31/12/2012 nilimuandikia barua katibu mkuu wa BAVICHA taifa juu ya masikitiko yangu ya barua aliyoniandikia kwamba nitoe vielelezo na maelezo ya ziada wakati kamati tendaji ya bavichabado haijapokea ripoti ya kamati ndogo iliyoundwa na kamati tendaji ya BAVICHA Taifa. Na ikumbukwe kwamba katibu mkuu wa BAVICHA hakuwa mjumbe wa kamati ndogoniliyofanya nayo mahojiano, Lakini cha ajabu katibu mkuu huyo wa BAVICHA alikuwa ameshapata ripoti na akanihukumu bila ripoti hiyo haijawasilishwa kwenye kamati tendaji ya BAVICHA.

Pia katibu mkuu BAVICHA taifa alinitaka nitoe maelezo na vielelezojuu ya tuhuma zinazohusu mimi kuwachafua baadhi ya viongozi na wanachama,Kwahiyo nilimtaka katika barua yangu,Katibu mkuu wa bavicha anitajie hao anaowaitabaadhi ya viongozi na tuhuma zinazonikabili. 

Tar.04/01/2013nilipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kwa jina la Daiel Naftal akinialikakwenye kikao cha kamati tendaji siku ya tar. 05/01/2013.Baada ya mwaliko huonilifika katika ukumbi wa mbezi garden kama mwaliko ulivyonitaka.
Siku hiyo ya Tar.05/01/2013 kikao cha kamati tendajikiliendelea na mimi nikatakiwa kukaa nje ya ukumbi wa kikao mpakanitakapoambiwa niingie.

Ilipofika saa 4 usiku nikaitwa niingie kwenyekikao,Niliitikia wito nikaingia kwenye kikao,Baada ya kuingia kwenye kikaoMwenyekiti wa 
BAVICHA bwana John heche alinitambulishwa kwa wajumbe na baada yautambulisho huo John Heche akanisomea mashitaka na katibu mkuu wa BAVICHA akanifafanulia mashitaka yangu.Cha kushangaza na kusikitisha tuhuma nilizosomewa na kutakiwakuzijibu sijawahi kuzisikia na kupewakwa maandishi kama mwongozo na taratibu za katiba ya chama unavyotaka kwa mwanachamaanayetuhumiwa.Nilipotakiwa kujibu tuhuma hizo,kwanza niliwaambia wajumbewakamati tendaji kwamba sina imani na mwenyekiti wa kikao Ndugu John Heche kwa sababu tuna conflict of interest za kisiasa.

Maana mimi na John heche tuligombea uenyekiti wa BAVICHA mwaka 2011 na mimi nilienguliwa ili Heche apite kirahisi.Kwa maana hiyo hawezi kunitendea haki kwenye kikao hicho. Pianiliwambia wajumbe wa kamati tendaji kwamba sina imani na katibu wa BAVICHA TAIFA kwa sababu alishaniandikia barua ya kunihukumu hata kabla ya ripoti yakamati ndogo haijawasilishwa mbele yakamati tendaji.

Baada ya hoja yangu hiyo kwa wajumbe ndipo yalipozuka malumbano makubwa dhidi ya hoja yangu kutokuwa na imani na mwenyekiti na katibu. Katikahali ya kusikitisha ndipo Ndugu Jonh Heche alipoamuru mabaunsa watatu waliokuwepo ndani ya kikao wanikamate na wanitoe nje ya kikao, Mabaunsa hao wakanikamatana kunitoa nje ya kikao kama walivyoagizwa na bosi wao Ndugu John Heche.

Tar.06/01/2013 nikaanza kupata taarifa kwamba nimefukuzwa uanachama wa CHADEMA, taarifa hizo nilizisoma kupitia mitandao ya kijamii kama facebook na JamiifForums na baadae nikaanza kusikia na kusoma kwenye vyombo vyahabari(televisheni na magazeti) kwamba nimefukuzwa uanachama wa BAVICHA nachama kwa ujumla.

Ninafahamu kwamba kukoma kwa uwanachama ibara ya 5.4.6 nikufukuzwa uanachama na baraza la vijana,wanawake au wazee kwa utovu wanidhamu.Kutokana na kifungu hiki ninakuja kwako katibu mkuu wa CHADEMA-TAIFA kuomba ufafanuzi wa utaratibu wawanachama kufukuzwa uanachama katika katiba ya chadema na mwongozo wake.Katiba ya chadema ibara ya 6.5.2 kwa mujibu wa ibara ya 5.4.3na 5.4.4 ya katiba ya chama inasema.mwanachama yeyote hatachukuliwa hatua zakinidhamu ama kuonywa amakuachishwa ama kufukuzwa uanachama bila kwanza.

a) Kujulishwamakosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wikimbili.

b) Kupewanafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika

c) Mwaachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki mbili baada yakusikilizwa.Pia katiba ya chama:
Haki za mwanachama ibara ya 5.2.4kujitetea,kusikilizwa na kukata rufaa anaposhitakiwa ama kuchukuliwa hatua zakinidhamu kichama.

Kwa hiyo naomba ofisi ya katibu mkuu iweze kunipa ufafanuziwa taratibu za bavicha kunivua uanachama maana mwongozo wa mabaraza hauoneshitaratibu za kumvua uanachama.Na kwa sababu mwongozo wa mabaraza hauoneshiutaratibu wa kufuata ilimwanachama avuliwe uanachama kwa hiyo naomba ufafanuziwa katiba ya chadema.

Nimeambatanisha na barua nilizowahi patiwa na kamatindogo,barua ya katibu BAVICHAna majibu yangu na pia naambatanisha na maelezoya Ndugu John Heche dhidi ya tuhuma zangu kwa vyombo vya habari.Wako kakita mapambano dhidi yadhuluma,chuki,fitina na udhalilishaji wa utu na demokrasia

………………………………………………..

MTELA ALLAMU MWAMPAMBA

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group, send email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment