Thursday 10 January 2013

[wanabidii] UDHAIFU WA CHADEMA/CUF UTALETA MGAWANYIKO NCHINI

Ndugu zangu

Siku moja baba wa taifa aliwahi kuonya kuhusu chama kinachotaka
kuongoza nchi kwa kutamka hadharani kwamba vyama vya kikanda , dini ,
kabila au upande fulani wa muungano havitakiwi na haviwezi kuongoza
nchi hii .

Aliposema hivi hakugusia ni chama gani au vyama kwangu mimi naona kwa
wakati huu ni CHADEMA na CUF ambapo CUF inanguvu sana visiwani wakati
CHADEMA imeanza kuwa na nguvu katika baadhi ya maeneo ya nchi lakini
sio visiwani kwa sana .

Matokeo yake ni kwa viongozi wa vyama hivi kwa nyakati tofauti kutoa
matamshi ya kutaka kuwa na muungano wa mkataba au serikali tatu
kutokana na vyama hivi kutokuwa na wafuasi waliosambaa nchi nzima .

Nawashauri waendeleze harakati za kujenga vyama vyao maeneo yote ya
nchi na sio baadhi ya maeneo na kuleta visingizio vya serikali tatu au
muungano wa mkataba kwa maslahi yao ya kisiasa .

Udhaifu wao usiwe kisingizio cha kuwagawa watanzania .

Tukileta utengano katiak nchi hii hakuna atakayebaki , wale wanaotaka
nchi kutengana kwa sababu zozote zile wao waanze kujikata vipande
sehemu za miili yao.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment