Saturday 12 January 2013

[wanabidii] SERIKALI YA TANZANIA YABABAISHA BWEGE KUHUSU KUCHUNGUZA PESA ZILIZOFICHWA SWITZERLAND!


SERIKALI ya Uswisi imesema Serikali Tanzania haijaonyesha nia ya dhati kutaka kuchunguza na kupata mabilioni ya fedha yaliyofichwa na Watanzania katika benki mbalimbali nchini humo.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi Jumamosi, jijini Dar es Salaam jana, Balozi wa Uswisi nchini, Olivier Chave alisema mpaka sasa hakuna jitihada zozote zilizofanywa na Serikali ya Tanzania kutaka ufumbuzi wa tuhuma hizo.
Balozi Chave alisema hayo muda mfupi baada ya kumaliza mazungumzo yake ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe. Hata hivyo wote wawili hawakuwa tayari kueleza ni kipi kilichojiri katika mazungumzo yao.
Katika kikao cha tisa cha Bunge, Novemba mwaka jana, Zitto aliwasilisha hoja binafsi kulitaka Bunge kuchunguza na kuielekeza Serikali kuchukua hatua dhidi ya Watanzania walioficha fedha na mali haramu nje ya nchi.
Katika mazungumzo yake jana, Chave alisema: "Uswisi iko tayari kushirikiana na Tanzania kujua uhalali wa fedha hizo na endapo zikigundulika ni fedha chafu basi tutazirejesha nchini." Aliongeza:
"Serikali ya Uswisi haina tatizo kwani tumeshafanya hivyo kwa nchi za Ufilipino na Nigeria hivyo tutafurahi na Tanzania kama tutamaliza suala hili". Alisema habari zinazoandikwa kuhusu mabilioni hayo kuhifadhiwa katika Benki za Uswisi, zinaharibu picha ya nchi hiyo mbele ya mataifa mengine, hivyo angependa suala hilo kumalizwa na kwamba wao wako tayari kusaidia.
Chanzo: Mananchi


N.B.
Huyu Balozi awe very careful sio hasha akapewa 24 hours ahame nchi. Yeye aliona wapi mwizi akajichunguza mwenyewe?
Kama ni hivyo tungelimrejesha yule Mhindi wa pesa za Radar aliejificha huko Switzerland.
Mzee Vijisenti mwenyewe kakubali kama vipo vijsenti nje na wala hakuulizwa kitu, vipi leo patakuwepo nia safi ya kuchunguza hizo pesa zilizofichwa?
Anyway, tumuombe Mungu huu Muungano ubakie hivi hivi, else Zanzibar ikipata mamlaka kamili, basi tutazivalia njuga hizi pesa na senti moja haitoletwa Bara, kwasababu Bara hamzitaki!

...bin Issa





0 comments:

Post a Comment