Tuesday 22 January 2013

[wanabidii] Re: MAONI YA MH BENJAMIN MKAPA KUHUSU GESI YA MTWARA

On Jan 22, 4:11 pm, Selemani Rehani <sreh...@hotmail.com> wrote:
> Watazungumza sana lakini kiini cha yote haya ni mambo yafuatayo:
>
> 1. Serikali hii imepoteza imani kwa wananchi. Haiaminiki tena. Wamepoteza trust na credibility. Kwa nini? huo ni mjadala unaojitegemea.
>
> 2. Serikali imepoteza uhalali wa kutawala
>
> 3. Imeshindwa kuongoza, kuonyesha njia na kuwapa tumaini wananchi
>
> 4. Kuna ombwe la uongozi na hivyo wananchi hawana tumaini na tumepoteza muelekeo na dira
>
> 5. Vitendo vya ufisadi vimekithiri na kuwafanya wananchi wasiiamni tena serikali yao kusimamia raslimali zao
>
> 6. Makosa makubwa yaliyofanywa katika matumizi ya raslimali nyingine kama vile madini, wanyama etc, yamewafanya wana Mtwara kupoteza imani kabisa na Serikali.
>
> 7. Tabia ya serikali kuwakumbatia 'wageni au wawekezaji' na kuwasahau wazawa imepelekea kuwafanya wananchi wa mtwara kupoteza imani.
>
> 8. Mikataba mibovu, isiyokuwa na tija iliyoisainiwa na serikali katika sekta ya madini
>
> 9. Majibu ya jeuri kutoka kwa Mawaziri, Rais na Serikali yote kwa ujumla
>
> 8. Nini cha kufanya? ni kushughulikia hayo? je Serikali hii inaweza kurudisha imani kwa wananchi, sijui, labda wakitoka madarakani na wakapewa nafasi ya kujipanga upya. Kwani sasa bado wananyukana katika makundi ya kugombania Urais.
>
> Selemani Rehani
>
> Date: Tue, 22 Jan 2013 15:26:45 +0300
> Subject: [Mabadiliko] TAMKO LA NDUGU BENJAMIN WILLIAM MKAPA
> From: fkatula...@gmail.com
> To: mabadilikotanzania@googlegroups.com
>
> Katika wiki za hapa karibuni kumekuwa na mijadala na mazungumzo mengi kuhusu mikakati ya maendeleo ya mikoa ya Kusini hususan Mkoa wa Mtwara.  Mazungumzo hayo yamekuwa na lugha kali na yameambatana, hatimaye, na maandamano na mikutano ya hadhara.  Kiini chake ni matumizi ya gesi iliyogunduliwa mkoani kwa ajili ya miradi au mipango ya maendeleo ya mkoa huo, mipango iliyopo mbioni kutekelezwa au inayotarajia kutekelezwa.  Mwenendo wa mazungumzo, maandamano na mikutano ya hadhara imeelekea kuashiria shari na kuvunjika kwa amani.
>
> Aidha vituko na kauli hizo zimekaribia kujenga kutokuelewana kati ya Viongozi wa Vyama vya Siasa na Serikali, kati ya wanachama wa vyama vya siasa na viongozi wao, kati ya wananchi na viongozi wa Serikali.  Mtafaruku huu haufai kuachwa uendeleee na kutishia usalama.  Mipango ya maendeleo siyo Siri.  Mikakati na mbinu za Utekelezaji wake siyo Siri.  Maelezo yake mazuri yanaweza kutolewa yakadhihirisha namna na kasi ambayo raslimali zitawanufaisha wananchi wa eneo zilizomo na Taifa zima.  Utekelezaji wa miradi unategemea masharti kadhaa, k.m. Uwapo wa mitaji na teknolojia.  Lakini pia mwekezaji, awe Serikali au Sekta binafsi, atataka iwepo hali ya utulivu na usalama wa watu, hali na mali.  Hayo yatadaiwa na wawekezaji wa ndani na wa nje.  Vurugu, fujo, vitisho havivutii uwekezaji.
>
> Nikiwa Mwana Mtwara na raia mwema mpenda nchi, nimefadhaishwa sana na matukio haya ya siku za karibuni Mtwara.  Kwa sababu hiyo natoa wito kwa wadau wote wa maendeleo ya Mtwara kusitisha harakati hizi na maandamano na mihadhara na badala yake wajipange KUKAA PAMOJA katika meza moja, kupitia historia, kutathmini mipango, kuchambua kwa kina mikakati ya utekelezaji wake, na hatimaye kufikia muafaka wa Ujia wa maendeleo. Fujo, vitisho, kupimana nguvu na malumbano kamwe si masharti ya maendeleo.  Mazungumzo yataboresha sera, ya uwekezaji ya mkoa na nchi.
>
> Linalowezekana leo lisingoje kesho.
>
> Benjamin William Mkapa
>
> Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
> --
> 'Walk The Talk'
> Frederick M. Katulanda
> Cell: +255 784 642620,
> Alternative:+255 754 642620
> E-mail: fkatula...@yahoo.com
>
> --
> Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
> Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
> Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
>
> TEMBELEA Facebook yetu:http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
>
> For more options, visit this group at:http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
>
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
> To unsubscribe from this group, send email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment