Tuesday 8 January 2013

[wanabidii] Re: Maoni ya kupunguza uchafuzi wa mazingira kwa SUMATRA

 
Miji yetu na barabara zetu zinazidi kukithiri kwa uchafu. Pamoja na sababu nyingine wasafiri na wamiliki wa vyombo vya usafiri (mabasi, boti) wanachangia katika utupaji wa taka za kila aina nje. Wasafiri hawana mwamko au uelewa ya kuwa utupaji taka hizi na ni chanzo cha uchafuzi wa mazingira na uharibifu wa miundombinu. Wamiliki na wasimamizi wa vyombo vya usafiri hawajaelemika na kuweka mazingira ya kuwezesha wasafari kutotupa taka nje ya magari. Katika mabasi mengi (ya huduma za mjini kama vile daladala, na hata mabasi yaendayo safari nje ya miji mikubwa) hakuna vyombo vya kuwekea taka, wala tangazo la kuwataka abiria kutotupa taka nje. Ushahidi uko wazi unafika sehemu mabasi ya mikoani yanaposimama kwa ajili ya abiria kula chakula, ambapo takribani kilomita moja kabla na baada ya vituo hivyo, utaona jinsi taka (plastics na vibebeo vingine vya vyakula)vilivyozagaa mithili ya mapambo! (Mombo na Korogwe, Aljaziira na-njia ya Iringa/Mbeya, nk.
Natambua SUMTRA ilikwishaweka taratibu za kuzuia uchafu huu kwa kuwataka wamiliki kuwa n vyombo vya kuweka taka ndani ya mabasi, lakini inaonekana ilikuwa nguvu ya muda mfupi tu. Kumetokea nini? Nani alitakiwa kuhakikisha kuwa zoezi hili linasimamiwa vyema? Hali ni mbaya na ya kutia aibu.
Nina mapendekezo machache kwa sumatra na wadau wengine:
1. Weka masharti kwenye leseni ya kutaka kila chombo cha usafiri wa abiria kote nchini kuwa na sehemu ya kuhifadhi taka. Hii ni pamoja na kuwataka wamiliki kuweka maandishi yanayowakumbusha abiria kutotupa taka nje ya chombo cha usafiri. SUMATRA kwa kushirikiana na mamlaka zingine iweke mkakati wa kukagua (spot check) kama sharti hili linazingatiwa na hatua zichukuliwe kwa wanaokiuka.
2. Tutangaze kuwa "UCHAFU NI NOMA" Elimu kwa raia itolewe kwa kupitia vyombo vya habari na mitandao mingine. Hapa Asasi za kiraia (NGOs) zinaweza kusaidia kugharamia sehemu ya elimu na matangazo haya.
3. Wamiiliki wa vyombo vinavyopitia katika njia zilizo kwisha athirika (Dar-Morogoro, Arusha, Tanda, Mbeya Iringa nk) watoe ushirikiano wa kusafisha sehemu zilizokithiri kwa uchafu ili kuondoa aibu hii.
4. Watu waanotoa huduma ya vyakula na vinywaji katika njia kuu waagizwe kutumia vifungashio vinavyo haribika (digestible materials) ili kuokoa uharibu unaoendela.
Natumaini maoni haya yatazingatiwa na kuwa chachu ya kuchukua hatua. Na pia mtaweza kunipa mtejesho wa haraka
Wenu mpenda nchi safi
 
Makongo
----------------------------------------------------------------
Japhet Maingu Makongo
Director, Ubunifu Associates Ltd
P.O. Box 32971, Dar es Salaam,
TANZANIA
Website: www.ubunifu.co.tz, info@ubunifu.co.tz,
Tel: +255 22 2762027, Mobile:+255 754 571 256

0 comments:

Post a Comment