Tuesday 22 January 2013

[wanabidii] MAFUNZO KWETU WADADA TENA WALE WANAOSEMA WA KISASA

Nilipoingia katika mahusiano naye nilimuamini, nikampa kila kitu
nilichoweza. Nakumbuka enzi zile nyumbani tulikuwa tuna ng'ombe,
niliiba maziwa kila siku na kumpelekea kwao. Akanenepa!! Penzi letu
likawa huru alipoanza maisha yake mwenyewe. Sikuwa najua lolote kuhusu
mapenzi. Alinifundisha. Nikaegemeza maisha yangu yote kwake.
Akanifanya nikawa mtumwa wa ngono kila nikienda chumbani kwake. Kama
haikutosha sasa akaanza kunifundisha kunywa pombe. Niliamini kuwa
ndiye mume wangu mtarajiwa, kwa nini nikatae?

Nilimkubalia kila kitu. Alinilazimisha ngono hata nilipokuwa katika
siku zangu. Kweli nilikuwa msomi na niliyajua madhara ya kufanya hivyo
lakini sikutaka kumuudhi huyo niliyeamini kuwa ni mume wangu.
Nilipenda tututmie kinga lakini aliipinga sana. Nikapata mimba ya
kwanza!! Hakuwa na pesa lakini alinilazimisha niitoe.

Nikaiba pesa nyumbani nikafanya alivyotaka. Kwa mara ya kwanza
nikatyoa mimba. Haikuniuma sana!! Niliamini kuwa ni yeye atakuja
kunioa na atanifichia aibu hii. Nilitegemea sasa tutaanza kutumia
kinga. Lakini hapana haikuwa hivyo.

Aliendelea kunilaghai. Tayari aliujua udhaifu wangu. Alinishika hapa
na pale. Nikishtuka tayari amefanya anavyojua. Pombe kidogo na
nyingine kidogo. Nikazoea lakini nikawa nawahi kulewa. Akautumia
udhaifu huu kunifanyia jambo baya lililonifanya niandike haya kwako.
Akaniingilia kinyume na maumbile. Alinilawiti!!

Nilishindwa kumshtaki popote. Nikavumilia kwa kuwa alikuwa mume wangu
mtarajiwa. Mume asiyejulikana hata kwa wazazi. Mchezo ule ukaendelea.
Akajitetea eti hataki nipate mimba tena, hivyo hiyo ni mbinu mbadala.
Najuta kumuamini!! Lakini huyo alikuwa mume wangu.

Miaka ikapita, ule urembo wangu niliozoea kuuona katika kioo
ukatoweka, simu za mara kwa mara kutoka kwake zikatoweka, akawa mkali
sana kwangu. Hakutaka niende kwake. Wakati huo nilikuwa nasoma chuo.
Pesa ya mkopo ikitoka ananitafuta na tunakuwa marafiki tena.

Anasema ananipenda na atanioa. Ananilewesha na kunitumia kinyume na
maumbile. Pesa ikiisha na mapenzi yanaisha nabaki mwenyewe katika
msoto. Sasa akaanza kubadilisha wasichana waziwazi. Ningesema nini
mimi? Ninajua alishindwa kusema neno moja tu. Tuachane!!

Nilijua tayari ameniacha!!! Afya yangu ikadolola sana, nikalazimika
kwenda kupima hospitali. Sikuwa na virusi. Nikapewa ushauri
nikautumia. Siku zikasonga nikampata mwanaume mwingine. Huyu alikuwa
ananijali sana. Nikaanza kumsahau yule aliyenitenda. Nilipomaliza chuo
akajitambulisha nyumbani na alitaka kunioa. Akanio kweli. Maisha
yakaanza.

Mwaka wa kwanza, mwaka wa pili na hadi wa tatu. Sikuwa nabeba mimba.
Mume wangu alikuwa mvumilivu sana, hakuwa hi kunilaumu. Lakini
niliumizwa na mawifi. Nikaamua kwenda hospitali. Nikaambiwa kizazi
change kiliharibiwa kwa kutoa mimba mara kwa mara.

Pia mapenzi ya kinyume na maumbile yamenivuruga kabisa. Nililia sana
huku nikimkumbuka yule aliyeuleta uchungu huu kwangu. Dunia haikuwa
mahali pangu sahihi. Nimekuandikia barua hii mdogo wangu.

Uisome mwenyewe!! Lakini uwasimulie wengi baada ya kifo changu.
Uwasimulie bila kuchoka wasichana wa kileo wanaodanganyika na kufanya
mambo magumu kuwaridhisha wapenzi wao. Waambie watakufa kwa mateso
kama mimi.

Wasipokusikiliza usijisikie vibaya maana hata mimi nilikuwa
siwasikilizi watu waliponambia lolote kuhusu yule mume mdanganyifu.
Sitajiua lakini nitakufa kabla ya wakati!!! Nimekuandikia wewe kwa
kuwa u mwandishi. Japo kwa sasa u mtoto mdogo najua utaipata nafasi
siku moja ya kuwafikishia wasichana hawa.

Usilie kwa sababu nitakufa. Lia kwasababu mwanaume mwenzako AMENITENDA
HIVI!!! TAFADHARI TAFAKARI

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment