Tuesday 29 January 2013

[wanabidii] Kwa nini serikali tatu?

Wanabidii,
 
Nanukuu kauli moja ya mwenyekiti wa CHADEMA katika kikao cha Kamati Kuu (CC) juzi ambapo agenda moja kubwa ilikuwa ni kupitisha mpango mkakati wa mwaka 2013 ili kushinda chaguzi zote kuanzia serikali za vitongoji, vijiji na mitaa mwaka 2014 na Uchaguzi Mkuu 2015.

 
Katika suala zima la Muungano, Mbowe alisema uwepo wa serikali tatu hauepukiki kwa kuwa tayari Tanzania Visiwani wameshakuwa na serikali yao hivyo ni jukumu la Watanzania Bara kupata serikali ya Tanganyika na kisha kuwepo na serikali ndogo ya Muungano. Alisema serikali tatu inawezekana ikiwa viongozi wataacha unafiki wa kusema muungano utavunjika huku tayari wakitoa uhuru wa Zanzibar kuwa na Rais, bendera na wimbo wao ya taifa. Tunawaunga mkono wenzetu Wazanzibar katika kupigania uhuru kamili na kwa sasa sisi ndio tunaoonekana wa ajabu kushindwa kuuliza serikali ya Tanganyika," alisema.
Swali;
Je kuna sababu za msingi ambazo CHADEMA wanazo mpaka kufikia hatua ya kuzitaka serikali tatu tofauti na ilivyo hivi sasa?

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment