Thursday 10 January 2013

[wanabidii] Hoja ya JK kuhusu ubunge wa Kafumu yaibua mapya - Mwanzo

KITENDO cha Rais Jakaya Kikwete kuhoji hukumu iliyomwengua Dk Dalaly Peter Kafumu kuwa Mbunge wa Igunga, kimewakera baadhi ya wanasheria nchini ambao wameeleza kuwa hatua hiyo ni kuingilia uhuru wa mhimili mwingine wa dola. Akizindua Daraja la Mbutu mkoani Tabora, Januari 7, mwaka huu, Rais Kikwete pamoja na mambo mengine, alihoji uamuzi uliomwengua katika nafasi ya ubunge Dk Kafumu kwa kigezo cha kufanya kampeni kwa kutumia ujenzi wa daraja hilo.

 
Rais Kikwete alihoji mantiki ya uamuzi huo wakati ujenzi wa daraja hilo ni moja ya mambo yaliyopo kwenye Ilani ya CCM ya 2010 – 2015.
"Mwaka 2010 katika Uchaguzi Mkuu nilifika hapa kumnadi aliyekuwa mbunge wa jimbo hili, Rostam Aziz na ujenzi wa Daraja la Mbutu ni moja ya mambo yaliyopo kwenye ilani yetu," alisema Rais Kikwete na kuongeza:
"Katika uchaguzi mdogo baada ya kujiuzulu Rostam, CCM iliendelea kunadi ilani yake ya kujenga daraja hilo kwa kuwa lilikuwa halijakamilika baada ya mbunge wake kujiondoa."
Akizungumzia kauli hiyo, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Law Society (TLS), Francis Stola alisema hukumu hiyo ilikuwa sahihi kwani ni makosa kwa kiongozi wa Serikali kutumia jukwaa la kampeni za kisiasa kuzungumzia masuala yanayohusu utendaji wa Serikali akisema kufanya hivyo kunaweza kutoa ushawishi kwa wapigakura na kuvuruga mwenendo wa uchaguzi.
http://wotepamoja.com/archives/11055#.UO6YIrF4rIA.gmail

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment