Sunday 6 January 2013

Re: [wanabidii] UFAFANUZI KUHUSU MIRADI YA UTAFUTAJI NA UVUNAJI WA GESI ASILIA NCHINI

Wanabidii,
 
Heri ya mwaka mpya. Angarau hoja hii ya gesi ya Mtwara inaanza kurejesha jukwaa katika uhai wake baada ya kupumzika katika sikuu za mwisho wa mwaka na kuanza mwaka mpya.
 
Mimi nionavyo maelezo ya Waziri kuwa kutakuwa na matoleo yatakazowekwa kwa ajili ya matumizi ya watu wa Mtwara na Lindi yanajitosheleza. Kama mtu atadai zaidi ya hapo analo jambo na nafikiri tusimkubalie mtu huyo kwa kuwa atatugawa.
 
Hoja ya wanasiasa kuelekeza nguvu zao huo ni sawa kwa kuwa hawakuwahi kuungwa mkono huko kusini kwa hiyo wanatafuta kila njia ili waweze kuungwa mkono. jambo la msingi hapa je kwa mkakati huu wa kuwagawa watanzania unakubalika. Kwa upande wangu haukubaliki, labda watafute njia nyingine.
 
Kahawa ya Bukoba na Kilimanjaro imesomesha watanzania wote je na wao waanze kudai kwamba iliwanufaishaje. Wenye Almasi je nao wasemeje. nafikiri tuache ushabiki katika hili mali za watanzania ni zetu wote.
 
KEMS.
 
Kunyaranyara, E.M.S.
From: jbifabusha <jbifabusha@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Friday, 4 January 2013, 21:05
Subject: Re: [wanabidii] UFAFANUZI KUHUSU MIRADI YA UTAFUTAJI NA UVUNAJI WA GESI ASILIA NCHINI
Denis,
Kwa hiyo twende Nigeria, Kuwait na nchi zingine tuweke mabomba tuvute mafuta kwasababu hakuna aliye yaweka. Watu wa Mtwara wana haki ya kunufaika na maliasili iliyomo kwenye eneo lao sawa na maliasili ya maeneo mengine. Mimi naona lazima serikali iwe na mipango ya kuwanifaisha watu wa maeneo ambako mali asili inazalishwa ndiyo maana halisi ya social corporate responsibilty.


Send from Samsung Mobile
denis Matanda <denis.matanda@gmail.com> wrote:
Watu wa Mtwara wamefanya nini kuweka gesi ile pale? Mimi kwa mtizamo wangu ni kuwa watu hawana haki ya kudai kitu ambacho hawajachangia chochote kukiweka au kukitengeneza. Ni coincidence tu ya kijiografia!
On Jan 5, 2013 12:20 AM, "ELISA MUHINGO" <elisamuhingo@yahoo.com> wrote:
Maelezo mazuri ya waziri yanayojitosheleza na kuungwa mkono na Bart na wengine hakujaondoa hoja ya wanaMtwara ya kutaka kufaidika na raslimali zetu sawia. Hakujaondoa dai la wengi la kutaka mgawanyo mzuri wa raslimali zetu.
 
Kwanza ni haki kujua kama kahawa, pamba na kadhalika mapato yetu yamegawanywa sawa kwa watanzania wote.
 
Yaani Barabara zimejengwa sawa, Hospitali na usambazaji madawa umegawiwa sawa nchi nzima, Shule nzuri zimejengwa sawa vijijini yanakolimwa mazao hayo sawa na mijini.
 
Waziri asipojielekeza huko na kukiri kosa atachochea mengine.
Ukisema mapato ya taifa yamegawiwa sawa Kigoma kama Dares salaam unawakasirisha waha nk. Na unayesema hivyo ndiye unayevunja Taifa, Mikoa, Wilaya, Tarafa, Kata na vijiji vyetu.
 
Ipo haja ya kusikiliza wananchi wanasema nini bila kukurupuka kutamka na kupongezana kwa yaliyotamkwa.
--- On Fri, 1/4/13, Bart Mkinga <bmkinga@yahoo.com> wrote:

From: Bart Mkinga <bmkinga@yahoo.com>
Subject: Re: [wanabidii] UFAFANUZI KUHUSU MIRADI YA UTAFUTAJI NA UVUNAJI WA GESI ASILIA NCHINI
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>, "Wanazuoni" <wanazuoni@yahoogroups.com>, "wanataaluma@googlegroups.com" <wanataaluma@googlegroups.com>
Date: Friday, January 4, 2013, 2:03 AM

Katika hili, naungana na serikali.
 
Hapa kuna sababu za kiuchumu, hizi ni lazima ziheshimiwe kuliko kuegemea sababu za kisiasa katika kila jambo. Sielewi busara ya viongozi wa kisiasa na wale wengine wote wanaounga mkono matakwa ya watu wanaotaka gesi isisafirishwe kwenda Dar es Salaam eti tu kwa vile gesi hiyo inapatikana Mtwara kwa hiyo kila kitu kinachohusiana na gesi ni lazima kiwe Mtwara.
 
Sababu za kiuchumi zipo wazi kama ambavyo Waziri Professor Muhongo alifafanua:
 
§  Miundombinu ya ufuaji na usafirishaji wa umeme wa gesi tayari ipo Dar es Salaam, kweli kuna sababu ya kuanza kujenga mitambo mipya na miundombinu mipya ya usafirishaji umeme kutokea Mtwara? Kwa faida ipi itakayoongezeka kwa wana-Mtwara, TPDC, TANESCO, makampuni ya gesi na Taifa kwa ujumla?
 
§  Moja ya matumizi ya gesi hii itakuwa kupeleka gesi kwenye viwanda ambavyo vinaweza kuzalisha umeme wao wenyewe kwa matumizi ya viwanda hivyo. Zaidi ya asilimia 80 ya viwanda vyote vya Tanzania vipo Dar es Salaam, wanaotaka gesi isisafirishwe kwa bomba kwenda Dar es Salaam, wanataka isafirishwe kwa malori kwenda Dar? Maana gesi haitatumika kwaajili ya kuzalishia umeme wa gridi pekee.
 
§  Gesi hii itatumika pia kama nishati ya kuendeshea magari. Aasilimia kubwa ya magari yapo Dar es Salaam. Usafirishaji wa gesi kwa njia ya bomba utakuwa na unafuu wa gharama kuliko kama ikisafirishwa kwa malori mpaka Dar es Salaama
 
§  Lakini pia tufahamu kuwa gesi hii itasafirishwa kwenda mikoa mbalimbali kwa matumizi kama yale ya kuendeshea magari na mitambo ya viwandani, ukitaka kupeleka gesi Bukoba, Mbeya, Arusha, Dodoma, Mwanza, n.k. ni rahisi kusafirisha kutokea wapi, Dar es Salaam au Mtwara?
 
§  Tukitaka kuwa wakweli wa nafsi zetu, kujenga mtambo wa kufulia umeme Mtwara kutaongeza kitu gani cha pekee kwa uchumi wa mkoa wa Mtwara au ajira ya watu wa Mtwara? Mimi nimefika pale Mtera, panazalisha umeme wa maji, Je, ni nini kilichoongezeka kiuchumi kwa mkoa wa Dodoma/Iringa? Ule mtambo upo kwa zaidi ya miaka 15, Mtera haijawa mji na haijawa na chochote cha pekee ukilinganisha na vijiji vingine
 
Lakini kuna jambo jingine ambalo ni muhimu sana kulitambua na kulitafakari. Hivi ni sahihi kufikiria kuwa Watanzania waishio maeneo yenye madini au gesi wana haki zaidi ya kufaidika na mapato yatokanayo na rasilimali asilia hiyo kuliko Watanzania wa maeneo mengine?
 
Leo hii kama tungefanya sensa ya watanzania wote na kuona mchango wa mapato ya serikali yamekuwa yakichangiwa zaidi na watu wa mkoa gani na wilaya gani, huenda mikoa hii ambayo leo ina dhahabu au gesi inaweza kuonekana kwa miaka mingi imetegemezwa na mikoa mingine.
 
Hivi ni halali kwa mfano kusema kuwa mkoa fulani una madaktari wengi kuliko mikoa mingine, na hivyo hospitali za mkoa huo zina haki ya kuwa na madaktari wa kutosha wakati hospitali nyingine katika mikoa mingine hazina madaktari kabisa? Hivi ni halali leo hii kusema kuwa kwa kuwa mikoa fulani ina hifadhi za wanyama, ni lazima hoteli za kitalii zijengwe katika mikoa hiyo tu kwa vile watalii wanakuja nchini Tanzania kuangalia wanyama waliopo katika mikoa yao?
 
Rasimali kubwa katika ujenzi wa Taifa lolote ni watu, na rasilimali hii ipo mikoa yote ya Tanzania, na inachangia maendeleo ya nchi hii kwa viwango tofauti tofauti na kwa namna tofauti tofauti kwa manufaa ya watu wote hata wale wasiochangia chochote. Kama kinachochangiwa na rasilimali hii kuu ya watu hakigawanywi kwa upendeleo wa maeneo, kwa nini rasimali asilia ambayo ni ndogo kuliko rasimali kuu ya watu, iwe na upendeleo maalum kwa kutegemea eneo ilipo?
 
Watanzania tuache ubinafsi, tuache uchoyo, rasimali asilia zetu zisaidie kutuunganisha kuliko kututenganisha kwa namna yeyote ile. Tokea uhuru wa nchi hii michango ya mikoa mbalimbali katika uchumi wa Tanzania imekuwa kwa viwango tofauti tofauti lakini mgawanyo wake haujawahi kuzingatia viwango vya michango ya kila mkoa. Kwa nini leo hii tufikirie kuwa mkoa wenye gesi asilia una haki zaidi kuhusiana na faida za gesi kuliko mikoa mingine? Au Watanzania hao wanataka na ile mikoa iliyoitegemeza mikoa mingine kwa miaka mingi nayo iwadai fidia? Tukifikia hapo hatutakuwa na Taifa moja. Tuache fikra na mioyo ya ubinafsi, ni mioyo ya namna hiyo ndiyo iliyopalilia baadhi ya viongozi wetu na watendaji kuwa wala rushwa, wabadhirifu na mafisadi – kutaka mimi nifaidi zaidi kuliko wengine.
Bart
 
From: Yona Maro <oldmoshi@gmail.com>
To: Wanazuoni <wanazuoni@yahoogroups.com>; wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>; wanataaluma@googlegroups.com
Sent: Wednesday, January 2, 2013 9:26 PM
Subject: [wanabidii] UFAFANUZI KUHUSU MIRADI YA UTAFUTAJI NA UVUNAJI WA GESI ASILIA NCHINI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUFAFANUA KUHUSU MIRADI YA UTAFUTAJI NA UVUNAJI WA GESI ASILIA NCHINI
 
1.0   UTANGULIZI
 
Wizara ya Nishati na Madini inapenda kutoa ufafanuzi wa miradi ya Gesi Asilia ambayo itatekelezwa kwa kushirikiana na wawekezaji katika Sekta ndogo ya Gesi Asilia na kueleza manufaa makubwa yatakayopatikana kwa wananchi wote wa Tanzania wakiwemo wale wa Mikoa ya Mtwara na Lindi.
 
Siku ya Alhamisi, tarehe 27 Disemba 2012, baadhi ya Vyama vya Siasa vya Upinzani viliratibu na kuhamasisha baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Mtwara, wengi wao wakitokea Mtwara Mjini kufanya maandamano ya kudai raslimali ya Gesi Asilia iwanufaishe wakazi wa Mtwara na kupinga mradi mkubwa wa ujenzi wa Bomba la Gesi Asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam. Wizara ya Nishati na Madini inapenda kutoa taarifa ifuatayo kwa Wa-Tanzania wote kwa kupitia vyombo vya habari.
 
Tokea Uhuru, uchumi wa Tanzania umetegemea kilimo cha mazao ya biashara kama vile katani (Tanga na Morogoro), pamba (Mwanza, Mara na Shinyanga), kahawa (Kilimanjaro, Kagera, Ruvuma na Mara), chai (Iringa) na tumbaku (Tabora). Fedha za mazao haya zimewanufaisha wakazi wa mikoa yote ya nchi yetu bila ubaguzi wo wote wala wakulima wa kutoka mikoa hiyo hawajawahi kufanya maandamano wakidai upendeleo (dhidi ya Wa-Tanzania wengine) wa aina yo yote ile.
 
1

 
Mapato yatokanayo na uchimbaji wa dhahabu (Mwanza, Geita, Mara, Shinyanga na Tabora), almasi (Shinyanga) na tanzanite (Manyara) yamewanufaisha Wa-Tanzania wote bila ubaguzi wo wote ule! Minofu ya samaki wa Ziwa Victoria (Mara, Mwanza na Kagera) imeliingizia Taifa letu fedha nyingi ambazo zimetumiwa na wakazi wa nchi nzima bila ubaguzi wo wote.
 
Aidha kuna mikoa ambayo inazalisha mazao ya chakula kwa wingi kwa manufaa ya Wa-Tanzania wote. Mahindi kutoka Rukwa, Mbeya, Ruvuma na Iringa yanasafirishwa kwenda mikoa yote ya nchi yetu bila kujali eneo yanakolimwa na wakazi wa mikoa hiyo hawajawahi kudai mahindi hayo ni kwa ajili ya watu wa mikoa hiyo pekee. Sukari ya Kilombero, Mtibwa na Kagera inatumiwa na wakazi wa mikoa yetu yote bila ya kuwepo madai ya mikoa inayozalisha sukari hii kupewa upendeleo wa aina yo yote ile. Maji ya Mto Ruvu yanatumiwa na wakazi wa Dar Es Salaam bila manung'uniko yo yote kutoka kwa wakazi wa eneo la chanzo cha Mto Ruvu.
 
Umeme wa kutoka Mtera, Kidatu na Kihansi (Dodoma na Morogoro), Hale (Tanga), na Nyumba ya Mungu (Kilimanjaro) unatumiwa na wakazi wote wa Tanzania bila ubaguzi au malalamiko ya wenyeji wa sehemu ambazo umeme huo unafuliwa na kusafirishwa kwenye Gridi ya Taifa. Kwa hiyo, kutokana na mifano hii michache, ni wajibu wa wazalendo na wapenda maendeleo wa kweli na hasa Wa-Tanzania wanaopinga ubaguzi wa aina yo yote ile kujiuliza kwa kina sababu zilizopelekea Vyama Siasa vya Upinzani kupanga, kuhamasisha, kushabikia na kuongoza maandamano ya tarehe 27 Disemba 2012 pale Mtwara Mjini.
 
2.0   RASLIMALI YA GESI ASILIA TANZANIA
 
Gesi Asilia ilianza kugundulika hapa nchini tangu mwaka 1974 kwenye Kisiwa cha Songo Songo, Mkoani Lindi. Baada ya hapo Gesi Asilia imegundulika maeneo ya Mtwara Vijijini, yaani Mnazi Bay (1982) na Ntorya (2012), Mkuranga (Pwani, 2007), Kiliwani (Lindi, 2008). Kiasi cha Gesi Asilia iliyogunduliwa katika maeneo haya inakadiriwa kuwa Futi za
 
2

 
Ujazo Trilioni 4.5 – 8. Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kumekuwa na kasi kubwa ya utafutaji Mafuta na Gesi Asilia uliojikita zaidi kwenye maji ya kina kirefu cha bahari. Kiasi cha Gesi Asilia iliyogundulika katika kina kirefu cha maji inafikia takribani Futi za Ujazo Trilioni 27. Kiasi cha wingi wa Gesi Asilia yote iliyogunduliwa nchi kavu na baharini inafikia takribani Futi za Ujazo Trilioni 35.
 
Kufuatana na Sheria za nchi yetu zinazotumiwa kugawa mipaka ya mikoa iliyopo kando kando mwa bahari (isivuke 12 nautical miles au 22.22 km kuingia baharini), Gesi Asilia iliyogunduliwa hadi sasa katika
 
-- Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    

0 comments:

Post a Comment