Thursday 10 January 2013

Re: [wanabidii] Tarime inaelekea wapi?

Kibaya zaidi ndugu zako nao hawana mtu wa kusemea bungeni.
Hali ni mbaya sana huko kwenu na wananchi wanahasira sana maana wako kwenye utajiri lakini utajiri huo hauwanufaishi na matokeo yake raslimali madini imegeula laana kwao maana wengi wameuwawa kwa kuhisiwa kuwa ni wavamizi au majambazi, hii imejenga chuki kubwa kati ya raia na wawekezeji. Mara ya mwisho nilipofika nilisikia kuna vijana walishawahi kudungua helkopta na kombea wakidhani kuwa ilikuwa imebeba dhahabu.
Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network

From: Victor Mwita <victormwita@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thu, 10 Jan 2013 14:22:23 +0300
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] Tarime inaelekea wapi?

Kila mwisho wa mwaka nimejenga mazoea ya kwenda nyumbani kwetu kijiji cha Muriba wilayani Tarime kwenda kuwasalimia wazazi na ndugu zangu huko. Lakini kila mwaka nazidi kupata impression kwamba maisha ya wananchi wa wilaya yetu yanazidi kudidimia. Kila ninapokua huko nakuta wizi wa mifugo unaombatana na mauaji ya kutisha ya raia unaendelea kama kawaida. Hii inanishangaza maana Serikali iliamua kuunda Kanda Maalum ya Kipolisi ili kushughulikia wizi na mauaji haya. Kwa mfano katika siku 6 nilizokaa huko (tarehe 28 Desemba hadi tarehe 03 Januari 2013) jumla ya watu wasiopungua watatu waliuawa katika vijiji ya Nyantira na Kimusi kutokana na wizi huo wa mifugo. Nashindwa kuwaelewa Polisi waliopo katika kanda maalum wanawezaje kushindwa kudhibiti hali hii. Nilichogundua kazi wanayoifanya ni kuwakusanya vijana wanaoonekana maeneo ya Nyamongo ambao wamewabatiza jina la intruders na kuwaweka ndani na kisha kuwatoa kwa kupokea laki 1 kwa kila kijana. Hii nayo inazidi kufanya wazazi wawe maskini zaidi maana hakuna mzazi anayekubali kijana wake afungwe. Niliwahi kusikia maelekezo ya Serikali kwamba wawekezaji katika migodi wanalazimika kutenga maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo. Hilo halijafanywa na Barrick bali wamechukua kila eneo lenye dhahabu. Hawa wachimbaji wadogo sijui kama waziri wa madini anaweza akawasaidiaje. Tatizo ninaloliona ni ile dhana ya kuwadharau watu wa Tarime kwamba wanapenda vita kitu ambacho hakina ukweli sana. Kingine ni ubovu wa barabara katika wilaya hiyo. Nashangaa Halmashauri na TanRoads Mara wanashindwaje kurekebisha barabara za Tarime! Hata ile barabara ya Sirari to Muriba ambayo inapata ruzuku ya EU kwa ajili ya Kahawa haijafanyiwa matengenezo tangu mwaka 2005. Watu wanalazimika kulipa nauli kubwa kwa safari fupi ya kilometa 26! Kitu kingine kinacholeta kero kwa wananchi wa huko ninakotoka ni ukosefu wa mawasiliano ya simu. Utafiti unaonyesha kwamba karibu kila familia inamiliki simu zaidi ya moja lakini hakuna mtandao kabisa. Nashangaa hawa service providers wameweka minara yote Nyamwaga ambapo ni bondeni!!! Kero nyingine ni masoko ya mazao hayapo kabisa na matokeo yake wananchi wanauza mazao yao Kenya. Ina maana hakuna namna ya kuyanunua mazao yanayolimwa huko kwetu? Jamani somebody has to do something ili kuwasaidia wananchi wa huko wasiendelee kuwa maskini. Inaniuma sana jameni

--
Victor Caleb Mwita
Ministry of Livestock and Fisheries Development
P.O. Box 9152
Dar Es Salaam
Tel: 0766750673, 0789142275

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment