Thursday 17 January 2013

RE: [wanabidii] Research za Talaka

Dada Hilda, nimepata elimika sana. Nina hakika walio wengi hawajui kuwa kipato ni uhuru na ndio maana mfumo dume unanyima fursa ‘KE’. Hongera kwa kipande hiki. Demetria Kalogosho

 

From: wanabidii@googlegroups.com [mailto:wanabidii@googlegroups.com] On Behalf Of Hildegarda Kiwasila
Sent: Friday, January 18, 2013 8:08 AM
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Research za Talaka

 



Research Design yako inasemaje-is it a comparatory cross-sectional study or one case study area? Kufanya eneo moja haitokusaidia kuelezea sababu na kulinganisha na maeneo mengine na sababu zake. Kuna maeneo mengine nchini hata kama mume akimuacha mke au hamtaki na haingii nyumba yake, bado yu mkewe na anakwenda kuchukua hela akisha kuuza mazao au mfugo, atachukua mfugo auze labda kama mama ana watoto wa kiume wakubwa wamfukuze baba yao.Akitaka asimsogelee wazazi wa mke budi warudishe mahari (mifugo). Wakati huo huko aliolewa mdogo, amezaa, amezeeka mifugo irudi why (nenda wilaya za Mikoa za Ziwa kwa wasukuma na eneo la Mara region-Musoma Rural, Tarime, Serengeti). Mikoa ya Pwani ni matrilineal au hurithi kwa Mama. Mtoto wa Kike na wa kiume hupata mgao wa mali sawa. Mume hana mamlaka na mali ya mke aliyerithi kutoka kwao. Ila studies zimeonyesha-wanaume humdanganya mke kumfanya amuandikishe yeye jina kama anampenda kweli. Mashamba yanapopimwa au kuandikishwa kijijini aandike Mrs yeye sio Ms Mariam Abdalla bali Mrs Mariam Hussein-jina la mume Hussein au aandike Mr A. Hussein.... akisha kuipata mali hiyo ya mashamba ya minazi na mkorosho, bonde la kilimo cha mpunga anaanza kuuza kisingizio waanzishe biashara. Akipata hela hujenga nyumba nzuri, kufungua duka etc na kuoa mke mwiongine wa nyongeza maana ana mali sasa. Hii huzusha ugomvi, kesi za talaka na ugomvi wa mali. Huko Mikoa ya Lindi na Mtwara akina mama wazee wamepoteza mali zao kwa mtindo huu wa mume kutaka mali iandikishwe jina lake kama anampenda kweli na kumuamini. Utafiti ulifanywa miaka ya mid 1990s hivi.

Talaka pia ni situational kama kuna mfumo fulani mpya wa maisha ulioingia mahala ukawaamsha wanawake mfano-Ujasiriamali.Hawabaki tena kuwa watumwa wa mila kuonewa, kunyanyaswa na kukubali kuteseka. Wanapata kipaumbele mikopo ya Fica and other NGO funding support. Ana hela haonewi tena kupigwa na kurudiwa asubuhi na wakwe mawifi kumuonea.anayo hela anajitegemea kitu ambacho waume wengine hawakitaki na shinikizo toka nduguze. Hapa mke huomba talaka unless apewe uhuru afanye biashara zake kwenda kununua samaki Rufiji-Bagamoyo, anakaanga ndoo kadhaa anakwenda kuuza Morogoro-chalinze kutoka DSM.Mwingine anakwenda Nairobi, China kubeba bidhaa kuuza. Kubeba mbao Iringa kuleta DSM. Hapa talaka huongezeza kutokana na kutaka Uhuru kibiashara na matrilineal societies zitaongezeka maana wanawake hawakubali kuonewa na ukimpiga tu ndugu na wazazi wanakuvalia njuga-muache. hawapigwi hovyo na kuogopa kuondoka kurudi kwao kama maeneo ya patrilineal ambapo unapigwa na ukirudi kwenu unafukuzwa rudi huko huko-nani arudishe ng'ombe!
Maeneo mengi traditional na ya coast ya waislam mfano Lushoto usambaani, ZNZ, bagamoyo, Lindi, Morogoro etc wanawake waliolewa ktk umri mdogo. Hivi waume zao walizeeka wao wakiwa mid years mume mzee sana hajiwezi kikazi. Mikopo ya ujasiriamali ya vocoba etc imewapa wanawake uwezo wa biashara na uzalishaji mali. Baadhi wamefungua magenge, maduka home na kuwaajiri waume zao ambao hubaki home na kusimamia genge, duka etc na huwalipa mshahara na kibabu nacho kinauza sigara zake, nazi hapo kuongeza kipato na ni mstaafu ajira au hana uwezo wa kilimo tena. Hii utaikuta Bagamoyo, Lushoto-Mnazi, Mkundi Mbaru; Pare maeneo ya Mikonge zamani vibabu wastaafu mikongeni wapo hoi.

Kukiwa na miradi ya ujenzi wa barabara, Madaraja, Mabwawa yafanyayo na kampuni za kigeni au local waletao wafanyakazi wa ndani na nje ambapo eneo hujaa wanaume wenye hela watafutao vimwana ambapo baadhi yao  wapo ktk ndoa ya wake 4 hadi 6 etc talaka hutokea ghafla kuwa tatizo namba moja. Wanawake huona kuwa wana market yao ni kubwa wanatakiwa leo yupo anateseka na kuzeeka ktk penzi la kuchangia-wanaacha wachumba na waume zao na kudai talaka. Fungua mafaili ya vijiji-Kata kama yapo bado ya maeneo ya Mtera Dam, Kidatu, Pangani I and II ya Kihansi hydropower stations utaona hili. walipokuwa wanajenga Daraja la Mkapa-Rufiji au wanakojenga barabara mpya kwa sasa-Teget-bagamoyo-chalinze na maeneo mengine TZ. Ila matokeo yake ni vifo. Maana wale wanaume wenye hela waendeshao malori makubwa, makatapila watokao Somalia, ethiopia, Kenya etc wageni na wenyeji toka bongoland baadhi walikuwa HIV positive wamewapa penzi la dhati la muda (walipata pa kuengemea na pa kupata kulelewa) walikuwa HIV positive. Baadhi waliondoka baada ya mradi na kuwaachia maradhi na watoto walizaliwa positive au kufariki nao baada ya miaka kadhaa effect zake zinaonekana kwao. talaka huwa number 1 maeneo ya miradi mikuja ya muda mrefu. Ndio maana social and cultural impact assessment huandika miradi ya kuelimisha jamii kuepuka matatizo kama haya. Hivyo ingefaa ufahamu-factors nyingine zaidi ya mila na desturi ambazo zinaweza kuwa kichokoo cha talaka kufanya zionekane kuwa tatizo kuu kuliko maisha ya ndoa ya kawaida na mlongo wa mama au baba kuwa sababu pekee. Katika shughuli zetu za utafiti bongoland tunakutana na haya. 1997 niliona sauala hili la talaka kuwa namba 1 ghafla Mapanda ward kutokana na mradi wa Bwawa la umeme la Kihasi. Tofauti na tafiti zetu za nyumba eneo hilo za 1989, 1992. Vivyo hivyo katika evaluation ya Pangani II mid 2000.

--- On Thu, 17/1/13, Wilson Gwoma <gwomason@yahoo.co.uk> wrote:


From: Wilson Gwoma <gwomason@yahoo.co.uk>
Subject: Re: [wanabidii] Research za Talaka
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thursday, 17 January, 2013, 13:51

Nakushauri ufanye research yako kwenye kijiji kimoja wapo cha mikoa ya pwani maana my experience talaka nyingi ziko ukanda huo kutokana na mila na desturi za watu wa ukanda wa pwani, sina maana maeneo mengine hakuna talaka but ukanda huu unaongoza, Chagua kijiji kimoja tu, utapata majibu ya kutosha.--- On Thu, 17/1/13, Festo Liheta <fliheta@yahoo.co.uk> wrote:


From: Festo Liheta <fliheta@yahoo.co.uk>
Subject: [wanabidii] Research za Talaka
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, 17 January, 2013, 14:20

Ndugu wanabidii, nafanya research kuhusu talaka, naomba yeyote ambaye amewahi kuona au amefanya research kuhusu talaka kwa tanzania anisaidie manake nimeshindwa kabisa kupata kazi za hapa tanzania. natanguliza shukrani zangu.

Festo

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment