Sunday 13 January 2013

Re: [wanabidii] Re: MWANGOSI NA DR ULIMBOKA WAMUWEKA PABAYA JK

Yona. Naogopa kusema ukweli ukasema nimekutukana.
Nilizaliwa mwaka 1952.
Ni mwana CCM kwa itikadi (Ujamaa na kujitegemea). Nimeishi hivyo na najaribu kuwalea watoto wangu hivyo.
Ninaposema watu kwenda Msituni huenda likaja baada yangu kufa.
Nasema na narudia unapoona watu wanahangaika kupeleka malalamiko yao Washington ujue hiyo ni dalili mbaya. Unapobeza na kusema waache waende unawafanya watunwawe na mashaka na wapangaji unaowatunza (Kichwani).
 
Tatizo si dalili mbaya. Tatizo ni kukosa masikio ya kuelewa hali hiyo watu kama wewe au kwa sababu huelewi au unaogopa kuonyesha kuwa umeelewa.
 
Kuna hali mbaya inayojionyesha na sasa ni 'Fooly known'. Hali hiyo inapojitokeza na watu katika mitandao wakaisemea ni vizuri mkanyamaza kuliko kuwabeza wanaoumizwa nayo.
 
Soma tena ujumbe wangu unaoujibu. Waza tu kuhusu nilichoandika kuhusu Mwangosi na Ulimboka. Jiambie ukweli.
 
Kama huwezi kuuunga mkono ukweli labda kwa sababu ya ajira yako nyamaza kimya au tafuta kazi nyingine uifanye.
 
Jione unavyoeleweka unapotoa maoni juu ya madhaifu tunayoyaona ndani ya Serikali yetu.
Wakati wa Siad Barre ilionekana kuwa akitoka tu nchi itasambaratika.
Wakati wa Tito, ilijulikana kuwa nchi itakosa kutawalika.
Tunasema kuwa tusiharakishe kuunda shirikisho la Africa Mashariki hadi Museven wa Uganda awe amemaliza mihula miwili ametoka madarakani maana anavyoiongoza uganda inaweza kuingia civil war baada yake.
 
Tunasema Tanzania inaelekea kubaya ila hali haijaenda out of Control.
Unaposema sera za vyama hazijulikani wakati serikali yetu inatekeleza sera za vyama hivyo unafanya tufikiri kuna Yona wawili au watatu. Yuko anayetoa taarifa zenye mashiko na huyu watu wanayesema ana shida gani kichwani.
 
Nikijua kuwa mawazo unayotoa ni yako au ni ajira nitakuelewa zaidi. Lakini hadi sasa kama ni ajira nami niliwahi kubadilisha ajira. Badilisha. Waliokwenda msituni (ambako naonya tusiwapeleke vijana) waliumia sawa kama waliokuwa mijini. Tanzania iliwasaidia wanamibia, Wazimbabwe wamsumbiji kwenda huko. Tunahitaji kujua kabla ya kwenda kuwa ni kubaya. Ndilo lengo letu kusema hivyo. Siamini kuwa huelewi.
Najua wewe si mvivu wa kusoma. Na maandishi haya si mengi kukushinda kuyasoma mara mbili na ukaelewa nilichomaanisha.
Marahaba.


--- On Sun, 1/13/13, Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:

From: Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>
Subject: [wanabidii] Re: MWANGOSI NA DR ULIMBOKA WAMUWEKA PABAYA JK
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, January 13, 2013, 1:01 AM

Elisa kama kuingia msituni wewe sio mtu wa kwanza kusema hivyo na
haitokuwa mara ya kwanza kwa watu kuingia msituni ila ujue kama ikiwa
hivyo hakuna atakayefaidika , nyie sambazeni vyama vyetu , toeni sera
zenu zikubalike mchaguliwe watu wawaamini wawaingize madarakani lakini
kinyume na hapo mmedoda , watu wanasimama kwenye mikutano ya hadhara
hawana agenda ya pamoja , toka mwaka 2010 mpaka sasa hivi hawasemi
watafanya nini au wamefanya nini leo wanatuletea hii .na wewe
unatishia kuingia msituni .

Ingia msituni utapambana na sokwe na watakutoa nishai .

On Jan 13, 5:19 am, denis Matanda <denis.mata...@gmail.com> wrote:
> Nakuheshimu kaka na najua unajua ukweli kwenye hili!
> On Jan 12, 2013 5:39 PM, "Yona Maro" <oldmo...@gmail.com> wrote:
>
>
>
>
>
>
>
> > Hii nchi inaendeshwa kwa sheria na taratibu zake zilizopo - Haiendeshwi na
> > Washington wala New York wala matamko yao .
>
> > 2013/1/12 Mohamedi Mtoi <mouddym...@gmail.com>
>
> >> **
> >> Kwa nini mseme kuwa sio Dr Kafumu? Kwa nini mu-msemee mtu ambaye tayari
> >> kasha sema tena kwa kukitilia shaka kile alicho sema?!
>
> >> Kauli hii ya Kafumu inasadifu kilicho ndani ya mioyo ya viongozi waliooko
> >> kwenye utawala unao anguka.
>
> >> Asicho kiamini Kafumu ndio ambacho hakiamini Bosi wake kuwa mahakama
> >> imetendeka kazi yake kumvua ubunge! Matokeo yake Bosi naye ana ishangaa
> >> mahakama kumvua Kafumu ubunge kama Kafumu anavyo shangaa alio waita wana
> >> harakati wa magharibi.
>
> >> Huu ni msiba.
> >> Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network
> >> ------------------------------
> >> *From: * kimd...@gmail.com
> >> *Sender: * wanabidii@googlegroups.com
> >> *Date: *Sat, 12 Jan 2013 12:40:56 +0000
> >> *To: *<wanabidii@googlegroups.com>
> >> *ReplyTo: * wanabidii@googlegroups.com
> >> *Subject: *Re: [wanabidii] MWANGOSI NA DR ULIMBOKA WAMUWEKA PABAYA JK
>
> >> Nadhani huyu siyo Dr. Peter Kafumu aliyegombea ubunge Igunga na kama ni
> >> yeye maadinko haya yanatupa picha ya mhusika! Katika karne hii baadhi ya
> >> wasomi kama ndugu yetu, mwenye PhD, bado tunaona mfumo wa chama kimoja ni
> >> sahihi! Very Interesting! Kweli bado tuna mwendo mrefu na inatia shaka kama
> >> tutafika
> >> Idriss Mussa
> >> Sent from my BlackBerry® smartphone from Orange Botswana
> >> ------------------------------
> >> *From: * Dr Peter D Kafumu <kaf...@yahoo.com>
> >> *Sender: * wanabidii@googlegroups.com
> >> *Date: *Sat, 12 Jan 2013 03:40:44 -0800 (PST)
> >> *To: *<wanabidii@googlegroups.com>
> >> *ReplyTo: * wanabidii@googlegroups.com
> >> *Subject: *Re: [wanabidii] MWANGOSI NA DR ULIMBOKA WAMUWEKA PABAYA JK
>
> >> Hivi wale vijana aaliokufa morogoro na kule singida mbona wao
> >> hawatambuliki kuwa ni wahanga wa siasa hizi chafu za kiamgharibi za vyama
> >> vingi?
>
> >> --- On *Sat, 1/12/13, Mohamedi Mtoi <mouddym...@gmail.com>* wrote:
>
> >> From: Mohamedi Mtoi <mouddym...@gmail.com>
> >> Subject: [wanabidii] MWANGOSI NA DR ULIMBOKA WAMUWEKA PABAYA JK
> >> To: wanabidii@googlegroups.com
> >> Date: Saturday, January 12, 2013, 8:44 AM
>
> >> KUUAWA kikatili kwa mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daudi Mwangosi na
> >> tukio la kutekwa, kuteswa kwa kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk.
> >> Steven Ulimboka, limechukua sura mpya ambapo sasa limetinga katika Seneti
> >> ya Marekani, Tanzania Daima Jumamosi limeelezwa.
>
> >> Taarifa kutoka Washington nchini Marekani zinasema Rais Jakaya Kikwete
> >> amelalamikiwa rasmi katika Seneti na wanaharakati na watetezi wa haki za
> >> binadamu nchini, na kwamba masuala hayo sasa yatafikishwa kwenye Shirika la
> >> Umoja wa Mataifa la Kutetea Haki za Binadamu (UNHRC) kwa hatua zaidi.
>
> >> Mbali na mauaji ya Mwangosi na tukio la Dk. Ulimboka, Rais Kikwete pia
> >> amelalamikiwa kwa kufumbia macho matukio mengi ya kuteswa na kuuawa kwa
> >> raia pamoja na kufungiwa kwa gazeti la kila wiki la uchunguzi la
> >> MwanaHalisi, kutoroshwa wanyama hai kwa kupelekwa nje ya nchi na hatua ya
> >> polisi kutumia silaha za kivita kupambana na raia wasio na silaha wakiwemo
> >> wanafunzi wanaoandamana.
>
> >> Ripoti hiyo ya wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu yenye kurasa
> >> 27, inatuhumu utawala wa Rais Kikwete kwa kukandamiza demokrasia kwa
> >> kutumia polisi na vyombo vingine vya dola.
>
> >> Watetezi hao wa haki za binadamu, wamedai kuwa baada ya kufanikiwa
> >> kuingiza masuala haya ya ukiukwaji wa haki za binadamu katika Seneti ya
> >> Marekani, sasa wanafanya kila liwezekanalo kuhakikisha suala hili
> >> linafikishwa Umoja wa Mataifa kwa kile walichokiita, kuiadabisha serikali.
>
> >> Kwa mujibu wa nyaraka zilizopatikana, na pia kusambazwa katika baadhi ya
> >> taasisi za habari, suala hilo liko mikononi mwa Seneta Kerry, ambaye baada
> >> ya majadiliano katika Seneti, ripoti hiyo itapelekwa UNHRC.
>
> >> Habari zinasema baadhi ya wajumbe wa Seneti waliofanikiwa kuona ripoti
> >> hiyo wamemeshitushwa na kile walichokishuhudia katika picha
> >> zilizoambatanishwa.
>
> >> Aidha, ripoti hiyo pia imeeleza jinsi rushwa ilivyoshamiri nchini,
> >> ukandamizaji juu ya uhuru wa maoni na matumizi mabaya ya vyombo vya dola
> >> kudhibiti vyama vya upinzani na kutumia silaha za kivita kupambana na raia
> >> wasio na silaha.
>
> >> Ripoti hiyo ya kuishitaki Serikali ya Kikwete, pia imelaani vitendo vya
> >> polisi kusambaratisha maandamano ya wanafunzi wa shule za msingi jijini Dar
> >> es Salaam, walioandamana Julai 31, mwaka jana kupinga ukosefu wa walimu
> >> nchini.
>
> >> Mgomo wa wanafunzi ulikuja baada ya walimu wa shule za msingi na
> >> sekondari kupitia jumuiya yao - Chama cha Walimu Tanzania (CWT) – kuitisha
> >> mgomo nchi nzima wa kutaka kuboreshwa kwa mazingira ya kazi zao, nyongeza
> >> ya mishahara na malimbikizo ya posho.
>
> >> Nyaraka zilizowasilishwa na wanaharakati hao, zimeambatanishwa na picha
> >> zinazoonesha namna Jeshi la Polisi lilivyohusika kuuawa kwa Mwangosi, picha
> >> mbaya ya maiti ya mwanahabari huyo, na namna Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
> >> Iringa, Michael Kamhanda alivyokuwa akishuhudia askari wake wakimsulubu
> >> mwanahabari huyo kabla ya kufunga kazi kwa kumaliza uhai wake.
>
> >> Kadhalika, kumeambatanishwa picha zinazoonesha maiti za watu waliouawa
> >> wakati wa maandamano huko Arusha, na ile inayosadikiwa kutokea kule Songea.
> >> Picha nyingine za kusikitisha ni zile zinazoonesha askari zaidi ya watano
> >> wakimdhibiti mwanaharakati mmoja katika maandamano, na umati wa wanafunzi
> >> wa shule za msingi wakiandamana, huku nyingine zikionesha askari mwenye
> >> silaha ya kivita akimsindikiza mwanafunzi wa kike mwenye mfuko wa madaftari.
>
> >> Tangu mwaka 2005 ambapo masuala mazito ya rushwa yamekuwa yakiibuliwa,
> >> ikiwamo ununuzi wa rada feki, wizi wa fedha za umma kutoka kwenye Akaunti
> >> ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), mkataba tata
> >> wa Richmond, ukusanyaji wa kodi, utoroshwaji wa wanyama hai, wizi wa nyara
> >> za serikali, ikiwamo pembe za ndovu, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituhumu
> >> serikali kushindwa kuchukua hatua.
>
> >> Vilevile, wananchi wamekuwa wakituhumu Serikali ya Kikwete, kukumbatia
> >> wezi wa fedha za umma katika halmashauri za miji na wilaya, uporaji wa
> >> ardhi unaofanywa na makampuni makubwa ya ndani na nje ya nchi.
>
> >> Jana, Tanzania Daima Jumamosi haikufanikiwa kumpata Mkurugenzi wa
> >> Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu kuzungumzia iwapo serikali ina taarifa
> >> juu ya jambo hili kwa kuwa simu yake ilikuwa ikiita muda wote bila
> >> kupokelewa.
>
> >> Kova ajivua
> >> Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, Suleiman Kova jana
> >> ametangaza rasmi kujivua katika sakata zima la kuchunguza kutekwa na
> >> kuteswa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Ulimboka.
>
> >> Aidha, Kova pia amekanusha madai ya kuunda tume kuchunguza suala hilo,
> >> akitaka asiulizwe jambo lolote, huku akisukuma tukio hilo kwa wakubwa wake.
>
> >> Juzi, Kamanda Kova aliliambia Tanzania Daima kwamba, jana angeweka wazi
> >> suala hilo ili Watanzania wajue kilichojiri kuhusiana na kutekwa na kuteswa
> >> kwa Dk. Ulimboka, jambo ambalo limetikisa anga, likiwemo lile la kukamatwa
> >> kwa raia wa Kenya, Mulundi anayedaiwa kuhusika na tukio hilo.
>
> >> Hata hivyo, kinyume na matarajio ya wengi, jana Kamanda Kova aliruka
> >> kimanga na kudai kwamba wenye uwezo wa kulitolea maelezo ni wakuu wake wa
> >> kazi, kwa maana ya Ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.
>
> >> Kuhusu kuundwa kwa kamati ya kuchunguza utekaji huo, Kova alisema
> >> kilichofanyika wakati huo ni kuundwa kwa jopo la uchunguzi ambalo taarifa
> >> zake hazina ulazima wa kutolewa mbele ya jamii zaidi ya kutumika kwa ajili
> >> ya utekelezaji wa kile walichokibaini.
>
> >> Alisema baada ya kukamilisha kazi yake, alipeleka jukumu la kupeleleza
> >> sakata hilo katika ofisi ya mkurugenzi wa makosa ya jinai nchini (DCI)
> >> ambayo ndiyo yenye jukumu la kutoa maelezo.
>
> >> Chanzo: Tanzaniadaima 12 Jan, 2013.
> >> Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network
>
> >> --
> >> Jobs in Africa -www.wejobs.blogspot.com
> >> International Jobs -www.jobsunited.blogspot.com
>
> >> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> >> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com<http://us.mc1601.mail.yahoo.com/mc/compose?to=unsubscribe@googlegroup...>
> >> Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> >> Disclaimer:
> >> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
> >> legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts
> >> must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you
> >> agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
> >>  --
> >> Jobs in Africa -www.wejobs.blogspot.com
> >> International Jobs -www.jobsunited.blogspot.com
>
> >> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> >> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> >> ukishatuma
>
> >> Disclaimer:
> >> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
> >> legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts
> >> must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you
> >> agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
> >> --
> >> Jobs in Africa -www.wejobs.blogspot.com
> >> International Jobs -www.jobsunited.blogspot.com
>
> >> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> >> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> >> ukishatuma
>
> >> Disclaimer:
> >> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
> >> legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts
> >> must be presented responsibly. Your continued membership
>
> ...
>
> read more »

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment