Monday 21 January 2013

Re: [wanabidii] Re: MARAIS WA ZAMANI WA ZANZIBAR WATAKA MUUNGANO WA MKATABA!

Kaka Matinyi,
Mengi yanasemwa pande zote mbili, lakini la muhimu ni hali ipo vipi hivi sasa baina ya washirika hawa wawili?
Kweli ni Muungano wa nchi mbili au wa nchi moja na jimbo fulani?

...bin Issa.


From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: saidissa100@yahoo.com
Sent: Monday, January 21, 2013 11:05:39 AM
Subject: RE: [wanabidii] Re: MARAIS WA ZAMANI WA ZANZIBAR WATAKA MUUNGANO WA MKATABA!

Issa,
Ina maana wewe humjui "Hapa pangu"? Humjui siyo? Karafuu iko wapi siku hizi? Wale waliotaka kuufutilia mbali utalii washatulia? 
Halafu siamini kwamba eti wewe Issa hujui kuwa wimbo mkubwa visiwani hivi sasa ni kwamba Waarabu wataleta misaada kuanzia na Oman, halafu Arab League, OIC, na mataifa mengine, na hoja ni kwamba eti Zanzibar ni ndogo, Wazanzibari ni wachache, kwa hiyo misaada itasaidia zaidi. Huo wimbo mpaka Maalim Seif anauimba, bila hata haya, akija huku na kwingineko. 
Lakini pia hili la "sisi" na "ninyi" halifai kabisa. Ni ubaguzi tu. Muungano una malalamiko yake na kama tungekuwa viongozi makini yangetatuliwa, lakini ubinafsi wa viongozi wa Tanzania, siyo Tanzania Bara, ndiyo tatizo. Ninaposema ubinafsi viongozi nazungumzia TANZANIA, yaani Bara na Visiwani.
Matinyi.

 

Date: Mon, 21 Jan 2013 10:52:22 -0800
From: saidissa100@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] Re: MARAIS WA ZAMANI WA ZANZIBAR WATAKA MUUNGANO WA MKATABA!
To: wanabidii@googlegroups.com; matinyi@hotmail.com

Kaka Matinyi,
Sasa kaka Matinyi kama kwanza ilikuwa Seif, halafu Karume na sasa Salmin na kesho Shein, hivyo bado hujafahamu tu Wazanzibari wanasema nini?
Kama hukubali kuwa matatizo yaliyopo ni kwasababu ya Muungano basi kwanini hatuwezi kuyatatua?

>Shida yetu kubwa ni kwamba tuna viongozi wezi, wabinafsi na sisi wananchi hatufanyi kazi.
Hili ndilo jambo moja linalotufanya tuukimbie huu Muungano. Wenzetu mmezidi wizi na sio wizi tu lakini hata mkiwapata hao wezi hamfanyi kitu kwasababu ndio nyinyi wenyewe wezi - samahanini kwa lugha jamani, kwani sisemi kuwa nyote ni wezi - ni wakubwa wenu tu.
Mzee Vijisenti kakubali kuwa anapesa nje, je, aliulizwa chochote? Yule Mhindi wa Radar yupo Switzerland, je, tumechukuwa hatua zozote za kumrejesha? Sitaki hapa kuzungumzia juu ya hizo pesa zilizofichwa huko huko Switzerland na ambazo serikali haitaki kuzidai kama Balozi wa Switzerland alivyoeleza. Mambo haya sisi Wazanzibari tunahisi yanasaidia kuturejesha nyuma, japokuwa nasi sio Mitume!

>si kweli kwamba wajomba zetu watatoa misaada kama watu wanavyodanganyana kila kukicha
Tamaa ya misaada Wazanzibari hatuna. Kwani hivi sasa tunakuenda kwa misaada kutoka nchi gani? Wanaopata misaada zaidi baina ya sisi na nyinyi ni nani? Suala la mgawanyo wa misaada kutoka nje pamoja na ajira kwa wazanzibari ndani ya taasisi za Muungano baada ya miaka 49 kupita ndio kwanza lilipata muelekeo majuzi hapa Unguja. 
Kwahivyo, Kaka Matinyi, sisi hatutegemei misaada hata kidogo. Misaada ni yenu nyinyi. Sisi tunategemea vikia vya mbuzi!
And this reminds me juu ya zile pesa kutoka South Korea. Kaka zitafika lini hizi pesa Visiwani? Naona ulizitaja sana!

...bin Issa.


From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Monday, January 21, 2013 10:11:58 AM
Subject: RE: [wanabidii] Re: MARAIS WA ZAMANI WA ZANZIBAR WATAKA MUUNGANO WA MKATABA!

Issa,
 
Kuwaelewa Wapemba wanasema nini ni jambo moja, na kujadili wanachokisema akina Seif na mwenzake Karume na sasa Salmin ni jambo jingine kabisa. Mimi nisichokubaliana nacho ni unafiki wa kusema "tunataka muungano wa mkataba" wakati wanachokisema ni "tuuvunje muungano".
 
Aidha, mimi sikubaliana na madai kwamba matatizo yaliyopo yatatatuliwa na hatua ya kuuvunja muungano. Shida yetu kubwa ni kwamba tuna viongozi wezi, wabinafsi na sisi wananchi hatufanyi kazi. Umaskini utazidi pale tutakapochukua hatua ya kuuvunja muungano kwa kuwa kila upande utajiongezea gharama zisizokuwa na sababu za kuiendesha nchi na .
 
Tutaongeza matatizo tu; na wananchi wetu wanadai mengi wasiyoyaelewa kutokana na uongo wa viongozi wetu.
 
Matinyi.
 

Date: Mon, 21 Jan 2013 10:08:00 -0800
From: saidissa100@yahoo.com
Subject: [wanabidii] Re: MARAIS WA ZAMANI WA ZANZIBAR WATAKA MUUNGANO WA MKATABA!
To: matinyi@hotmail.com; wanabidii@googlegroups.com

Kaka Matinyi,
Kama ungeliishi Pemba labda ungelifahamu hawa Wazanzibari wanasema au wanataka nini.
Anyway, labda ipo siku utawafahamu!

..bin Issa.


From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: saidissa100@yahoo.com
Sent: Monday, January 21, 2013 9:54:22 AM
Subject: RE: MARAIS WA ZAMANI WA ZANZIBAR WATAKA MUUNGANO WA MKATABA!

Wanachozungumzia Watanzania hawa wawili, Salmin na Karume, ni kuuvunja Muungano kwa kuwa hakuna kitu kama hicho kinachoitwa Muungano wa Mkataba. Kwani huu hauna mkataba? Hiyo mifano waliyoitoa siyo miungano ingawa inatumia neno "muungano" na hili ni suala la uelewa tu.
 
Kwa hiyo wao hazungumzii MUUNGANO bali wanazungumzia kuuvunja Muungano uliopo.
 
Tusichanganye mambo. Hakuna Muungano wa nchi mbili zenye madaraka yote ndani na nje. Hakuna.
 
Matinyi.
 

Date: Mon, 21 Jan 2013 09:48:43 -0800
From: saidissa100@yahoo.com
Subject: MARAIS WA ZAMANI WA ZANZIBAR WATAKA MUUNGANO WA MKATABA!
To: wanabidii@googlegroups.com

Rais Mstaafu wa Zanzibar, Baba wa Maridhiano ya wazanzibari na Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambae ni mtoto wa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya watu wa Zanzibar, Mhe Amani Abeid Amani Karume leo amekutana na Jaji Joseph Warioba na kuwasilisha maoni yake. Katika maoni yake amesema kwamba wakati wa siku za mwanzoni, Muungano ulikuwa wa heshima na usawa kati ya Zanzibar na Tanganyika lakini kadiri siku zinavyokwenda unachukua sura ya nchi moja -Tanganyika – kuuhodhi Muungano huo dhidi ya Zanzibar. Akasema akiwa Rais kwa kipindi cha miaka 10 ameshuhudia mengi dhidi ya maslahi ya Zanzibar. Alisema hizi ni zama mpya za uwazi na ukweli na kwa hali iliyofikia sasa hakuna njia nyengine zaidi ya kila nchi – Zanzibar na Tanganyika – kurejesha mamlaka yake (sovereignty) kitaifa na kimataifa na kisha nchi hizo mbili kushirikiana kupitia Muungano wa Mkataba kati yao. 

Chanzo: Mzalendo

Taarifa kutoka kwa watu wa karibu na Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour, zinaeleza kwamba kiongozi huyo ametoa maoni yake tarehe 13 Januari, 2013 na katika maoni yake ameieleza Tume ya Mabadiliko ya Katiba ikiongozwa na Joseph Warioba kwamba anataka kuona Zanzibar na Tanganyika kila moja ikiwa ni nchi yenye mamlaka kamili ndani na nje na kisha zishirikiane kwa mfumo wa ushirikiano kama ule uliopo baina ya nchi za Afrika kupitia Umoja wa Afrika (AU). Dk. Salmin Amour amesema msingi wa umoja wa nchi za Afrika umetokana na mashirikiano kati ya vyama vya ukombozi chini ya PAFMECA. Akasema Umoja wa Vyama vya Ukombozi vya Afrika Mashariki na Kati (PAFMECA) ulitambua haja ya nchi za Afrika kuungana baada ya uhuru lakini kwa msingi wa kuheshimu mamlaka ya kila nchi (sovereignty) na mipaka yake. Hivyo, akataka mahusiano mapya kati ya Zanzibar na Tanganyika uzingatie msingi huo ambao ndiyo pia uliojenga misingi ya Umoja wa Afrika (African Union). Waliokuwa bado wana mashaka na umoja wa Wazanzibari katika kutaka mamlaka yao kamili naamini sasa watawafahamu Wazanzibari.
Waasisi wawili wazito wa Zanzibar ambao uzalendo wao hauna mashaka, aliyekuwa Katibu Mipango wa ASP, memba wa Baraza la Mapinduzi la mwanzo kabisa mwaka 1964 na Waziri katika Wizara tofauti za Serikali ya Zanzibar na ya Muungano kwa miaka mingi, mwanachama wa CCM mwenye kadi ya uanachama nam. 7, Mzee Hassan Nassor Moyo, na Katibu Mkuu wa mwanzo wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia alikuwa Naibu Waziri katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na katika Serikali ya Muungano na kisha akawa Balozi wa Tanzania nchini Guinea na Ethiopia, Mzee Salim Said Rashid, wamemaliza kutoa maoni yao mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba asubuhi hii. Wote wawili hawakutafuna maneno jinsi Zanzibar ilivyodhulumiwa katika Muungano huu wa kikatiba na wakamalizia kwamba wanataka Zanzibar yenye mamlaka kamili ndani na nje ya nchi itakayofuatiwa na Muungano wa Mkataba kati yake na Tanganyika.

Chanzo ni facebook ya ismail juss/MZALENDO



--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 




0 comments:

Post a Comment