Hildegard, Nlitamani sana kusoma taarifa yote ya utafiti ili niweze kuchangia zaidi. Taarifa hii inaeleza kwa ufinyu sana mambo halisi ya Mererani. Haioneshi kwamba wanaopata fedha, wale wauzaji wa Tanzanite iliyochimbwa nawakwenda kujenga wapi au wanawekeza wapi. Kwa taarifa yako, pamoja na kwamba madini hayo yako Manyara lakini uwekezaji mkubwa unafanyika Arusha. Kuna mtaa Arusha ukifika hapo utakua Wamasai kibao wanauza madini yao na mafanikio yao utaanza kuyaona kuanzia kwenye sura zao. Wale wanaoathirika na UKIMWI pale ni vibarua tu. Watu waliokwenda kule kwa kutegemea watapata kitu. Wakati mwingine wanajikuta hawana hata mlo wanaangukia kwenye umasikini. Mererani hakuna barabara ya lami iliyofika kule. Barabara ni mbovu kwa miaka yote hiyo ya uchimbaji!!!!! Hakuna hospitali kuna kizahanati tu. Mbona hajakipiga picha ukione??? Yapo mengi ila kikubwa we dont have guided development na kwa kuwa tuko confused si wajamaa si mabepari hata direction hatuwezi kuwa nayo. Matin --- On Mon, 21/1/13, Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk> wrote:
|
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment