Sunday 20 January 2013

Re: [wanabidii] Re: MAANDAMANO MAKUBWA MTWARA - 19.01.2013

Huu i mwanzo tu lakini yapo maeneo mengi ambayo yanashughuli za aina hii
zinazowachanganya wananchi, mfano: madini yanayochimbwa hapa nchini
yanaenda ku processiwa wapi, na je kama huko kuchakatwa kungefanyika
hapa nchini vijana wetu wasingepata ajira? viongozi wetu wabadilike kwani kama
ni kuwavumilia tumewavumilia vya kutosha na tayari tunaanza kuamka.

From: heri rashid <herirashid@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Saturday, January 19, 2013 2:28 PM
Subject: Re: [wanabidii] Re: MAANDAMANO MAKUBWA MTWARA - 19.01.2013

Kwa maoni yangu, Suala la gas Mtwara huenda hatujalifahamu! Inasafirishwa kwenda Dar kwa ajili ya nini? na kwanini Dar na si sehemu nyingine? Kwani hakuna njia nyingine ya kusafirisha hadi tutumie mabomba? Bandari ya Mtwara itapanuliwaje wakati rasilimali kama hizi zingetumika kuipanua. Tusishabikie maneno ya wanasiasa waliofisika kimawazo na wanaoona kila kitu kiwe Dar.
 
Mawazo yangu Mitambo ya kusafisha ijengwe palepale Mtwara, gas itoke pale ikiwa tayari kwa matumizi sio crude ikasafishe Dar. kwa kufanya hivyo tunafanya maeneo mengine kuendelea na mengine kubaki gizani. Hii ni fursa ya kufungua maeneo ya kusini ambayo kwa mda mrefu yamesahaulika.
 
Tusitishiane kuwa wawekezaji watakimbia, watakaokimbia hawako serious na uwekezaji.

--- On Sat, 1/19/13, nchunguye festo <nchunguye1971@yahoo.com> wrote:

From: nchunguye festo <nchunguye1971@yahoo.com>
Subject: Re: [wanabidii] Re: MAANDAMANO MAKUBWA MTWARA - 19.01.2013
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, January 19, 2013, 3:07 AM

Yona kwa nadharia nakukubali. Hili haliwezekani ndani ya mfumo na utawala tulio nao. UTOPIA at its best

From: Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>
To: Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Saturday, January 19, 2013 1:57 PM
Subject: [wanabidii] Re: MAANDAMANO MAKUBWA MTWARA - 19.01.2013

Waachiwe waandamane ni haki yao ya msingi kuandamana na kusema mawazo
yao wako huru kabisa .

Uhuru wao unaishia pale wanapoanza ubinafsi wa kwanza hiki ni chetu
sio cha watanzania , watanzania wengine hawaruhusiwi kunufaika na hivi
na vile hiyo sio sahihi .
Lazima watambue maeneo ya kusini yanafaidika zaidi na mradi wa gesi na
mafuta kwa kipindi kirefu kijacho nitatoa mfano kidogo chini .

Bandari zao zitapanuliwa na kuwa kubwa kwa ajili ya biashara hii ya
mafuta na gesi , wataweza kuuza sio dsm tu maeneo mengine ya nchi na
nchi jirani haswa kusini mwa nchi kama Malawi , Zambia , msumbiji .

Kuna hoteli n huduma nyingine mbalimbali zitajengwa na zimeanza
kujengwa kutokana na sekta hii ya mafuta maeneo ya kusini kwa ajili ya
wafanyakazi na wadau wengine wa biashara maeneo hayo .

Vyuo vya ufindi na mashule yatajengwa kutokana na vipato vinavyotokana
na sekta hii kwa ajili ya kuandaa wafanyakazi wa sekta hii na nyingine
zinazofanana kwa kipindi kirefu .

Sasa wananchi wakianza maandamano sasa hivi na virugu wajue fursa
nyingi watapoteza , wawekezaji wanaotoa mitaji yao kwa ajili ya ujenzi
na miundombinu ya mafuta na mengine wanapenda kuhakikishiwa usalama
wao na wa mali zao kwanza ndio mengine yaendelee .

Waangalie wasije wakakosa vyote , wasipoangalia itakuwa kama north
mara na maeneo mengine ya migodi kwenye vurugu ambapo makampuni
yanaweka mageti makubwa walinzi na silaha wao utawaona kwenye ndege
kutoka na kuingia tu .

On Jan 19, 1:41 pm, Sylvanus Kessy <frke...@yahoo.com> wrote:
> Ndugu wanabidii
> Mzimu wa Gas unaendelea kuitafuna nchi, ukianzia huku Mtwara. Leo wananchi wamehamasishana Wilaya zote, za Lindi na Mtwara ili kupinga GAS ISITOKE  Mtwara.
>
> Hakika Elimu na makubaliano yanahitajika. Viongozi wanaohusika watafute Hekima ya hali ya juu kutatua tatizo hili. Tukiendelea kusema ni wahuni watafanya mambo ya kihuni na tutapata hasara kubwa zaidi!
> sylvanus

--
Jobs in Africa - http://www.wejobs.blogspot.com/
International Jobs - http://www.jobsunited.blogspot.com/

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
0 comments:

Post a Comment