Thursday 24 January 2013

Re: [wanabidii] NDOA YA KAKA YANGU,MREJESHO; VITA YAHAMIA KWA MTOTO


To be honest kama kuna mpenda dini ataona nimekosea katika mawazo yangu anisamehe.

Yona,
Hii kitu ya kushikilia dini wakati mtu anaendelea kupata taabu kufikia kushindwa just to own a peace of mind ni ujinga. Angekuwqa ni mwanamke anabondwa ndani mngeenda kupekua vitabu vya dini ati wasiachane!! kama mwanamke ameamua kuondoka acha aende!! dunia imebadilika na hao wanawake wamebadilika, Ni wangapi wako tayari kuvumilia ugumba wa wenza wao kama wenzetu wa zamani, tuende na nyakati ndugu yangu, hiki ni kizazi cha "warap" dunia ya leo kila mtu anafikiria maslahi yake na sio kama zamani walifikiria kujenga pamoja kila kitu na kiwe chao wote.

Napongeza uamuzi wa huyo bwana. japo mtoto anahitaji malezi ya pande zote mbili ila nina uhakika kwa style ya huyo mama hakuna malezi yanayofaa tena kutoka upande wake. Mwanamke hajaridhika na hiyo ndoa and she want something more!! utamlazimishaje jamaa aendelee kumkumbatia?

Hii sheria ya mtoto kuchukuliwa na baba akiwa na miaka 7 nadhani haitutoshi wote, ingewekwa hivyo kwa mtu asiye na uwezo wa kumtunza mwanae ipasavyo (mahakama ikiridhia) ila kama una uwezo wa kumlea mwanao its better upewe japo kuwe na kikwazo cha miaka 2 angalau.

Unaweza kumlazimisha punda kwenda kisimani lakini si kunywa maji. Huyo kaka yako aanze maisha yake upya na asiangalie nyuma. nothing can shape his life more than yeye mwenyewe, wengine ni watazamaji tu.

--
"Anyone who conducts an argument by appealing to authority is not using his intelligence; he is just using his memory." Leonardo daa Vinci

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment