Wednesday 23 January 2013

Re: [wanabidii] NDOA YA KAKA YANGU,MREJESHO; VITA YAHAMIA KWA MTOTO

Kuvunja ndoa ni kosa kubwa ambalo hautasameheka ndugu yangu tena ukiwa kwenye ile hali ya wewe mwenyewe kama kichwa cha nyumba na familia kukubaliana na uvunjaji wa ndoa .

Biblia inasema hivi kuhusu mwanaume katika ndoa
"Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo; naye ni mwokozi wa mwilli" Efeso 5:3
"Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa; na mtu aitawalaye roho yake kuliko mtu atekaye mji" Mith 16:32

Katika Ndoa Biblia inasema
"Msitende neno lolote, kwa kushindana wala kwa majivuno, bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake" Wafilipi 2: 3

Mume mwenye mamlaka na uongozi wa kweli atamtia moyo mkewe na kukuza vipaji na talanta zake hata shughuli za kiuchuni zitaendelea. Kama mume waweza mara nyingine ukawa mtu wa kumlaumu mkeo kuwa amekosa sifa za mwanamke wa mithali 31

Sasa acheni hasira na utoto kaeni tena muongee muone jinsi ya kumaliza tofauti zenu muende mbali zaidi .

2013/1/23 Joseph Ludovick <josephludovick@gmail.com>
NDOA YA KAKA YANGU;MREJESHO;VITA YAHAMIA KWA MTOTO

Ndugu,baadhi mtakumbuka niliomba ushauri hapa juu ya matatizo ya kaka yangu na mkewe.wapo waliochangia hapahapa,na wapo waliochangia kwa inbox.wapo wachache waliohoji busara ya swala kubwa kama hilo kuletwa mtandaoni.ndugu,huu ni mtandao wa kijamii,japo watu huutumia kwa sehemu kubwa kujiburudisha tu,wapo wanaoweza kusaidiana kijamii kwa kujifunza na kupeana ushauri wa maana.huu ndiyo uelewa na imani yangu.kwa hiyo nitaendelea kuitumia mitandao ya kijamii kama moja ya nguzo muhimu ya kupashana habari.na kwa kweli yapo maendeleo juu ya story ya awali ambayo pia tunahitaji baadhi ya maoni kabla hatujashauri kaka afanye nini.
Mke wake na kaka alimpeleka mtoto wao mdogo kwa bibi yake upande wa mke bila mashauriano,ruhusa,wala makubaliano na kaka.mtoto ana mwaka mmoja sasa.ameachishwa kunyonya katika umri huo.sababu ya kufanya hivyo zinatolewa tofauti na zenye kujichanganya.kwanza shemeji alimwambia kaka taarifa juu ya kumpeleka mtoto asubuhi ya siku aliyomsafirisha.akitoa sababu kuwa house girl wao ameuguliwa na mama yake so asafiri na mtoto.kisha mtoto akabaki huko.ndipo baadaye zikasikika kashfa kuwa ameamua kumpeleka mtoto kwa bibi yake kwa kuwa hawana fedha hata ya kumlisha mtoto.kwa hiyo ameona mtoto atapata taabu.lakini ukiacha mbali kuwa huu ni uongo,yeye mwenyewe shemeji ni mfanyakazi akilipwa zaidi ya laki 6 kwa mwezi.hata kama mume wake hana hela kabisa ,je hata yeye ameshindwa kumlisha mwanaye?
Wakati mwingine akiulizwa anasema amekuwa na msongo wa mawazo kutokana na kutoelewana na kaka hivyo anashindwa kunyonyesha mtoto.lakini habari za baadaye ni kuwa shemeji ameshaomba na kupata scholarship nje ya nchi na anajiandaa kwenda huko.kwanza mipango yote ya aplication alifanya kwa siri bila mume wake kujua,pili masomo haya yatachukua miaka 2 au zaidi.inawezekanaje mke akafanya mipango na maamuzi ya jambo kubwa hivi bila mume wake kujua ,kushirikishwa,kuruhusu? lakini ndilo lililotokea.kumbe kumpeleka mtoto ilikuwa maandalizi haya.mengine yote ilikuwa gerasha tu.
sasa baada ya majadiliano mengi katika ngazi ya familia,kaka anashikilia sasa msimamo kuwa NDOA yao ivunjike,na watengane.yuko tayari kutoa TALAKA,na anasema haoni uwezekano wowote wala maana ya kuendelea na mke anayemdharau,kumvunjia heshima,asiyeweza kumstahi,na mwenye kuthamini wanaume wa nje kuliko yeye mume wake.kaka anasubiri tu vikao vya kifamilia.

VITA YA MTOTO.
nimeiita vita kutokana na kaka mwenyewe kuiita hivyo.kisha kutengana kaka anataka sasa mtoto arudishwe kwa namna yoyote ile.yule ni mtoto wake na wala hatapangiwa namna ya kulea mtoto wake na wakwe,wala mtoto wake hatalelewa kwa bibi.kaka anasema anataka kulea mtoto wake.tumemweleza juu ya sheria inayotaka mtoto akae na mama hadi akiwa mzima kiasi nadhani miaka 7,ameikataa hoja hii na kusema mtoto hakai na mama yake hata sasa.kwa hiyo hoja hiyo haina mashiko,na kama lazima atakwenda kulelewa kwa bibi upande wa baba.hapa kaka anasema anasubiri kuona wakwe wakiingilia namna yeye anavyopaswa kulea mtoto wake.
lakini pia kaka anasema ameshapata chumba,na anajiandaa kutengeneza mazingira kupata mfanyakazi wa kulea mwanaye na ataishi na mwanaye akilelewa na msaidizi wa ndani.mama yake hana uhitaji wa kukaa naye ndo maana alimpeleka mbali,na vilevile hata wakisema eti mtoto akae na mama,mama yupi wakati mama huyu anakwenda masomoni.
Tumemuuliza kuwa vipi kama mke wake akisema anaachana na mpango wa masomo ili alee mtoto,kaka akasema hiyo haiwezi kuwa point kwani itakuwa ni mashinikizo tu na anasema uamuzi wake ni huu katika mazingira yoyote ya baadaye.na ndiyo maana anaiita vita.
Ndugu naomba maoni yenu juu ya swala hili.mambo ya kusema wayamalize au waendelee,limeshapita,tafadhali tujielekeze kwenye hoja ya mtoto.nawashukuru sana kwa mawazo

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 



--
www.wejobs.blogspot.com Jobs in Africa
www.jobsunited.blogspot.com International Job Opportunities

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment