Friday 18 January 2013

Re: [wanabidii] Natamani kuwa mwanasiasa


Miradi ya vijana funded by the Foundation of Civil Society ya Tanzania nao ilianza vizuri na mafunzo ya Life skills-wajitambue. Kisha ya capacity building kuhusisha wataalamu wa sekta mbali mbali-kilimo, ufugaji wa mbuzi wa maziwa, kuku wa kienyeji kwa mayai, nguruwe, ng'ombe kisasa, SACCOS ili wajiunge nazo kufungua accounts huko etc. Baada ya mafunzo waliowengi wameingia katika bajaji na pikipiki, mashamba ya kilimo waliyopewa na vijiji-wameyatupilia mbali hawana time. nani alime bustani au mazao aingie tope. Kila mmoja anataka easy-come-easy go. Kuku zimepangaranyika, nguruwe aliyebaki nazo kupokezana uzao kumekwisha za pamoja zimeuzwa. nani aamke kulisha kuku na mifugo mingine. Ukiangalia kinachoendelea kila inapokuja NGO ingine-walewale wanajitokeza na kulalama hawana ajira na cha kufanya. wanapata mafunzo tena. Muda wa mafunzo na posho ukiisha-wanarudi kijiweni. Repeated training, re-inventing the wheel hakuna kinachoendelea kulalama tu vijana hatusaidiwi, bhangi mdomoni, kula kwa mama ntilie. Lakini eneo lina mabonde mazuri ya kilimo walimao ni wazee. Maeneo mengine kuna hata irrigation system-hawataki kilimo ila hawana ajira ndio tatizo kuu.

Mbona Butiama kuna maeneo mazuri ya Kilimo na mpaka Bwawa Marehemu Baba wa taifa alisaidia likajengwa hapoo na wanaogelea. Bonde la Ruvu, Kilombero, Ruaha etc. Ila vijana tupo kuiba mazao shamba, kupakia ktk fuso na kuuza mijini. Kama kilimo si muhimu, unaibaje mazao ya vizee ukauze. Hii haimaanishi hakuna vijana hata mmoja ajitumao-wapo kama Iringa Ilula wamelima na kuuza nyana na kutajirika sana. Waha kwa sasa wanapeta. Wamevunja mawe kunduchi DSM na sasa  waliowengi wamefungua maduka, bar, magenge, wamejenga majumba. Wale waliowakuta wakipasua mawe toka zamani wapo pale pale na bhangi. kazi kuvamia mashamba ya watu kuuza, kuvuta bhangi, kuvamia-kuuza eti hawana ajira na viwanja vya makazi. Lakini wanapovamia, huweka kibanda cha nyasi na kuuza eneo kwa malaki na kuvamia kwingine kusababisha conflicts.
Kutokuona kibanzi chako machoni jinsi gani unajiharibia maisha, kutokuwa na mipango ya maisha, externalization of errors (huwajibiki na hali yako ilivyo, kuwa wewe binafsi sio sababu bali mtu mwingine ndio sababu ya hali yako) ni kibanzi kikubwa cha wabongoland.

Wengine-vijana wanaweza wakaanzisha kitu kisiendelee kwani wakitegemea kitawafanya wapate donors zaidi. Hela ikija fanyekaujanja akanunue pikipiki. Kumbe ni wao wakilee, kizalishe (nyanya, mahindi, ufuta, mbuzi etc) kiwe endelevu sio donors walete hela halafu wagombanie uongozi waibiane waparaganyike.

Kutaka SIFA kwa kulaumu tu bila utendaji wenye output na outcome ni tatizo hata la viongozi huko chini. Kuanzisha vipya kila mara bila kuangalia na kujipima tulikotoka na kujifunza na hayo ya nyuma (hatujifunzi kutokana na makosa tukajirekebisha) ni tatizo la Kitaifa. Kunatuyumbisha sana ndani ya familia pia. Ndani ya familia, kama zuzu, unafikiria umasikini wako utaisha kwa kuoa wake wengi au kuwa na mifugo mingi bila ya kuangalia ubora wa maisha yako, uwezo wako kifedha au kiardhi-carrying capacity na ulinzi wa mazingira na maisha yako (hata HIV ktk ndoa ya wengi). Ni hao wa uza nyumba kariakoo kwa bilioni kadhaa, oa wake, ingia mabondeni jenga ije bobolewa na city. Vuna dhahabu-ongeza mifugo, lima Magu mpunga safirisha peleka ZNZ na kenya; ongeza mifugo, hamisha  baadhi ya familia ikachunge Kilombero Ramsar site, fukuzwa-hamahama, watoto hawasomi, poteza mifugo, pigana na polisi, swekwa jela, tesa familia. Ungefuga na kulima endelevu pale ulipo-ungeokoa muda na mali na watoto kusoma. Hii haipambi ubongoni kwa wabongo. Na mwanasiasa atataka SIFA sio kutetea sustainable land use bali waruhusiwe kuzagaa-karne hii hadi Namtumbo kwenye big 5 za kilimo wakalishie mazao mifugo? SIFA ya GAS ya Mtwara-sasa ndio KURA zilipo-kazi imeanza. Aluta contunua!!

Mpaka wanasiasa tutakapotaka kubadilika na kubadilisha watu wetu makwetu ndio maendeleo yatakapopatikana. Tuwe kama USA tunapogombania nafasi, tukipata-kazi ni moja sio kuwekeana vikwazo-kuonyesha mfano bora wa utendaji na Vijiji tuishipo majimbo yetu kuwa mfano. Vijiji na majimbo yetu raslimali tele hayawi mfano-lawama za nini?

--- On Fri, 18/1/13, john mahaba <mahabajo@yahoo.com> wrote:

From: john mahaba <mahabajo@yahoo.com>
Subject: Re: [wanabidii] Natamani kuwa mwanasiasa
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Friday, 18 January, 2013, 8:12

Dada Hilda kwanza nikupongeze kwa hoja zako nyingi unazochangia ndani ya hili jukwaa
kwani kama ni elimu tunaipata vilivyo. binafsi huwa naguswa na mambo mbali mbali yaihusuyo jamii
na hasa ya eneo ninalotokea (Butiama) mwishoni mwa mwaka jana nilibahatika
kuwa na jamaa zangu kijijini, na nilifanikiwa kukaa na vijana wenye umri wa miaka
18 hadi 25, wakati wa mazungumzo yetu wengi wao waliitolea lawama serikali kwa kushindwa
kuwa na mipango madhubuti ya kuwaondoa kwenye umasikini. Baaada ya mazungumzo hayo
nilijaribu kuwaomba kila mmoja anipe mpango anaotaka kuutekeleza kama hiyo serikali ikiamua
kumwezesha, kati ya vijana 12 niliokuwa nao hakuna hata mmoja aliyekuwa na hata kitu wazo
lakini ndo hawa hw wanaoilaumu serikali kwa kutofanya chochote, nashukuru baada ya mazungumzo
yetu na wao na baada ya kuwapitisha kwenye mchakato mdogo wa kuwa na vipaumbele
vyao kimaisha leo hii baadhi wamenipigia simu na kuniambia wameanzisha mradi wa kulima
mihogo na viazi ambavyo baada ya miezi 4 wengi watajifunza kutoka kwao.
NAOMBA TUWATIE MIOYO WALIOCHANGANYIKIWA NA UGONJWA WA KISIASA.



--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment