Thursday 17 January 2013

Re: [wanabidii] Natamani kuwa mwanasiasa

Hilde hilo la mwisho ndio linanipa mashaka na mustakabali wa nchi hii, maana inabidi kuhonga ili baadaye ukawafanyie watu hao hao kazi!! Wanasiasa wakongwe wameiharibu nchi hii kwa hongo. Vyama vipya vya siasa vimejaza mamluki wanaotafuta pesa na sio kuiendeleza nji hii. Wakipewa vijisenti kidogo utawasikia wanahama chama hiki kwenda kile na kuanza matuuusi!
Ushauri wako wa maendeleo ya bottom-up ni mzuri sana na ndio tulioujaribu katika mipango ya ASDP lakini sijaona kama wananachi wana-address real issues. Matokeo yako wanaishia kuongozwa na wataalam ambao nao wanapendelea taaluma walizosomea au kuweka miradi yenye ulaji kwao

2013/1/18 Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
Ingefaa vile vile, baada ya uchaguzi wa wabunge na madiwani-serikali itumie wizara husika kuunda timu mchanganyiko wa wataalamu kutoa mafunzo concentrated ya muda mfupi kwa wachaguliwa. Mafunzo yawafunue kuwaelekeza mfumo wa nchi-utawala upoje, majukumu yao na iwaelekeze jinsi ya kuhamasisha maendeleo bottom-up; jinsi ya kupanga mpango kazi, kuutelekeza na kuutolea taarifa zake.

Halafu, iwapime utendaji wao wachaguliwa kama wao waipimavyo GVT na watumishi wengine wa umma ambao kila mwaka form maalum za maendeleo kazini.

Ninasema hivi kutokana na evidence kwamba-unaweza ukafika kijijini kuwe kwa CCM, Chadema, CUF, TLP etc ukaona kuna kila kitu hapo lakini watu wapo na umasikini-wamebweteka. Utasikia tu kutoka watu hao-serikali ilete hiki, serikali itupe hiki na kile.

Mijini serikali ituondolee uchafu huu (atupao yeyeye mtaroni) na maji machafu haya-anayotiririsha yeye lakini pale pana sewer pipe. Mwanasiasa kubweteka na uchafu huu unakuona lakini huhamasishi watu wako kufanya itakiwavyo ktk wajibu wao na wa afya yao. Hata kutokomeza ukeketaji kwa mfano-unangojea serikali kuu sio wewe kuongea na watu wako. Kama wangejituma kwa kuhamasishwa na huyo mwanasiasa wao wangezalisha ya kutosha kula (hata kama wasiuze) lakini wana chakula tosha ndani hawafi njaa. Lakini pamoja na resources zote hata chakula hawana na mvua imenyesha vizuri.Wengine eneo lao ni la zao la mtama na mihogo lakini wanalima wrongo crop-mahindi ekari na ekari na kila mwaka yanakauka wanakosa chakula. Wangelima mtama, mihogo, ufuta kama ilivyokuwa zamani-wangepata, wakauza wakanunua mahindi.
Lakini kiongozi yupo anaona haya hawashauri nao wabishi hawamsikilizi hata bwana shamba.

Ukitaka kuionyesha CCM haifai au chama kingine chochote hovyo-onyesha mfano kwako through community mobilization. Wakusikie, watumie kinyesi cha mifugo walionayo wawekeshe mbolea shambani; walime na kufuga kisasa, maji na udongo, miti, nyasi vipo bure kwa nini nyumba iwe wazi umchungulie huko kijijini? Kwa nini aweke paa bila kufunga vizuri nyumba ziezuriwe. Kwa nini asipande miti ya kivuri karne na akiokota mbegu kumwaka na kuuzungushia mche mdogo miba utakua na kudumu. Usirane na gari ingia toka tu nawe uwe na shamba na mifugo ya mfano waite waje kuona. waelekeze kwa lugha ya kwenu waone kulinda haki na utu ni muhimu ili tuache kukatana viungo, kuchomeana nyumba kwa Imani za kishirikina au kufanyiana mipango ya kuibiana mifugo na vita visivyoisha. Maana tunafanyiana wenyewe kea wenyewe. Hivyo ni sisi wa kuacha vitendo viovu tunafanyo-mioyo mibaya ya tamaa na visasi. tukubali kubadilika. Tukiweka tamaa, tutakuwa pale pale daima.

Tukiweka visasi-ndio kabisa hatufiki mbali na wala hayatatuliki mpaka dunia iundwe upya. Bora usiwe mwanasiasa maana ni lawama.Pia inabidi uwe na hela za kuhonga ili uchaguliwe ama sivyo-itakuwa kwako muda utakaopoteza na vijisenti vyako finyu vitaliwa na wananchi wako na wasikuchakue.

--- On Fri, 18/1/13, Victor Mwita <victormwita@gmail.com> wrote:

From: Victor Mwita <victormwita@gmail.com>
Subject: [wanabidii] Natamani kuwa mwanasiasa
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Friday, 18 January, 2013, 5:42


Ndugu wadau
Kwa muda mrefu nimetamani kuwa mwanasiasa nikiwa na lengo la kuwawakilisha wananchi wenzangu mjengoni na katika fursa mbalimbali ndani na nje ya nchi. Ni kweli kwamba huko nilikozaliwa kuna matatizo ya msingi ambayo kwa miaka mingi hayajawahi kutatuliwa. Tatizo kubwa ni siasa na vyama vyake katika nchi hii. Ili kutumiza azma yako inabidi ku-sacrifice sana muda, rasilimali (fedha) na utu wako kwa chama chako but hayo yote hayakuhakikishii kuendelea kubaki katika chama. Wakati wa kutafuta ticket ya chama ili uwe mgombea wa nafasi yoyote kuna mizengwe kibao!! Kubwa mno ni hii tabia ya watanzania kutaka uwape kitu kwanza ili ukawawakilishe!
Kwenye vyama nako kumejaa watu wa kila aina. Mwanzoni nilidhani vijana wanaoingia katika siasa wako serious kutaka kuleta maendeleo katika nchi hii, kumbe wanatafuta ajira na fedha. Ndio maana wananunulika na wanasiasa wazee na kuishia kujaribu kuharibu sifa za vyama vyao.
Mambo haya yananifanya nianze kupata wasi wasi na mustakabali wa siasa za nchi yetu. Najiuliza maswali kadhaa yasiyo na majibu. Kubwa zaidi ni hili na wananchi kuhitaji kitu kidogo kutoka kwa wagombea kabla ya kuwachagua. Je waliochaghuliwa watakuwa wanawawakilisha hao wapiga kura waliohongwa au wanaenda kutimiza matakwa yao? Labda ndio maana wawakilishi wetu wakishafika mjengoni wanafanya kila wawezalo kujiongezea posho na mishahara mikubwa ili kupata mitaji wa kwenda tena kununua kura next elections. Tumeona wawakilishi huko Kenya walijiandalia pension ya nguvu. Na ninaamini hata hapa kwetu hilo linakuja.
Vijana amkeni msimamie hatma ya nchi yetu. Kumbukeni the country is bigger than the individual. Msitumike kuvuruga vyama vyenu kwa faida yetu sisi ambao miaka yetu inaelekea mwisho lakini bado tuna uroho wa madaraka. Fikiria iweje wewe kijana mzee akupe vijisenti kidogo ili akutumie kuharibu carrier yako yote katika siasa?! Just say no and stay focused.
Bado najiuliza kama niingie katika siasa za huko kwetu na niingie kwa style gani
--
Victor Caleb Mwita
P.O. Box 9152
Dar Es Salaam

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 



--
Victor Caleb Mwita
Ministry of Livestock and Fisheries Development
P.O. Box 9152
Dar Es Salaam
Tel: 0766750673, 0789142275

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment