Saturday 12 January 2013

Re: [wanabidii] MWANGOSI NA DR ULIMBOKA WAMUWEKA PABAYA JK

Duh! Ama Kweli sikio la kufa...... Anayejibizana na mtu wa kaliba hii anahitaji kutambua anafanya hivyo na mtu wa aina gani na pia naye ajitambue iwapo hana shughuli nyingine muhimu ya kufanya.

Sent from my iPhone

On 12 Jan 2013, at 20:36, Yona Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:

Ndugu Isango

Wengine tunajua mengi kuliko hizi Propaganda unazipiga zizizokuwa na kichwa wala miguu hata hiyo taarifa imebeba upande mmoja , kuna wakati CUF nao walikuwa na malalamiko kama hayo wakaweka picha za upande wao pekee sasa hivi jiulize CUF wako wapi mbona hawaonyeshi upande wa pili ?

Kwenye picha moja nimeona picha ya Mchumba wake SLAA kule Arusha lakini hawajaandika ilikuwaje mpaka ikamtokea hivyo , ukifuatilia utajua kwamba alivunja sheria hakutii sheria fulani ikatumika nguvu akaumizwa tena huyu ni mtu wa karibu na katibu mkuu wa chama chenu tulitegemea awe mfano wa kuigwa katika kufuata sheria na taratibu za nchi . Katika tukio hilo Dr slaa alinukuliwa na chombo fulani cha habari cha kimataifa akiapa kwamba lolote litakalotokea asilaumiwe .

Kule singida ambapo wewe ni kiongozi baadhi ya viongozi wa chadema wamefunguliwa kesi kwa kuhusishwa na kifo cha kada wa UVCCM , sasa nendeni kwa hao mabwana zetu kawaambieni kuna viongozi wenu wanekesi ya kujibu .

Kule Iringa kwa mwangosi waambieni mabwana zenu kuna watu wanachunguzwa sasa hivi na mmoja wao ni kiongozi mmoja wa NGO ya watoto ambaye mwaka 2015 atagombea ubunge .

Tunajua kwamba mwaka 2010 hao mabwana zenu waliingiza mamluki waliofundishwa huko nje kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali za Ubunge na udiwani baadhi wamepata kwa vyama vya upinzani waambieni tunawajua waendelee kukaa na kufanyia hujuma zao huko huko linapokuja suala la nchi wamepigiwa msitari .

Tunajua baadhi yenu mmepewa mafunzo haswa nchi ya Ujerumani na mataifa mengine kwa ajili ya kazi maalumu nikitaja hapa hamtakatiza mtaa .

Nimalizie hapa .

NASEMA KWA MSISITIZO KWAMBA HAO MABWANA ZENU SI LOLOTE WALA CHOCHOTE TUMEWACHOREA MSITARI , TUKO IMARA NA HATUTISHIKI MICHEZO WALIYOIFANYA MIAKA YA 70 NA MWANZONI MWA 20 WASIIRUDIE TENA .

TUMEWACHOREA MSITARI .

2013/1/12 Josephat Isango <joseisango@yahoo.com>
Haya ndio mambo ambayo tumesema mapema hatuyataki. Lakini na wewe HK badala ya kujibu hoja umekuja na hoja ya Umri wetu na suala la siasa. Tunajadili suala la mauaji ya watanzania. Nimelazimika kwenda kwenye website kuangalia Umri wako nikakuta hata wewe kwa umri ni mdogo kwangu. Sasa kwa kigezo hizo tu, nakushauri mimi kama mkubwa niliyekutangulia kuzaliwa. Jadili hoja, ili unyeshe mfano, huo mchango uliochangia umeeingia kule kule kwa yule tuliyemkataa. Hapa unachangia mawazo bila kujali umri wa watu. Tunahitaji uelewa. Sasa wewe unataka kuchangia humu tuwe tunaulizana umri? Mbona wakati wa kujiunga hatuulizani umri. tujikite kwenye hoja, Suala la Mauaji ya kikatili linalofanywa na polisi sehemu mbalimbali, suala la Dr. Ulimboka ambaye hata wewe uliwahi kuliunga mkono, suala la Wanaharakati kushtaki katika seneti ya Marekani, suala la Wizi wa Wanyama hai............... hayo ndo yalikuwa katika mjadala. Kama nimekurudisha katika mstari, usitoke tena changia mawazo.

--- On Sat, 1/12/13, hkigwangalla@gmail.com <hkigwangalla@gmail.com> wrote:

From: hkigwangalla@gmail.com <hkigwangalla@gmail.com>

Subject: Re: [wanabidii] MWANGOSI NA DR ULIMBOKA WAMUWEKA PABAYA JK
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Saturday, January 12, 2013, 8:52 AM

Mijadalaa hapa inakuwa too low kwa sababu limeingia kundi la watoto wa shule wanaojifunza siasa basi hawana hoja bali wanajadili majina ya watu tu! Sasa mjadala umekuwa Dr Kafumu na Ph.D yake na dhihaka kede kede!
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

Date: Sat, 12 Jan 2013 15:42:30 +0000
Subject: Re: [wanabidii] MWANGOSI NA DR ULIMBOKA WAMUWEKA PABAYA JK

Isango mbona haumkumbushi maoud mbwana aliyekufa kwenye uchaguzi wa damu kule igunga yeye akapa ubunge.hawajasaulika.subirini tume ya kimahakama?mtakwisha
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

From: Josephat Isango <joseisango@yahoo.com>
Date: Sat, 12 Jan 2013 03:58:36 -0800 (PST)
Subject: Re: [wanabidii] MWANGOSI NA DR ULIMBOKA WAMUWEKA PABAYA JK

Dr. Peter D. Kafumu, ni huyu Daktari aliyekuwa Mbunge wa Igunga au mtu katumia jina lake? Kama ni huyo mbona kama Udaktari ni cheo ninachokiheshimu kwa kuwa wana elimu sasa imekuwaje huyu akateleza kuandika hiki? Yangeandikwa yote hadi mauaji ya Tarime, Mauaji ya Albino, Mauaji yaliyotokea Zanzibar, au hata ukatili unaofanywa kwa wanchi kunyang'anywa ardhi ripoti hiyo mbona ingejaa Maktaba, hapa kuna mambo mengi yameachwa, likiwemo la Kijana wa Arumeru, mauaji ya Polisi kufanywa na wananchi haya yote kwa watetezi wa haki za binadamu hayakubaliki. Dr. Nakuheshimu usilete siasa kwenye uhai wa binadamu, ukianza kuleta siasa kwenye uhai wa binadamu utasababisha watu wasio wa Chama chako wauawe kwa kuwa hawakuungi mkono. Ulikuwa Kiongozi, kumbe wananchi walikosea kukuamini kama ulikuwa na fikra za hivi. Heri Mahakama isikurudishe.

--- On Sat, 1/12/13, Dr Peter D Kafumu <kafumu@yahoo.com> wrote:

From: Dr Peter D Kafumu <kafumu@yahoo.com>
Subject: Re: [wanabidii] MWANGOSI NA DR ULIMBOKA WAMUWEKA PABAYA JK
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Saturday, January 12, 2013, 3:40 AM

Hivi wale vijana aaliokufa morogoro na kule singida mbona wao hawatambuliki kuwa ni wahanga wa siasa hizi chafu za kiamgharibi za vyama vingi?

--- On Sat, 1/12/13, Mohamedi Mtoi <mouddymtoi@gmail.com> wrote:

From: Mohamedi Mtoi <mouddymtoi@gmail.com>
Subject: [wanabidii] MWANGOSI NA DR ULIMBOKA WAMUWEKA PABAYA JK
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Saturday, January 12, 2013, 8:44 AM

KUUAWA kikatili kwa mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daudi Mwangosi na tukio la kutekwa, kuteswa kwa kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka, limechukua sura mpya ambapo sasa limetinga katika Seneti ya Marekani, Tanzania Daima Jumamosi limeelezwa.

Taarifa kutoka Washington nchini Marekani zinasema Rais Jakaya Kikwete amelalamikiwa rasmi katika Seneti na wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu nchini, na kwamba masuala hayo sasa yatafikishwa kwenye Shirika la Umoja wa Mataifa la Kutetea Haki za Binadamu (UNHRC) kwa hatua zaidi.

Mbali na mauaji ya Mwangosi na tukio la Dk. Ulimboka, Rais Kikwete pia amelalamikiwa kwa kufumbia macho matukio mengi ya kuteswa na kuuawa kwa raia pamoja na kufungiwa kwa gazeti la kila wiki la uchunguzi la MwanaHalisi, kutoroshwa wanyama hai kwa kupelekwa nje ya nchi na hatua ya polisi kutumia silaha za kivita kupambana na raia wasio na silaha wakiwemo wanafunzi wanaoandamana.

Ripoti hiyo ya wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu yenye kurasa 27, inatuhumu utawala wa Rais Kikwete kwa kukandamiza demokrasia kwa kutumia polisi na vyombo vingine vya dola.

Watetezi hao wa haki za binadamu, wamedai kuwa baada ya kufanikiwa kuingiza masuala haya ya ukiukwaji wa haki za binadamu katika Seneti ya Marekani, sasa wanafanya kila liwezekanalo kuhakikisha suala hili linafikishwa Umoja wa Mataifa kwa kile walichokiita, kuiadabisha serikali.

Kwa mujibu wa nyaraka zilizopatikana, na pia kusambazwa katika baadhi ya taasisi za habari, suala hilo liko mikononi mwa Seneta Kerry, ambaye baada ya majadiliano katika Seneti, ripoti hiyo itapelekwa UNHRC.

Habari zinasema baadhi ya wajumbe wa Seneti waliofanikiwa kuona ripoti hiyo wamemeshitushwa na kile walichokishuhudia katika picha zilizoambatanishwa.

Aidha, ripoti hiyo pia imeeleza jinsi rushwa ilivyoshamiri nchini, ukandamizaji juu ya uhuru wa maoni na matumizi mabaya ya vyombo vya dola kudhibiti vyama vya upinzani na kutumia silaha za kivita kupambana na raia wasio na silaha.

Ripoti hiyo ya kuishitaki Serikali ya Kikwete, pia imelaani vitendo vya polisi kusambaratisha maandamano ya wanafunzi wa shule za msingi jijini Dar es Salaam, walioandamana Julai 31, mwaka jana kupinga ukosefu wa walimu nchini.

Mgomo wa wanafunzi ulikuja baada ya walimu wa shule za msingi na sekondari kupitia jumuiya yao - Chama cha Walimu Tanzania (CWT) – kuitisha mgomo nchi nzima wa kutaka kuboreshwa kwa mazingira ya kazi zao, nyongeza ya mishahara na malimbikizo ya posho.

Nyaraka zilizowasilishwa na wanaharakati hao, zimeambatanishwa na picha zinazoonesha namna Jeshi la Polisi lilivyohusika kuuawa kwa Mwangosi, picha mbaya ya maiti ya mwanahabari huyo, na namna Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamhanda alivyokuwa akishuhudia askari wake wakimsulubu mwanahabari huyo kabla ya kufunga kazi kwa kumaliza uhai wake.

Kadhalika, kumeambatanishwa picha zinazoonesha maiti za watu waliouawa wakati wa maandamano huko Arusha, na ile inayosadikiwa kutokea kule Songea. Picha nyingine za kusikitisha ni zile zinazoonesha askari zaidi ya watano wakimdhibiti mwanaharakati mmoja katika maandamano, na umati wa wanafunzi wa shule za msingi wakiandamana, huku nyingine zikionesha askari mwenye silaha ya kivita akimsindikiza mwanafunzi wa kike mwenye mfuko wa madaftari.

Tangu mwaka 2005 ambapo masuala mazito ya rushwa yamekuwa yakiibuliwa, ikiwamo ununuzi wa rada feki, wizi wa fedha za umma kutoka kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), mkataba tata wa Richmond, ukusanyaji wa kodi, utoroshwaji wa wanyama hai, wizi wa nyara za serikali, ikiwamo pembe za ndovu, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituhumu serikali kushindwa kuchukua hatua.

Vilevile, wananchi wamekuwa wakituhumu Serikali ya Kikwete, kukumbatia wezi wa fedha za umma katika halmashauri za miji na wilaya, uporaji wa ardhi unaofanywa na makampuni makubwa ya ndani na nje ya nchi.

Jana, Tanzania Daima Jumamosi haikufanikiwa kumpata Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu kuzungumzia iwapo serikali ina taarifa juu ya jambo hili kwa kuwa simu yake ilikuwa ikiita muda wote bila kupokelewa.

Kova ajivua
Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, Suleiman Kova jana ametangaza rasmi kujivua katika sakata zima la kuchunguza kutekwa na kuteswa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Ulimboka.

Aidha, Kova pia amekanusha madai ya kuunda tume kuchunguza suala hilo, akitaka asiulizwe jambo lolote, huku akisukuma tukio hilo kwa wakubwa wake.

Juzi, Kamanda Kova aliliambia Tanzania Daima kwamba, jana angeweka wazi suala hilo ili Watanzania wajue kilichojiri kuhusiana na kutekwa na kuteswa kwa Dk. Ulimboka, jambo ambalo limetikisa anga, likiwemo lile la kukamatwa kwa raia wa Kenya, Mulundi anayedaiwa kuhusika na tukio hilo.

Hata hivyo, kinyume na matarajio ya wengi, jana Kamanda Kova aliruka kimanga na kudai kwamba wenye uwezo wa kulitolea maelezo ni wakuu wake wa kazi, kwa maana ya Ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.

Kuhusu kuundwa kwa kamati ya kuchunguza utekaji huo, Kova alisema kilichofanyika wakati huo ni kuundwa kwa jopo la uchunguzi ambalo taarifa zake hazina ulazima wa kutolewa mbele ya jamii zaidi ya kutumika kwa ajili ya utekelezaji wa kile walichokibaini.

Alisema baada ya kukamilisha kazi yake, alipeleka jukumu la kupeleleza sakata hilo katika ofisi ya mkurugenzi wa makosa ya jinai nchini (DCI) ambayo ndiyo yenye jukumu la kutoa maelezo.

Chanzo: Tanzaniadaima 12 Jan, 2013.
Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

www.wejobs.blogspot.com Jobs in Africa
www.jobsunited.blogspot.com International Job Opportunities

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
0 comments:

Post a Comment